Charles James, Michuzi TV

TANZANIA imepiga hatua kubwa kwenye ukuaji wa uchumi ambapo ukuaji wa pato la Taifa lenyewe umepanda kutoka Sh Trilioni 52 kwa mwaka 2015 hadi Sh Trilioni 124 ndani ya miaka minne yaani 2015 hadi 2019.

Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbas leo jijini Dodoma alipokua akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya tano kwa kipindi cha miaka minne huku akilenga zaidi ukuaji wa kiuchumi.

Dk Abbas amesema katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dk John Magufuli, Tanzania imeweka rekodi ya kukuza pato la Taifa, ukuaji wa pato la mwananchi mmoja mmoja, kudhibiti mfumuko wa bei, ukuaji wa uchumi wenyewe na ongezeko la mapato.

Akizungumzia pato la Taifa, Dk Abbas amesema kwa takwimu za miaka minne limepanda zaidi ya mara mbili ya ikivyokua katika kipindi cha awamu ya nne na kuweka rekodi ya kuwa kubwa zaidi kulinganisha na awamu zote toka Uhuru.

" Ni wazi sasa GDP yetu ni kubwa kuliko kipindi chochote toka tupate Uhuru na hiyo imeifanya Nchi yetu kuwa miongoni mwa Nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika.

Malengo yetu katika kipindi cha miaka mitano ijayo tufanye kazi na kukuza zaidi pato la Taifa na hata hiyo 10 bora kuna Nchi ambazo miaka muda siyo mrefu tutazishusha na sisi kukaa juu yao," Amesema Dk Abbas.

Amesema ili pia ionekane kweli Nchi inapiga hatua ni lazima pia mafanikio hayo yaendane na ukuaji wa pato la mwananchi mmoja mmoja jambo ambalo serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kwani licha ya pato la Taifa kukua pia pato la mwananchi mmoja mmoja pia limepanda.

Amesema kwa kipindi cha miaka minne pato la mtanzania mmoja mmoja limeongezeka kutoka wastani wa Dola 622 sawa na Sh 979,000 kipindi cha awamu ya nne hadi Dola 1063 sawa na Sh Milioni 2.3 awamu hii ya tano.

Dk Abbas amesema hili ni ongezeko kubwa zaidi la pato la mwananchi mmoja mmoja katika historia ya Tanzania ambapo awamu ya kwanza ilikua ni Dola 190 (Sh1,895), awamu ya pili Dola 205 (Sh 46,722), awamu ya tatu Dola 331.2 (Sh 277,000), awamu ya nne Dola 622 (Sh 979,000) na awamu ya tano pato hilo likikua hadi Dola 1063 sawa na Sh Milioni 2.3.

" Ukuaji wa uchumi wenyewe umekua kulinganisha na awamu nyingine ambapo tumekua kwa asilimia 6.9 huku awamu ya kwanza uchumi ukikua kwa asilimia 3.1, awamu ya pili asilimia 3.0, awamu ya tatu asilimia 5.7, awamu ya nne asilimia 6.3 na sasa awamu ya tano katika kipindi chake cha kwanza tumepaa hadi asilimia 6.9.

Lakini pia ukusanyaji wa mapato umepaa zaidi kutoka Bilioni 850 kila mwezi Katika kipindi cha awamu ya nne hadi Sh Trilioni 1.9 licha ya hapa katikati kukutana na changamoto ya ugonjwa wa Covid19," Amesema Dk Abbas.

Amempongeza Rais Dk Magufuli kwa namna ambavyo serikali yake imefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei ambapo katika kipindi chake ameweka rekodi ya kupunguza mfumuko wa bei kutoka wastani wa asilimia 9.2 mwaka 2015 hadi asilimia 4.3 na kufanya mfumuko wa sasa kuwa mdogo kulinganisha na kipindi chote cha tangia Uhuru.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma kuhusiana na mafanikio ya serikali ya awamu ya tano hasa katika eneo la ukuaji wa uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...