Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (katikati aliyevaa koti ya blue) akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (aliyevaa koti jeupe kushoto) wakipata maelekezo ya Utendaji kazi wa Kiwanda cha saruji Camel Cement kutoka kwa mfanyakazi wa kiwanda hicho. Mbagara, jijini Dar es salaam, Tarehe 04,Augosti 2020 {picha zote na Eliud Rwechungura}
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (aliyevaa koti ya blue) akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (aliyevaa koti jeupe kushoto) walipokuwa kwenye Kiwanda cha saruji Camel Cement kukagua utendaji Kazi wa kiwanda hicho. Mbagara, jijini Dar es salaam,
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (aliyevaa koti ya blue) akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (aliyevaa koti jeupe kushoto) wakipata maelekezo ya Utendaji kazi wa Kiwanda cha saruji Camel Cement kutoka kwa mfanyakazi wa kiwanda hicho. Mbagara, jijini Dar es salaam

………………………………………………………………….

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe kutembelea na kukagua utendaji Kazi wa Kiwanda cha saruji Camel Cement kilichopo Mbagara jijini Dar es salaam.

Katika ziara hiyo Waziri Bashungwa amebainisha lengo na Madhumuni ya kutembelea viwanda vya saruji nchini ni baadaa ya kupata fursa na maombi ya uhitaji wa saruji kutoka nchi jirani za uhitaji wa saruji kutoka Tanzania.

Waziri Bashungwa ameanza kwa kuvipongeza viwanda vya saruji nchini kwa kazi kubwa ya uzalishaji wa saruji inayotosheleza mahitaji ya nchi na nyingine kusafirishwa nje ya nchi na sasa mkakati wa wizara ni kuhakikisha viwanda vyote vya saruji vinazalisha kufikia uwezo wao uliosimikwa na kama kuna changamoto zinazozuia viwanda visifikie uzalizaji uliosimikwa ziweze kutatuliwa mara moja maana ndio kazi ya serikali kwa wawekezaji wote nchini.

Aidha, Waziri Bahungwa amevihakikishia viwanda vyote nchini juu ya tatizo la umeme kuwa mpaka sasa mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere upo katika hatua nzuri na muda si mrefu tatizo hilo litakuwa hisitoria na tutakuwa na uhakika wa umeme wa kutosha na unaopatikana muda wote ili dhima ya Rais John Pombe Magufuli ya Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya yenye uchumi wa Viwanda iweze kutimia na kutekelezwa kiurahisi.

Sambamba na hayo, Waziri Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe kukutana na wenye viwanda vya saruji ili kuweka mkakati wa kujenga viwanda vya saruji kwenye mikoa ya kati na kanda ya ziwa au kati maana sio lazima kujenga kiwanda sehemu ambapo zinapatikana malighafi zote

Bashungwa amemaliza kwa kuwakaribisha wawekezaji wapya na waliopo kuwekeza kwenye viwanda vya saruji katika mikoa ya kati na kanda ya ziwa maana teknolojia na miundombinu vimeboreshwa na vinaruhusu mwekezaji kujenga kiwanda mkoa wowote maana malighafi zinaweza kufika tena kwa bei rahisi na rafiki kwa wawekezaji kwa sababu kuna mikoa iko mbali na viwanda vilipo mpaka umbali wa kilometa 1000 na baada ya kusafirisha saruji sasa tusafirishe malighafi ili viwanda vijengwe huko huko.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe kutembelea na kukagua utendaji Kazi wa Kiwanda cha saruji Camel Cement kilichopo Mbagara jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...