Mwenyekiti wa Kijiji cha Darajani wilayani Liwale mkoani Lindi Hemed Mbanila akifafanua jambo kwa maofisa kutoka MJUMITA na TFCG wakati wa mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Ofisa Misitu Wilaya ya Liwale Nassoro Mzui.

Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Maliasili wakiwa katika mkutano wa kujadiliana kuhusu usimamizi shiririkishi wa misitu pamoja.

Ofisa Misitu wa Wilaya ya Liwale mkoani Lindi Nassoro Mzui (aliyesimama) akizungumza wakati mkutano uliowakutaisha Kamati ya Maliasili katika Kijiji cha Darajani pamoja na wadau wa uhifadhi misitu kutoka Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA) na TFCG uliokuwa ukijadili kuhusu umuhimu wa mradi wa kuhifadhi misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya misitu(CoFoREST).Kushoto ni Ofisa Sera na Urakabishi kutoka MJUMITA Elida Fundi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili Zaitun Likwata akizungumza namna ambavyo wajumbe wa kamati hiyo na wananchi wanavyoshirikiana katika kulinda na kuhifadhi misitu uliopo kwenye kijiji chao ili uwe na tija kwao.

Jengo la Ofisi ya Kijiji cha Darajani linavyoonekana baada ya kujengwa na wananchi wa Kijiji hicho kupitia fedha ambazo wanazipata katika msitu wa Narungombe unaomilikiwa na kijiji hicho.

Ofisa Misitu wa Wilaya ya Liwale mkoani Lindi Nassoro Mzui(wa kwanza kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Maliasili katika Kjiji cha Darajani.

Ofisa Sera na Urakabishi kutoka MJUMITA Elida Fundi(aliyesimama) akitoa maelekezo ya kwa viongozi wa Kijiji cha Darajani wakati wa mkutano huo

Wazee maarufu wa kijiji cha Darajani wakiwa makini kufuatilia maelezo mbalimbali yanayohusu mradi wa mradi wa kuhifadhi misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya misitu(CoFoREST)unaosimamiwa na TFCG na MJUMITA.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV.


WANANCHI wa Kijiji cha Darajani wilayani Liwale mkoani Lindi wamekiri kwamba uwepo wa siasa chafu katika kijiji chao umechangia kwa kiasi kikubwa kukataliwa kwa miradi iliyokuwa na nia njema kwao ikiwemo ile inayohusu utunzaji na uhifadhi wa misitu.

Wamekiri hayo wakati wa mkutano uliokuwakutanisha baadhi ya wananchi, wajumbe wa kamati ya asili na uhifadhi, pamoja na wadau kutoka mashirika yanayojihusisha na utunzaji wa misitu ya asili wakiwemo TFCG na MJUMITA.

Wakizungumza kwenye mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali , wananchi hao wamesema siasa imechangia kuwarudisha nyuma kwani vijiji vingine ambavyo vilikubali kuwa na miradi ya utunzaji misitu na kuitumia kwa maendeleo ya wana kijiji wamepiga hatua kubwa ikiwemo kujenga ofisi , madarasa, nyumba ya mtumishi, kununua trekta na mengine mengi ya maendeleo.

Wamefafanua siasa chafu kutoka kwa baadhi ya wanasiasa ulisababisha uvunaji haramu wa rasilimali misitu katika Msitu wa Narungombe kuendelea na hivyo kijiji kukosa mapato yanatokana na rasimali hiyo lakini kwa sasa tayari wamejifunza na hawatarudia tena makosa kwani shida yao ni maendeleo na sio siasa chafu za kukwamisha miradi ya maendeleo.

Msitu wa Narungombe wenye ukukwa kwa hekta 5,033 ni sehemu ya Msitu wa Angai uliopo wilaya ya Liwale mkoani Lindi na kwamba kukwama kwa mradi wa usimamisi shirikishi wa misitu ya jamii imetokana na baadhi ya wanasiasa kuendesha kampeni za chinichini za kuwaambia wananchi wakate.

Wananchi hao wamewaambia waandishi hao waliambatana na maofisa wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) na Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG) wanaotekeleza Mradi wa Kuhifadhi Misitu kwa Kuwezesha Biashara Endelevu ya Misitu (CoFOREST) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) wanachotaka ni kuona msitu walionao unakuwa na tija kwa wote badala ya mtu mmoja mmoja.

Mmoja ya wazee wa Kijiji cha Darajani Abdulrahman Ngokwe ameeleza wazi walipelekewa mradi unaohusu uhifadhi misitu pamoja na matumizi bora ya ardhi lakini kwasababu ya mambo ya siasa walikata lakini leo wanajuta kwani wenzao waliokubali wamepiga hatua kubwa ya maendeleo.

"Wakati tunaletewa huo mradi Serikali ya kijiji ilikuwa chini ya CUF na hao ndio walikuwa wanapinga miradi hii mizuri.Pia palikuwepo na watu wachache waliokuwa wanavuna misitu kwa njia haramu.

Baada ya kuona tulikosea tulimua kwenda manispaa kuomba msamaha na kuwaambia tunahitaji mradi uwepo na kwetu, wametukubalia na sasa tumeanza na tunaamini tukianza kuvuna misitu wetu tutapata maendeleo kama wengine,"amesema.

Amesema vijiji jirani vya Likombora, Turuki na Mihumo wamefanikiwa sana kupitia mradi huo."Tunashukuru mradi huu umekuja na hapa kwetu lakini tunaomba radhi sana kwa kuukata wakati tunaletewa mwanzoni."Kwa upande wa Ofisa Misitu wa Wilaya ya Liwale, Nassoro Mzui amefafanua wilaya hiyo ina vijiji 27 vyenye misitu ya asili na kati ya hivyo 23 vipo katika Msitu wa Angai na vijiji vinne vipo nje ya msitu huo.

"Katika Wilaya ya Liwale programu ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya jamii(USMJ) inatekelezwa kupitia mpango wa Mnyororo wa Thamani  wa Mazao ya Misitu (FORVAC) na CoFOREST.Pamoja na mafanikio yaliyopatikana kutokana na miradi hii bado kuna changamoto ikiwemo ya ukubwa misitu,hivyo kusababisha ulinzi kuwa hafifu,"amesema.

Kuhusu kijiji cha Darajani amesema kuwa awali walikataa mradi huo, hivyo waliamua kupeleka mradi kwenye maeneo mengine lakini kwa sasa wamekubali a hivyo wameanza mchakato na hasa katika kuangalia masuala ya kuwa na sheria ndogondogo ambazo zitawaongoza wana kijiji katika kutekeleza shughuli zao.

Aidha amesema wilaya hiyo inajivunia kwa kuondoa idadi ya vijiji tegemezi kutoka bajeti ya wilaya huku akitoa rai kwa wilaya nyingine nchini kuhamasisha USMJ kwani ni mfumo rafiki na endelevu kwa misitu ya vijiji na wao ni mashahidi ya jinsi ambavyo wameendelea kunufaika.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kijiji cha Darajani Hemedi Mbanila ameongeza wao wapo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha misitu inakuwa salama na inaleta tija kwa wananchi wote.

Ofisa Ofisa Sera na Uraghibishaji wa MJUMITA ametoa sababu za kutembelea kijiji hicho pamoja na vijiji vingine ambavyo vinatekeleza miradi hiyo na lengo kuu ni kuona na kujifunza kutoka kwa wananchi na wao watatoa ushauri, maoni na mawazo yao ili kuboresha uhifadhi wa misitu.
Ametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa taasisi na masihirika kufanya ziara ya kutembelea vijiji ambao vina misitu ya asili kusambaza elimu ya USMJ ili kuokoa zaidi ya hekta milioni 17 kati ya milioni 22 za misitu ya vijiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...