*Dkt.Mtasiwa ahimiza wafanyakazi kutumia chombo cha Baraza la wafanyakazi.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV 
TAASISI ya Taifa ta Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imesema kuwa utafiti wa Ugonjwa wa Virusi vya Corona bado unaendelea na pale utakapokamilika watatoa taarifa watatoa .

Hayo ameyasema Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Profesa Yunus Mgaya wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi wa Taasisi hiyo, amesema kuwa licha ya kufanya tifiti ya ugonjwa wa virusi vya Corona wanaendelea kufanya tafiti mbalimbali.

Profesa Mgaya amesema kuwa kuundwa kwa Baraza hilo kutaongeza kufanya tafiti zaidi kwa maendeleo ya Taifa pamoja na Kimataifa.

“Tunaendelea kufanya tafiti mbalimbali na hili la ugonjwa wa virusi vya Corona tunaendelea kufanyia tafiti na pale utakapo kamilika tutatoa matokeo”amesema Profesa Mgaya.

Katika Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri NIMR Dkt.Deo Mtasiwa amesema kuwa wafanyakazi wanatakiwa kutumia chombo cha Baraza katika kushauriana masuala mbalimbali ikiwemo na masilahi ya wafanyakazi.

Amesema kuwa Baraza la Wafanyakazi moja ni kuhakikisha mipango ya Taasisi inafikiwa kwa kutambua wajibu na haki katika kufanikisha malengo na kuambiana ukweli pale wakati mmoja akiwa anafanya uzembe.

Mtasiwa amesema suala la maadili liendelee kusimamiwa na kuweza kufanya taasisi kuendelea kufanya utafiti ambao ndio kazi yenu kwa wananchi wa Tanzania kutokana na kuwa ubunifu wa taaluma zenu katika kufanya utafiti.

Aidha amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuondoa uzembe na vitendo vyovyote vya rushwa mahali pa kazi pamoja na kubana matumizi yasiyo na ulazima ili kuongeza tija katika kufikia malengo ya taasisi .

Katibu wa RAAWU Kanda ya Mashariki Mecky Humbo amesema kuwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi wanatakiwa kujua wajibu na haki zao pamoja kutambua umuhimu wao katika kusaidia Taasisi katika kufikia malengo.a upande wa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa NIMR Wilfred Mandara amewataka wajumbe kuzinduliwa kwa Baraza hilo ni kazi kwao katika kuhakikisha wanasaidia Taasisi kufikia malengo.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Kituo cha NIMR Mbeya Dkt. Nyanda Ntinginya amesema kuwa baraza la wafanyakazi kwa kila mjumbe anaweza kutoa mchango wa kufanya taasisi kufika mbali zaidi 

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Deo Mtasiwa  akizungumza wakati wa uzinduzi  wa Baraza la Wafanyakazi NIMR uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa  NIMR Wilfred Mandara akitoa maelezo ya mikakati ya baraza  kutoa ushauri kwa Taaisi katika kufikia malengo katika uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa NIMR na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Mkurugenzi NIMR Profesa Yunus Mgaya akitoa  maelezo juu ya kuanzishwa kwa baraza hilo na kuzinduliwa, jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Kituo cha NIMR  Mbeya Dkt. Nyanda akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi na namna watavyofanyia kazi maelezo ya viongozi wao.Katibu wa RAAWU Kanda ya Mashariki  Mecky Humbo akizungumza kuhusiana na utaratibu wa uendeshaji wa mabaraza ya wafanyakazi na miiko yake  katika uzinduzi wa baraza la  wafanyakazi NIMR uiofanyika uliofanyika jijini Dar es Salaam. Katibu wa RAAWU Kanda ya Mashariki  Mecky Humbo akizungumza kuhusiana na utaratibu wa uendeshaji wa mabaraza ya wafanyakazi na miiko yake  katika uzinduzi wa baraza la  wafanyakazi NIMR uiofanyika uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja mgeni Rasmi Dkt.Deo Mtasiwa viongozi waalikwa na Wajumbe wa wa Baraza la wafanyakazi
Baadhi ya wajumbe baraza katika uzinduzi wa baraza hilo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...