Mgombea kura za maoni CCM Dr. Suzan Kolimba akisoma fomu ya kuomba ridhaa ya  nafasi ya ubunge jimbo la Ludewa
 Mgombea kura za maoni CCM Dr. Suzan Kolimba akipokea fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Ludewa
 Mhadhiri Chuo kikuu huria makao makuu Evaristo Mtitu akipokea fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge jimbo la Ludewa
 Mgombea kura za maoni CCM Goodluck Mgaya akipokea fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Ludewa
 Mgombea  kura za maoni CCM Injinia Alfales Chengula akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge jimbo la Ludewa
 Mgombea kura za maoni CCM Baraka Lucas akipokea fomu ya kuomba ridhaa kugombea ubunge jimbo la Ludewa
Mgombea kura za maoni CCM Deogratius Nchimbi akipokea fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge jimbo la Ludewa



Na Shukrani Kawogo, Njombe.

Wagombea kura za maoni katika nafasi ya ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  jimbo la Ludewa waendelea kumiminika katika ofisi za chama wilayani Ludewa mkoani Njombe akiwemo aliyekuwa mbunge wa viti maalum Dk. Suzan Kolimba na kufikisha idadi ya watu 20.

Zoezi hilo ambalo lilianza siku ya jana ambapo walijitokeza wagombea 12 na siku ya leo ni ya pili ambapo wamejitokeza wagombea 8 na kufikisha idadi hiyo ya watu 20.

Akizungumza na wanahabari baada ya kuchukua fomu Dk. Kolimba amesema kuwa ameamua kuchukua fomu ya kugombea jimbo ili kuongeza kasi  ya maendeleo ndani ya jimbo hilo.

Aidha kati ya wagombea 8 waliojitokeza katika siku ya pili ya uchukuaji fomu wawili ni vijana wa umri wa miaka 27 ambao ni Goodluck Mgaya pamoja na Injinia Alfales Chengula.

Wagombea hao waliochukua fomu kwa siku ya jana na leo ni
 1.Dr.Primus Nkwera
2.Deo Ngalawa
3.Fikiri mgina
4.Joseph Kamonga
5.Dr.Luka Mkonongwa
6.Mwl.Helmani Yanga
7.Dr.Philipo Philikunjombe
8.Crodwick Mtweve 
9.Dr.Neema Mturo
10.Christopher Magogo
11.Lenatus Njelekela
12.Gerecius Lugome
13. Alfales Chengula
14.Barnabas Mhagama
15.Baraka Lucas
16. Dr.Suzan Kolimba
17. Deogratius Nchimbi
18. Augustino Ngailo
19. Evaristo Mtitu
20. Goodluck Mgaya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...