Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KUFUATIA taarifa zinazozunguka katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na upimwaji wa ujauzito kwa wanafunzi wa kike shuleni Wizara ya Elimu imetoa tamko la ufafanuzi kuhusiana na jambo hilo kwa kueleza kuwa taarifa hiyo sio rasmi kutoka Wizarani.

Taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu Dkt. Leonard Akwilapo imeeleza kuwa hakuna sera au utaratibu unaoruhusu wakuu wa shule au mamlaka zozote zinazoruhusiwa kuwapima wanafunzi wa kike ujauzito.

Imeelezwa kuwa hata tatizo hilo likiwa limegundulika kinachotakiwa ni muda wa kukilinda kiumbe na baadaye mama kupata nafasi ya kuendelea na masomo yake kwa njia mbadala zilizowekwa.

Aidha imeelezwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina utaratibu maalumu wa kuwasaidia watoto walioacha shule kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupelekwa katika vituo vya Elimu ya Watu Wazima, Vyuo vya Maendeleo ya wananchi na Taasisi za Elimu ya Ufundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...