Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, akizungumza na wananchi wa Kata ya Rudi, Jimboni kwake, Wilayani Mpwapwa, leo, ambapo amewataka wananchi wa Kata hiyo kutunza mazingira kwa kutofanya shughuli za kilimo au kukata miti milimani jimboni humo. Pia amewaonya Watendaji wa Vijiji wanaoshirikiana na waharibifu wa mazingira katika maeneo hayo. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, akiingia katika darasa la shule ya msingi Rudi, lililojengwa mwaka 1950 katika Kata ya Rudi, Jimbo la Kibakwe, Wilayani Mpwapwa. Aliiagiza darasa hilo likarabatiwe bila kubadilishwa muonekano wake. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, akizungumza na wananchi wa Kata ya Rudi, Jimbo kwake, Wilayani Mpwapwa, leo, ambapo amewataka wananchi wa Kata hiyo kutunza mazingira kwa kutofanya shughuli za kilimo au kukata miti milimani jimboni humo. Pia amewaonya Watendaji wa Vijiji wanaoshirikiana na waharibifu wa mazingira katika maeneo hayo. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Rudi iliyopo katika Kata ya Rudi, Jimbo la Kibakwe, Wilayani Mpwapwa, leo, wakati alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kukagua madarasa yanayojengwa katika shule hiyo kongwe iliyojengwa mwaka 1950. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...