Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ya timu Simba, Haji Sunday Manara akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitambulisha wiki ya Simba Day.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MABINGWA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho (ASFC), Simba SC rasmi imetambulisha matukio yake kuelekea kilele cha Simba Day itakayofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 22, 2020 badala ya Agosti 8 na itaitwa Wiki ya Mabingwa 'Champions Week'.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ya timu hiyo, Haji Sunday Manara amesema wiki ya Simba Day itazinduliwa kesho August 14, 2020 ambayo itaambatana na matukio yakiwemo uzinduzi wa Logo mpya ya timu, Jezi za msimu wa 2020-2021, utambulisho wa Wachezaji wapya.

Manara amesema wiki ya Simba Day pia itaadhimishwa kwa kufanya Utalii wa Ndani, kutembelea Watoto waishio Mazingira magumu, Dua maalum (Kisomo), usafi sehemu za fukwe za Bahari ya Hindi (Salander Bridge) na Mbunge, Mussa Azzan Zungu ikiwa chini ya udhamini wa Mo Extra, Kuchangia Damu.

Pia Manara amesema lengo lao kuifanya Simba SC kuwa timu kubwa zaidi miaka 10 ijayo kama ilivyo kwa timu za Bayern Munich ya Ujerumani, "Tunataka kwa kila watu 10, basi watu Tisa wawe wanashangilia Simba SC", amesema.

Amesema wanaiomba Serikali kulifanya tukio la Simba Day kuwa kama siku ya mapumziko, pia amesema shughuli ya mwaka huu itakuwa ya kipekee (Another Level) kutumia viwanja vyote viwili vya Uhuru na Uwanja wa Banjamin Mkapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...