WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba ameonya mawakili wa serikali na taasisi za umma wanaotengeneza mazingira ya kushindwa kesi zenye maslahi ya umma kuacha kufanya hivyo mra mona ama watahesabika kama wahujumu uchumi.

Dkt Nchemba ameyasema hayo leo Agosti 4, 2020  jijini Dar es Salaam alipotembelea ofisi za Wakili Mkuu wa Serikali.

Amesema maslahi ya watanzania lazima yalindwe hivyo, kusiwepo taasisi au wakili ambaye kwa makusudi anasababisha serikali inashindwa kesi kutokana na kuahidiwa kiasi fulani cha fedha.

"Vita ya kiuchumi inachezwa kisheria hivyo ni lazima tuhakikishe tunashinda kwa kulinda maslahi ya watanzania na wale waliozoea kutumia mbinu ovu tusiwaruhusu kuendelea nao," alisema Dkt. Mwigulu.

Aliongeza kuwa "taasisi na mawakili mnaokwamisha kesi zenye maslahi ya taifa kwa makusidi tutawahesabu kuwa wahujumu uchumi kwa sababu haiwezekani tushindwe kesi kwa sababu ambazo tunaziita za kitechnical ambazo tungeweza kuziepuka."

"Wapo mawakili wa serikali ambao huaidiwa kwa fedha ili serikali ishindwe kwenye mashauri,  jambo hilo halitakubalika, mawakili kuweni macho hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi kwani wapo vibaraka wanaojifanya kuangalia uchaguzi lakini wana malengo mabaya na nchi" amesema Nchemba.

Kwa upande wake, wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata amesema serikali imeokoa zaidi ya Sh trilioni 11.4 kwa miaka miwili kutokana na uendeshaji madhubuti wa mashauri ndani na nje ya nchi.

Amesema miongoni mwa fedha zilizookolewa zinatokana na  kushinda kesi mbalimbali ikiwemo ukamataji wa ndege za Shirika la Ndege nchini (ATCL), kesi zilizofunguliwa nchini Afrika Kusini na Canada.

Malata alisema endapo  wasingekuwa madhubuti katika usimamizi na uendeshaji wa kesi na mashauri mbalimbali, fedha hizo zingeweza kulipwa kwa watu wasiostahili jambo ambalo lingesababisha hasara kwa taifa.

"Tumekuwa tukisimamia  mashauri yote ya madai na usuluhishi ndani na nje ya nchi kwenye mahakama zote na mabaraza zinazohusu serikali kuu, serikali za mitaa, kampuni binafsi, taasisi na mashirika ya umma na kwamba serikali ilikuwa inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kulipa mawakili wa kujitegemea ili kuwawakilisha kwenye kesi mbalimbali nje ya nchi lakini baadhi walikuwa sio waaminifu na kusababisha serikali kushindwa", amesema Malata.

Ameongeza kuwa katika bajeti ya mwaka 2018/19 walipatiwa zaidi ya Sh bilioni 7.2 na kati ya hizo walitumia Sh bilioni 2.2 kwa ajili ya kuendesha mashauri nje ya nchi ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kusajili mashauri mbalimbali kielektroniki kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi na kuendesha mashauri kwa njia ya video conference.

Aidha aliongeza kuwa panoja na yote hayo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo pamoja na upungufu wa watumishi, ukosefu wa wataalamu wa uendeshaji mashauri ya usuluhishi ili kupambana na mawakili wa nje ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...