Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

BAADHI ya wanasayansi wanaamini kuwa  mtu huzaliwa mara ya pili baada ya kufa kwake na wanasema kuwa John Kennedy F. Rais wa 35 wa Marekani  na Abraham Lincoln Rais wa 16 wa Marekani  ni  mtu mmoja aliyeishi katika nyakati mbili ila katika muonekano tofauti.

Pia baadhi ya wanahistoria wanaeleza kuwa mara nyingi historia hujirudia kwa maana historia ya mtu mmoja inaweza kujirudia  kwa mtu mwingine kama ilivyo.

Kuna mengi ambayo yanafikirisha juu ya maisha ya Lincoln na Kennedy, na hayo ni pamoja na ;

Abraham Lincoln alijiunga na chama cha Congress mwaka 1846 na
John F kennedy pia alijiunga na chama hicho mwaka 1946.

Lincolin alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 1860 na

Kennedy alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 1960.

Wake wa marais hawa wawili walifiwa na watoto wao wakiume wakiwa Ikulu. 

Lincoln aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa siku ya Ijumaa, 
Kennedy aliuawa pia kwa kupigwa risasi ya kichwa siku ya ijumaa na wote waliuwawa mbele ya wake zao.

Katibu wa Lincoln alimtahadharisha bosi wake asiende sinema na katibu wa Kennedy alimtahadharisha bosi wake asiende Dallas ambako mauti yaliwafika.

Lincoln alipigwa risasi kwenye jumba la sinema lililoitwa Ford na muuaji akakimbilia kujificha  ghalani na muuaji wa Kennedy alilenga risasi kutokea ghalani na kujificha kwenye jumba la sinema lililoitwa Lincolin lilijengwa na Ford.

Muuaji wa Lincolin aliuawa kabla hajafikishwa kwenye vyombo vya dola halikadhalika pia
 muuaji wa kennedy aliuawa kabla hajafikishwa kwenye vyombo vya dola.  

Pia marais hao wawili waliamini katika misingi ya  demokrasia na haki za binadamu hasa katika kukomesha biashara ya utumwa na usawa kwa wote.

Hata hivyo mrithi wa  Lincolin aliitwa Johnson huku mrithi wa Kennedy akiwa Johnson. 

Cha kushangaza zaidi Johnson Andrew aliyemrithi Lincolin alizaliwa mwaka 1808 na
Johnson Lyndon aliyekuja kumrithi kennedy alizaliwa mwaka 1908.

Mwisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...