Katibu wa CCM Wilaya ya Mbarali  akimkabidhi fomu ya Kugombea Ubunge Kada wa CCM Yunus Msanguka zoezi  la uchukuaji zimefanyika katika ofisi ya wilaya Mbarali mkoani Mbeya.


Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

Kada wa Chama cha  Mapinduzi  (CCM) Yunus Msanguka amechukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Mbarali

Akizungumza na Mwandishi wa Michuzi TV kwa njia ya Simu mara baada ya kuchukua fomu Msanguka  amesema amefikia uamuzi huo kutokana na katiba ya chama inamruhusu na  kuweza kuwatumikia wananchi atapopitishwa na chama hicho.

Amesema moyo wa kujituma katika chama anao hivyo atapoteuliwa  atakwenda kuwatumikia Wanambarali katika maendeleo.Amesema kuwa anachosubiri sasa ni  mchakato ndani ya chama akipita hapo ni kuipeperusha bendera ya chama hicho.

Amesema uwezo anao wa kupeperusha bendera hiyo kutokana na kuwa karibu na wananchi wa Jimbo hilo.Aidha, amesema kuwa kazi ni kuendeleza mazuri zaidi kutokana na sera za Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya kuwainua wanyonge.

Msanguka amesema Ukonga  akipita ataenda kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi."Nikiteuliwa ndani ya Chama kazi yangu itakuwa ni  kupigania maendeleo ya wanambarali  kwa  kauli mbiu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kwenda kisasa zaidi  kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa kasi"amesema Msanguka

Hata hivyo, amesema kama kijana amekuwa na maono mengi ya kutaka vijana kuinuka kiuchumi katika kuwaunganisha kwenye fursa wanambarali

Hata hivyo, amesema kama kijana amekuwa na maono mengi ya kutaka vijana kuinuka kiuchumi katika kuwaunganisha kwenye fursa zilizopo  wanambarali .

Msanguka ambaye pia m wa habari mkongwe amechukua fomu Ofisi za CCM Wilaya ya Mbarali zilizopo Rujewa mkoani Mbeya Jumatano tarehe 15 Julai 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...