Na Francis Godwin, Iringa
MAHAKAMA
ya hakimu mkazi Iringa imeondoa mahakamani hapo shauri dogo namba
5 la mwaka 2020 lililofikishwa katika mahakama hiyo na mstahiki meya
wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupitia chama cha demokrasia na
maendeleo (CHADEMA ) Alex Kimbe ya kupinga mchakato wa madiwani wa
chama cha mapinduzi (CCM) kutoka kumung'oa katika nafasi yake ya umeya
kwa tuhuma mbali mbali zikiwemo za matumizi mabaya ya madaraka.
Akisoma
hukumu ya kesi hiyo leo hakimu mkazi wa mahakama Iringa Aden
Kanje alisema kuwa maombi yaliyofikishwa mahakamani hapo na
mlalamikaji huyo Alex Kimbe ambae katika kesi yake hiyo alikuwa
akitetewa na wakili Barnabans Nyalusi vifungu ambavyo vilitumika
kufikisha maombi hayo vilikuwa vimekosewa .
Hakimu
huyo alisema kuwa hoja za upande wa wakili wa serikali alidai
kuwa hoja za mleta maombi mahakamani hapo hazikuwa zimezingatia
vigevyo vya kisheria hivyo aliomba mahakama hiyo kutupilia mbali
maombi hayo ya Kimbe kutokana na kutokidhi vigezo vya kisheria pia
aliomba kupewa gharama alizozitumia katika kufanya utafiti juu ya
shauri hilo kutoka kwa mleta maombi mahakamani hapo
Wakati upande wa wakili wa mleta maombi mahakamani hapo Barnabans
Nyalusi aliomba mahakama hiyo kutoa zuio la kumng'oa meya huyo
madarakakani kwa madai kuna taratibu ambazo zinapaswa kufanyika kabla
ya kumwondoa meya huyo madarakani .
Pamoja
na nne ambazo zilitolewa na wakili wa serikali katika kupinga
maombi hayo kusikilizwa na hoja zilizotolewa na wakili mlalamikaji
juu ya kupinga hoja za wakili wa saerikali mahakama hiyo
imelitazama suala hilo kisheria na kitaratibu za kimahakama na kuona
hoja za upande wa wakili wa serikali zina mashiko na kuwa hiyo
haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo la kuzuia kumng'oa meya
madarakani .
Kwani
imeona maombi yake yalitokana na hisia za mwombaji wa zuio hilo kuwa
yawezekana yasingefanyika hivyo na kimsingi mahakama kifungu
kilichotumiwa na mleta shauri hilo mahakamani kilikuwa na makosa ya
kisheria .
Alisema
kuwa kifungu namba 2(3) kilichotumiwa ni kifungu kinachosimamia
masuala ya sheria na mahakama ( Judicature and Apllication of Laws (
JALA ) kuwa pamoja na kifungo namba 95 na 68 (E) vya sheria ya
mwenendo wa mashauri ya madai .
Kuwa
mahakama hiyo haipati nguvu ya kimaamuzi katika shauri hilo hilo
hivyo kwa msingi huo maombi hayo yamekosa nguvu za kisheria hivyo
mahakama imelazimika kuyaondoa mahakamani hapo na rufaa ipo wazi
ndani ya siku 45 kwa upande wowote ambao utakuwa haujaridhika na
uamuzi huo wa mahakama kuwa Mahakama inaliondoa shauri hili kwa
gharama za uendeshaji wa kesi kwa upande uliopoteza .
Akizungumza
na wanahabari nje ya mahakama hiyo baada ya hukumu hiyo kutolewa
wakili Nyalusi alisema kuwa anakubaliana na uamuzi wa mahakama na
kuwa ambacho atakifanya ni kwenda kuziangalia hoja ambazo
zimetolewa na mahakama katika hukumu hiyo ili kuona namna ya kurudi
mahakamani hapo .
"
Hakimu hajafuta kesi kwa kutumia vifungu ila amesema vifungu
ambavyo sisi tumevitumia kuombea maombi yetu si sahihi yeye
ametoa kifungu ambacho lazima tukakisome na kuona maana zipo kesi
ambazo zimesikilizwa na mahakama kuu na kutumiwa kifungu hicho hicho
alichokitoa yeye tunaamini tutakwenda kusoma na tutashauriana
vizuri na hii sio mwisho " alisema wakili Nyalusi .
Hata
hivyo alisema kuwa wao walikuwa wanazuia mchakato wa kumuondoa meya
madarakani sio kuzuia meya kuondolewa kwa kuamini kuwa mchakato huo
haukufuata sheria maana kanuni za Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa zinaeleza wazi ili meya aondolewe kuna taratibu za kufuata
ila hazikufuatwa na kwa kuwa kilichojadiliwa mahakamani si maombi
yao ya msingi ila kilichojadiliwa na kutolewa maamuzi ni taratibu sio
hoja zao .
Hata
hivyo hivyo alisema kuwa hawezi kusema zaidi juu ya maamuzi ya
mahakama ila wanakwenda kujipanga zaidi maana hoja zao za msingi
mahakama hiyo haijaweza kuzigusia kabisa zaidi ya kutolea uamuzi
taratibu wa za ufikishaji wa maombi hayo mahakamani hapo .
Kuhusu
kuendelea kwa mchakato wa vikao vya kutaka kumwondoa meya madarakani
alisema kuwa wao hawajui kwanini mchakato huo unaendelea kwani
kimsingi kesi inapokuwepo mahakamani watu wenye hekima huwa
wanasimamisha shughuli zote ila wanashangaa kuona mchakato
ukiendelea kuitwishwa .
Shauri
hilo la mstahiki meya Kimbe kwenda mahakamani kupinga mchakato
huo wa kumwondoa lilifikishwa mahakamani hapo Machi 17 kabla ya jana
Machi 27 kutolewa maamuzi na mahakama hiyo japo wakati mahakama
meya huyo akiwa mahakamani hapo mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Iringa Himid Njovu ameitisha kikao cha dharua cha baraza la
madiwani kitakachofanyika leo baada ya kikao kama hicho kilichokuwa
na ajenda ya kumung'oa meya kushindwa kufanyika juzi kwa kukosa
mahudhuria ya wajumbe 17 ambayo ni therufi mbili ya wajumbe 26
ambao walipaswa kufika katika kikao hicho na badala yake kufika
wajumbe 15 pekee .
Kabla
ya kuanza kwa kikao cha juzi ambacho kiliahirishwa mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Njovu alisema kuwa
ili kikao hicho kiweze kuendelea kwa mujibu wa kanuni namba
9,2 kanuni ya kudumu ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
za 2015 zinaeleza kwamba akidi ya wajumbe wa mkutano maalum wa
Manispaa hiyo itakuwa ni therufi mbili ya wajumbe wote na
itahesabiwa wakati wa ufunguzi wa mkutano .
“ Kwa kanuni hiyo naomba ndugu mwenyekiti na CC (katibu wa kikao) wetu atuhesabie wajumbe waliopo katika mkutano huu na therufi mbili ya wajumbe wa mkutano huo na therufi mbili ya wajumbe 26 wa baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni wajumbe 17 na kama idadi hiyo itatimia basi mwenyekiti atafungua mkutano huo ili uendelee na kama idadi haitatimia basi mwenyekiti na baraza lake atatoa maamuzi atakayoona yanafaa” alisema Njovu na kukaa chini .
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe (mwenye shati jeupe kushoto)akiwa na wakili wake na viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wakitoka mahakama ya makimu mkazi Iringa baada ya mahakama hiyo leo kuondoa kwa gharama shauri la meya kupinga mchakato wa kuondolewa madarakani na madiwani wa CCM picha na Francis Godwin
:Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe kulia akiongea na wakili wake Barnabans Nyalusi baada ya mahakama ya hakimu mkazi Iringa kuondoa mahakamani hapo shauri lake la kupinga mchakato wa kumwondoa madarakani (Pic ha na Francis Godwin.
Picha nyingine meya akiwa na wafuasi wa chadema Iringa waliomsindikiza mahakamani hapo
“ Kwa kanuni hiyo naomba ndugu mwenyekiti na CC (katibu wa kikao) wetu atuhesabie wajumbe waliopo katika mkutano huu na therufi mbili ya wajumbe wa mkutano huo na therufi mbili ya wajumbe 26 wa baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni wajumbe 17 na kama idadi hiyo itatimia basi mwenyekiti atafungua mkutano huo ili uendelee na kama idadi haitatimia basi mwenyekiti na baraza lake atatoa maamuzi atakayoona yanafaa” alisema Njovu na kukaa chini .
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe (mwenye shati jeupe kushoto)akiwa na wakili wake na viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wakitoka mahakama ya makimu mkazi Iringa baada ya mahakama hiyo leo kuondoa kwa gharama shauri la meya kupinga mchakato wa kuondolewa madarakani na madiwani wa CCM picha na Francis Godwin
:Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe kulia akiongea na wakili wake Barnabans Nyalusi baada ya mahakama ya hakimu mkazi Iringa kuondoa mahakamani hapo shauri lake la kupinga mchakato wa kumwondoa madarakani (Pic ha na Francis Godwin.
Picha nyingine meya akiwa na wafuasi wa chadema Iringa waliomsindikiza mahakamani hapo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...