Mkuu Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni akiwa katika picha ya pamoja katika maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika katika viwanja vya Leader’s Club jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Taasisi wa Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni akimkabidhi moja kifaa tiba Mratibu wa Huduma Tiba wa Hospitali ya Palestina-Sinza Dkt.Nchang’wa Nhumba wakati walipokwenda kutoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Mkuu wa Taasisi wa Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa tiba katika hospitali ya Palestina-Sinza katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Mratibu wa Huduma Tiba wa Hospitali ya Palestina-Sinza Dkt.Nchang’wa Nhumba akizungumza mara baada ya kupokea vifaa tiba kutoka Taasisi ya Ustawi wa Jamii.
Baadhi ya wanawake wa Taasisi ya Ustawi Ustawi wa Jamii wakiwa katika Hospitali ya Palestina wakati walipopeleka msaada wa vifaa tiba katika hospitali hiyo.
Sehemu ya Vifaa Tiba vilivyotolewa katika Hospitali ya Palestina na Wafanyakazi Wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAFANYAKAZI Wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii imetoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali katika hospitali ya Palestina-Sinza ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutambua kama wanawake wanawajibu wa kuunga mkono serikali katika sekta ya afya.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa tiba hivyo Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni amesema kuwa vifaa tiba hivyo vimetokana na mchango wa wananwake wa Taasisi hiyo kwa kuamini wanawake tunaweza.

Amesema kuwa vifaa tiba walivyotoa wanaamini kuwa vitasaidia katika mahitaji ya Hospitali kwa kuhudumia wagonjwa wanaofika hapo.

“Sisi wanawake tunaweza ndio maana baada ya kutambua siku ya wanawake duniani inakuja tukajichanga kutoka mifukoni mwetu ili kuweza kufikia azima ya kununua vifaa tiba na kufikisha katika hospitali ili ndugu,jamaa na watoto wanaofika kuweza kutumia”amesema Dkt.Nyoni.

Nae Mratibu wa Huduma Tiba wa Hospitali ya Palestina-Sinza Dkt.Nchang’wa Nhumba amewapongeza wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa kutambua Palestina wanahitaji msaada kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wanaofika katika hospitali hiyo.

Dkt.Nhumba amesema kuwa Wanawake wa Ustawi wa Jamii waendelee kuwa na moyo huo hata wakati mwingine waweze kwenda kusaidia na kuongeza kuwa wanawake wa Taasisi zingine kuiga mfano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...