Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imewatambua wafanyabiashara wake ambao wamekuwa na utamaduni wa kulipa kodi bila kushurutishwa kwa kuwapa vyeti maalum vya kutambua mchango wao kwa manispaa hiyo katika ulipaji wa kodi.

Pia halmashauri hiyo imeahidi kujenga jengo la kituo cha pamoja kitakachokuwa na huduma zote zinazohusiana na uanzishaji biashara huku kukiwa na mkakati wa kuanzisha jengo la pamoja ambalo ltakuwa na huduma zote kwa lengo la kurahisisha utoaji huduma kwa wafanyabiashara wapya ambao wanataka kuanzisha biashara ndani ya manispaa hiyo.

Akizungumza mbele ya wafanyabiashara wa manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, ambao wametambuliwa kama walipaji kodi wazuri, Mkuu wa Wilaya hiyo Ng'wilabuzu Ludigija amesema Serikali inajivunia uwepo wa wafanyabiashara ambao wanatimiza jukumu la kulipa kodi kwa wakati bila  shuruti na bila kutozwa faini ambazo hazipendezi na kwamba wataendelea kushirikiana nao kuhakikisha yote ambayo yanaoekana ni chagamoto yanapatiwa ufumbuzi wake.

"Oktoba 10 mwaka huu tulikutana na wafanyabiashara kupitia Baraza la Biashara ma siku ile tulikuwa na makundi yote ambayo yaliwakilishwa,  tulipokea changamoto , ushauri kama Serikali,na hili leo linalofanyika ni utekelezaji wa yale yaliyoibuliwa na baraza la wafanyabiashara.

"Kwa muelekeo tunaokwenda nao kama nchi, kama taifa kwa walipa kodi na hasa kwa kuona umuhimu wa kulipa kodi kwa wakati ili Serikali iweze kutekeleza miradi ya maendeleo, sisi tunawashukuru sana, kama Serikali tutaendelea kuwapa kila aina ya ushirikiano na kila kwenye changamoto tutatafuta ufumbuzi wake.

"Lengo kubwa tunataka kuona tunaenda kama nchi na fedha ambayo mnaitoa tunahakikisha tunaisimamia kwa nguvu zote na inakwenda kutatua matatizo ya watanzania wote wakiwemo wa Ilala.Aidha tunajaribu kuangalia namna bora zaidi ya kuangalia katika ulipaji kodi, wakati mwingine tunashuhudia foleni na usumbufu katika kwenda kulipa kodi lakini nazishukuru benki zetu zote kwani zimekuwa msada mkubwa katika kuhakikisha walipa kodi wanaweza kutekeleza jukumu hilo kwa haraka zaidi,"amesema.

Pia amesema upande wa Serikali, hasa Manispaa ya Ilala wanao mpango wa kuanzisha kituo cha pamoja cha walipa kodi, hasa kwa wafanyabishara wapya ambao wanaotaka kuanzisha biashara."Mkurugenzi wa Manispaa yetu ya Ilala amenihakikishia na timu ya watalaam kuanzia tarehe 15 tunakwenda kujenga jengo la kituo kimoja cha kutoa huduma.

"Ambapo  taasisi zote muhimu zitakuwa sehemu moja  Anatouglou, pale ambapo tunataka kuanzisha biashara kusiwe na usumbufu , tunataka kurahisisha , huduma zote zipatikane sehemu moja.Pia tunao mpango wa kuanzisha vituo vya kulipa kodi ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wanaotoka Chanika na Msongola kuja mpala Manispaa ya Ilala, tumeanzisha kituo cha kukusanya mapato Buguruni na tunao mpango mwingine wa kuanzisha vituo vingine kwenye maeneo ya Tabata na Kinyerezi.

"Hiyo itasaidia wananchi na wafanyabiashara kutotumia muda mwingi kutafuta vituo vya kulipa mapato, na ndio maana tumepiga hatua kubwa ya ukusanyaji kutoka Sh.bilioni 46 miaka miwili iliyopita mpaka Sh.bilioni .bilioni 58,"amesema.

Amesisitiza umuhimu wa kufanya kazi pamoja badala ya kuviziana , hawataki kuona biashara zinafungwa na kwenye changamoto basi zipatiwe ufumbuzi kwa pamoja, lengo la Serikali ni kuona mfanyabiashara mdogo anakuwa.

Awali Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Jumanne Shauri amesema manispaa hiyo imamua kutoa tuzo hizo kwa walipaji kodi wakubwa, wa kati na wadogo ambao wamekuwa wakitimiza wajibu wao bila usumbufu wowote, hivyo ni vema wakatambuliwa na kuthaminiwa.

"Kupitia wafanyabiashara hawa mwaka jana tulipanga kukusanya kodi Sh.bilioni 57 lakini mpaka tunamaliza mwaka tulikuwa tumekusanya Sh.bilioni 58 sawa na asilimia 103. Sawa watu ambao walitusaidia ukusanyaj huo wa kodi ni pamoja na wafanyabiashara na hasa niseme wengi wao tunao hapa, wana utii bila shuruti ingawa kuna wafanyabiashara wachache ambao hawataki kulipa kodi, lakini tutapambaa nao na kubwa zaidi itakuwa ni kuwapatia elimu. 

"Kupitia elimu ambayo manispaa tunaitoa kuhusu masuala ya ulipaji kodi na umuhimu wake, kumekuwepo na ongezeko la wananchi wengi wamekuwa wafika manispaa wakitaka kupata utaratibu wa kuanzisha biashara,"amesema.

Aidha amesema kwa kuwa wanakwenda robo ya pili ya ukusanyaji kodi, ameendelea kuwahamasisha wafanyabiashara wanaolipa kodi waendelee kulipa na bahati nzuri kuna mifumo ya ulipaji kodi ya kieletroniki, hivyo wale ambao wanakwepa kulipa kodi watabainika.

"Kwa hiyo niseme wafanyabiashara hawa ambao wamepewa vyeti leo tunatambua mchango wao katika manispaa yetu, na vyeti hii ambavyo tunatoa kwao ni chachu ya kuendelea kulipa kodi, haitakuwa ile stori ya mgema akisifiwa tembo hulitia maji,"amesema.


Wakati huo huo Mweka Hazina wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Turusubya Kamala amesema katika kuhakikisha wanaendelea kukusanya kodi, wameweka utaratibu wa kuwa na siku maalum ya kukutana na walipaji kodi wakiwemo wafanyabiashara ambapo hutumia siku hiyo kubadilisha mawazo na kama kuna changamoto wanazitafutia umbuzi kwa pamoja.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya hiyo Ng'wilabuzu Ludigija akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wafanyabiashara mbalimbali wa wa wilaya hiyo ambao wamekuwa wakilipa kodi zao kwa wakati bila kushurutishwa.
Sehemu wanyabiashara wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye majadiliano na maofisa mbalimbali wa kodi wakati wa tukio la kukabidhiwa vyeti kwa wafanyabiashara hao ambao wamekuwa wakilipa kodi kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala(kulia) Ng'wilabuzu Ludigija akiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa tukio la utoaji tuzo kwa wafanyabiashara wa wilaya hiyo ambao wametambuliwa kama walipaji kodi kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Ng'wilabuzu Ludigija(wa pili kulia) akikabidhi cheti kwa Meneja Mwandamizi kutoka Benki ya NMB Adelard Mang'ombo (kushoto)kama sehemu ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha ukusanyaji kodi kutoka kwa wafanyabiashara.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Wilaya ya Ilala Jumanne Shauri(aliyesimama) akizungumza kabla ya tukio la utoaji tuzo kwa wafanyabiashara wamanispaa hiyo ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu la kulipa kodi bila usumbufu wowote.
Sehemu ya wajasiriamali wa manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wakionesha biadhaa zao wakati wa tukio la utoaji tuzo kwa wafanyabiashara ambao wanalipa kodi kwa wakati ndani ya manispaa hiyo.
:Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la utoaji tuzo kwa wafanyabishara ambao wanalipa kodi kwa wakati katika manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Ng'wilabuzu Ludigija(wa pili kulia) akikabidhi cheti kwa Meneja wa Kanda ya Mashariki na Pwani kutoka benki ya CRDB George Yetara(kushoto) ikiwa ni kuthamini na kutambua mchango wa benki hiyo katika ukusanyaji kodi.

 Mmoja ya wafanyabiashara wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam akiwa ameshika tuzo baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Ng'wilabuzu Ludigija(katikati).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...