Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

MBALI na kutoa huduma ya Maji kwa wananchi, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) hukumbuka jamii ya wananchi wanaowahudumia kwa kurudisha sehemu ya makusanyo yao kwa jamii zenye uhitaji.
Hivi karibuni Dawasa wametoa msaada wa mahitaji ya kibinadamu kwa kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu katika mji wa Kisarawe mkoani Pwani.

Kituo hicho cha Kisarawe Orphanage Centre kina jumla ya watoto takribani 29 kutoka maeneo mbalimbali.

Akizungunza kwa niaba ya Kituo hicho, Afisa Ustawi wa Jamiii Kisarawe Teofrida Mbilinyi amesema kituo hicho kinalea watoto wa aina tofauti na sio Yatima peke yake.

Teofrida amesema, wana watoto waliokuwa wanaishi kwenye mazingira magumu, watoto walio na kesi ambao hawawezi kulala mahabusu na wale waliofanyiwa ukatili wa kijinsia.

"Kituo hiki kinalea watoto wa aina mbalimbali, sio yatima peke yake bali hata sisi tunakiamini na huwa tunaleta watoto waliokuwa na kesi ambao hawawezi kulala mahabusu, waliofanyiwa ukatili wa kijinsia na hata wale tuliowaokota sehemu tofauti tofauti" amesema.

"Mmiliki wa kituo hiki anatambulika, tunashirikiana nae na hata yeye ndiye anayemleta mtoto (mtuhumiwa) kwenye kesi yake na pia anatambulika kisheria," ameeleza Teofrida.

Mmiliki wa Kituo hicho, Veronica Kilango ameeleza kituo hicho kilianza mwaka 2012 na alirithi kazi hiyo kutoka kwa baba yake na alianzia kwenye nyumba ya kupanga hadi sasa amepata eneo la kudumu.

Veronica amesema, wana watoto jumla 29, wanaoanzia elimu ya awali hadi kidato cha Sita ila wapo ambao walipita hapo na wapo Vyuoni huku wengine wakisomea fani za ufundi.

"Tunawashukuru sana Dawasa, nilipoambiwa wanakuja tulifarijika sana ujio wenu ni mzuri, mmeonesha moyo leo naamini watoto watafurahi kwa hiki mlichotuletea," amesema Veronica.

Kwa upande wa Dawasa Meneja wa Dawasa Kisarawe ,ndugu Erasto Mbwambo amesema wametoa mchango huo kwa kituo hicho ili kiwasaidie watoto hao ambao ni mwanzo kwani Kwa sasa Dawasa wanatoa huduma ya Majisafi wilaya ya Kisarawe.

Kwa upande wa msimamizi wa kituo ameongez kuwa kwasasa pia wanafanya shughuli mbalimbali za mikono ikiwemo kutengeneza asali, mafuta ya mnyonyo, viatu vya ngozi na kutengeneza mabatiki ili kuweza kujiendesha na kuweza kuhudumia watoto kituoni hapo.

Dawasa wametoa msaada ya kibinadamu na mahitaji mengine muhimu kwa kituo hicho yenye thamani zaidi ya milioni mbili ambazo ni Mchele, unga wa sembe, maharage, mafuta ya kula, Sukari, chumvi na sabuni za kufulia.

Dawasa inatoa huduma ya majisafi katika wilaya ya kisarawe baada kukamilika kwa mradi mkubwa wa majisafi uliogharimu zaidi ya Bilioni 10.6 ambao ulizinduliwa mapema mwaka huu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli.

Mmiliki na Mlezi wa Kituo cha Kisarawe Orphanage Centre Veronica Kilango (kulia) akipokea msaada wa Chakula kutoka kwa Meneja wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Kisarawe Erasto Mbwambo (wa pili kushoto) na Afisa Mawasiliano Dawasa Joseph Mkonyi (wa pili kulia) wakushuhudiwa na Afisa Ustawi wa Jamij Kisarawe Teofrida Mbilinyi (kushoto) baada ya kutembelea kituo hicho leo Kisarawe, Mkoani Pwani.

 Afisa Mawasiliano Dawasa Elizabeth Eusebius akipata maelezo  ya bidhaa zinazotengenezwa na watoto wa Kituo cha Kisarawe Orphanage kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii Kisarawe Teofrida Mbilinyi, Dawasa wametembelea kituo hicho kilichopo Kisarawe Mkoani Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...