Mkurugenzi wa uhusiano wa makampuni ya Total Marsha Msuya Kilewo akizungumza kuhusiana na udhamini wa Total katika ununuzi wa taulo za kike kwa wanafunzi na kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika vituo cha Total kujaza mafuta ili kuwezesha kampeni hiyo leo Mkoani Dar es Salaam.




Mwanamitindo na mwanzilishi wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation, Flaviana Matata (Katikati,) akiwa katika picha ya pamoja na wanawake wafanyakazi kutoka Total na taasisi hiyo mara baada ya kuzindua kampeni hiyo ya kuwasaidia watoto wa kike waishio katika mazingira magumu kupata taulo za kike kila mwezi, Leo jijini Dar es Salaam.
 

KAMPUNI ya mafuta ya Total Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation wamesherehea siku ya wanawake duniani ya namna ya pekee, ambapo Total Tanzania imedhamini ununuzi wa taulo kwa wanafunzi wa kike kupitia taasisi hiyo iliyo chini ya mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata.

Akizungumza wakati wakizundua kampeni hiyo iliyokwenda sambamba na ugawaji wa taulo za kike kwa wateja wanawake waliofika kujaza mafuta katika kituo cha Total cha East Oysterbay Mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi wa uhusiano wa makampuni ya Total Marsha Msuya Kilewo amesema, kwa mwezi Machi ambao maadhimisho ya siku ya wanawake hufanyika Total wamejiunga na Taasisi ya Flaviana Matata katika kudhamini ununuzi wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike ili kuwawezesha kupata elimu na kutimiza ndoto zao.

"Total tumekuwa tukirudisha kwa jamii kwa namna mbalimbali na kwa kuona juhudi zinazofanya na msichana mwenzetu Flaviana Matata tukaona ni vyema tukashiriki katika kuwasaidia watoto wa kike kwa kudhamini ununuzi wa taulo za kike....Hivyo kwa kila lita itakayonunuliwa katika vituo vyetu vya mafuta shilingi moja itachangia kununua taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi wa kike.'' Amesema.

Aidha amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika vituo vya mafuta vya Total  ili kuwawezesha watoto wengi zaidi kupata taulo za kike na kuweza kuhudhuria shule bila kukosa.

''Hili ni jukumu letu wote watanzania katika kuwasaidia watoto wakike 1500 nchini ambao hukosa siku 5 hadi 7 kwa mwezi kwa kukosa njia sahihi ya kujilinda wanapokuwa katika siku zao za hedhi, hizi ni takribani siku 60  hadi 84 kwa mwaka ambazo watoto wa kike hukosa masomo kwa kushindwa kununua taulo za kike.'' Amesema.

Kwa upande wake mwazilishi ya taasisi ya Flaviana Matata Foundation, Flaviana Matata amesema taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu katika kuhakikisha watoto wa kike wanakwenda shule na kupata elimu na ubia huo utaleta faraja na tabasamu kwa watoto wengi waliokuwa wanashindwa kuhudhuria masomo yao kwa kukosa taulo za kike kila mwezi.

Amesema hadi sasa wamewafikia watoto wa kike kati ya 1500-1700 ambao hupata taulo za kike kila mwezi na kupitia ubia huo Total na Flaviana matata watawapatia  taulo za kike zaidi ya 9000 wanafunzi wa kike  ambao wametoka katika familia duni. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...