Mwenyekiti wa Uchaguzi MNH-Mloganzila Bw. Julius Hhara akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa kwa wagombea wa nafasi mbalimbali.
Viongozi wa TANNA-Taifa katika picha ya pamoja na viongozi wa TANNA-
tawi la MNH-Mloganzila.
Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi-TANNA Taifa, Bi. Kulwa Kaombwe (kushoto) akiwa na Katibu wa Tume ya Uchaguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, Sr. Kanaeli Uriyo wakiwasikiliza wagombea wa nafasi mbalimbali wakijinadi wakati wa kuomba kura.
Bi. Mpoki Senje akijinadi wakati wa kuomba kura katika nafasi ya katibu
mwenezi wa chama hicho.
Baadhi ya wanachana wa TANNA-Mloganzila wakisikiliza sera za wagombea
wakijinadi wakati wa kuomba kura.
Msimamizi wa Uchaguzi kutoka TANNA-Taifa, Bi. Jema Kajange na viongozi wa kamati ya uchaguzi MNH-Mloganzila wakihesabu kura.



……………………………………………………………..
Wajumbe wa Chama Cha Wauguzi Tanzania (TANNA) tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila wamefanya uchaguzi rasmi wa viongozi kujaza nafasi nanekatika ngazi ya mwenyekiti, katibu, mweka hazina, katibu mkuu mwenezi pamojana wasaidizi wao lengo ikiwa ni kupata viongozi watakaosaidia kuendesha tawihilo jipya lenye wanachama takribani 200.

Kati ya vipaumbele vilivyonadiwa ni pamoja na kuboresha sera za 
kusimamiautendaji kazi wa wauguzi, kuitangaza vema taaluma hiyo, kudumisha umoja naushirikiano baina yao na watumishi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini yaanikwenye vitongoji hadi kimataifa na kuielimisha jamii juu ya majukumu namchango wao katika kutoa huduma bora.
 
Akizungumza wakati wa uchaguzi huo Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi-TANNA
Taifa ambaye pia kitaaluma ni Afisa Muuguzi Mwandamizi, Bi. Kulwa Kaombweamesema taaluma ya uuguzi inahitaji ushirikiano sana baina ya wauguzi na Serikaliau waajiri wao ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa jamii.

“Ili taaluma hii izidi kusonga mbele na kuwawezesha wauguzi kufanya kazi kwaufanisi inahitaji wauguzi kushirikiana bega kwa bega na waajiri wao ili
kuwawezesha kutoa huduma bora kwa jamii” amesema Bi. Kaombwe.
Aidha Bi. Kaombwe ameushukuru uongozi uliopita kwa kusimamia vizuri tawihilo kwa kipindi cha miaka miwili tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018 likiwa naidadi ya wanachama hai 55.

Kwa upande wake Mwenyekiti aliyechaguliwa kuongoza tawi hilo, Bw. WilsonFungameza amewashukuru wajumbe kwa kumchagua kuongoza nafasi hiyo nakutoa rai kwa wanachama, viongozi wenzake pamoja na Uongozi wa TANNA-Taifa kushirikiana kwa ajili ya kusongesha mbele gurudumu la taaluma ya uuguzi.

Miongoni wa majukumu ya viongozi hao ni pamoja na kutunza kumbukumbu zawanachama, kuhamasisha wauguzi kujiunga na chama, kusimamia mapato namatumizi ya chama ambayo yanatokana na michango ya kila mwezi yawanachama, wafadhili na marafiki wenye mapenzi mema na chama hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...