ZOEZI la kuokoa watu wote kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko katika mkoa wa Lindi limekamilika.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,
christopher Ngubiagai, amesema kuwa maeneo kama ya mto mkulu, Makangaga, Nakiu, Nakangaga, Kigongo na Nanjilinji ni maeneo yaliyokuwa hayafikiki kwa urahisi lakini kwa saivi yanafikika.

Hata hivyo Ngubiagai amesema kuwa wote waliokumbwa na mafuriko hayo wameshapatiwa msaada wa kibinadamu na wapo katika maeneo salama ya kuishi.

"Kuna watu zaidi ya 500 ambao walikuwa bado hawajafikiwa kutokana na ukubwa wa mto mwinyi mkuu ulivyo, lakini sasa hivi zoezi la kuwaokoa limekamilika, wote wameshafikiwa kwa kupelekwa na fiber boti na kuwatoa watu, kwenye maeneo hayo". Amesema Ngubiagai.

Amesema maeneo yaliyokuwa yanaleta usumbufu mkubwa kwa kutokufikika ni maeneo ya bonde la mto Mkulu, maeneo Makangaga maeneo ya vitongoji Kigombo, Nanjilinji, Likawage na Kiu.

Hivyo Ngubiagai amewaomba wadau wa kilimo kupeleka mbegu za muda mfupi na za kisasa ili wananchi pamoja na misaada wanayoipata baadae waweze kujitegemea wenyewe.

"Michango tunayoipata sasa iendane na mbegu bora na tuweze kusambaza kwa wananchi kusudi waweze kuzilima katika maeneo yao".

Amesema kuwa endapo mbegu hizo zitawafikia kwa wakati wanaweza kupunguza mzigo kwa serikali.

"Leo tumepata chakula cha kutosha kupatia wananchi hawa watu hawa, kesho na keshekutwa watu hawa wanahitaji chakula ili waweze kuishi na familia zao".

Hivyo wadau na taasisi mbalimbali wawawezeshe wananchi wa Mkoa wa Lindi kwa mbegu za mazao bora na za kisasa ili waendeleze maisha yao katika kaya zao.

Mvua nyingi zilikuwa zinanyesha zaidi katika mikoa mbalimbali hapa nchini huku Mkoa wa Lindi umepoteza zaidi ya watu 20 kwa mafuriko ya mvua kuzidi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe.christopher Ngubiagai

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...