Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt Benhajj Shaaban Masoud akimkabidhi Cheti cha ushiriki Hakimu Mkazi Mhe. Edga Edom Mwaiswaga baada ya kumaliza mafunzo hayo.

1. Mhe. Dkt. Paul F. Kiwelo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama awasilisha mada katika mafunzo hayo

 

     Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.Dkt Benhajj Shaaban Masoud akifunga Mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kwa Wasaidizi wa Sheria wa Majaji yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.


Na Rosena Suka, IJA-Lushoto

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Benhajj Shaaban Masoud amewataka Wasaidizi wa Sheria wa Majaji wa Mahakama ya Rufani kutumia vyema elimu ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi ili kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya sheria na haki nchini.

Akifunga rasmi Mafunzo hayo hivi karibuni yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Jaji Dkt Masoud aliwaeleza washiriki kwamba, imani ya wananchi ni kuwa, Mahakama ni mahali pa kupata haki, hivyo basi Maafisa wa Mahakama wanatakiwa kutambua muhimu walionao kwa wananchi wanaowahudumia.

 “Ninawasihi sana kujiepusha na rushwa, kataeni rushwa, kemeeni rushwa na toeni elimu pale mnapopata nafasi na uwezo wa kufanya hivyo juu ya madhara ya rushwa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi”

Aidha, aliendelea kwa kuwaomba Maafisa hao kufanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ili kutekeleza majukumu anayopewa Jaji husika kwa wakati na pia kwa viwango bora.

Kwa upande mwingine, Mhe. Dkt Masoud aliwapongeza wawezeshaji wa mafunzo kwa jinsi walivyoendesha mafunzo hayo kwa umahiri mkubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...