Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amemjibu mgombea urais wa kupitia Chadema Tundu Lissu kuwa ni muongo mkubwa na amekuwa akipotosha ukweli kuhusu vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo 'Machinga'.

Tundu Lissu akiwa katika moja ya mkutano wake wa kampeni amesikika akieleza fedha za vitambulisho vya Wamachinga ambazo ni Sh.20,000 kwa mwaka CCM ndio wamezitumia kununulia magari yao, ambapo Polepole ameamua kumtolea uvivu na kueleza ukweli ili umma watanzania wajue na kisha wampumze.

Akizugumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Polepole amesema mgombea huyo wa Chama cha Mbowe akiwa na maana ya Chadema ni mtu muongo sana.

"Hivi naomba kuuliza hivi TRA peke yake inakusanya fedha nchini"Tuanzie hapo, hoja ya uongo unajibu kwa ufupi, ni uongo mkubwa, Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) inakusanya pesa,TANAPA wanakusanya fedha, halmashauri zote zinakusanya fedha, ukiwa unafahamu mambo itakusaidia, makusanyo ya Serikali yanakusanywa katika mifumo kadhaa na ndio maana kuna maduhuli.Hivyo vitambulisho vya wamachinga vinaingia humo kwenye maduhuli.

"Aliuzwe anajua maduhuli?Anasema kitambulisho hakina jina ,lakini anapaswa kufahamu kitambulisho kina baa kodi, ujue jina kwenye kitambulisho sio kujua taarifa ndani kuna nini. Vitambulisho vilikuja kwa ajili ya kuondoa kero ambayo wajasiriamali walikuwa wanaipata,"amesema Polepole.
Amefafanua yeye amebahatika kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo na Musoma kwa Ubungo katika eneo la soko la mahakama ya ndizi mjasiriamali analipa sh,2000 hadi sh.3000 kwa siku na mwingine kwa mwezi analipa Sh.150,000.

"Yule anayelipa Sh.2000 kwa siku maana yake kwa mwaka mzima atakuwa aanalipa Sh.730,000 na Rais Dk.John Magufuli alipoingia alikuja na ubunifu wa vitambulisho kwa mjasirimali kulipa Sh.20000 kwa mwaka mzima.Kama mgombea wa chama cha Mbowe na mwakilishi mkazi wa mabeberu hajui jambo hili, huyu si mwenzetu.

"Na katika uchaguzi mkuu mwaka huu tunataka kuwathibitisha hao vibaraka wa mabeberu kuwa Tanzania ni nchi huru na inayo nafasi ya kuamua kuhusu mambo yake bila kupangiwa na yoyote.Hao vibaraka wa mabeberu hawatakuwa na chao baada ya Oktoba 28.

"Tanzania wana jambo lao , mtu ana hadaha watu kuwa fedha za vitambulisho zinanunua magari ya CCM. Tuna Bunge linafuatilia hesabu vizuri, ujue anataka kufunguliwa mashtaka kwasababu ya kutuchafua, sasa atambue hakuna anayemfungulia mashtaka, nataka kumwambia kabla ya vitambulisho vya wajasiriamali, CCM wanatembelea V8"amesema Polepole.

Ameongeza kwamba yeye amemuelewa Tundu Lissu wao bado wanatumia Pick up kule mkoani wakati CCM wameshatoka huko."Hatutamfungulia mashtaka yoyote kwa kutuchafya, tunamsubiria Oktoba 28 tukamalizane naye.Mbowe amemchomeka kuwa Makamu Mwenyekiti na kisha akamueweka kugombea urais, na wanajua urais ni wa ndugu Magufuli , hivyo arudi kwa waliomtuma maana nao huko wana jambo naye."

Kuhusu mwenendo wa Uchaguzi Mkuu, Polepole amesema uchaguzi ni jambo la kisheria na vyama vya siasa wameshirikishwa hatua zote za mchakato huo, hivyo wanaunga mkono mambo yote yanayoendelea kwa mujibu wa Katiba.

Pia amewaomba wananchi kule Zanzibar wapuuze maneno ya mfa maji ya mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad ambaye anapotosha kuhusu siku ya kupiga kura.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...