Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, leo Julai 25, 2021 amezindua kiwanda cha kubangua Korosho kilichopo Wilaya ya Newala mkoani Mtwara kinachomilikiwa na Kampuni ya wazawa ya Prosperity Agro Industries

Kiwanda hicho kinatarajia kubangua hadi tani 5000 za korosho kwa mwaka na kutengeza ajira 800 za ndani na nje ya Newala na kununua korosho zilizobanguliwa na wajasiriamali wadogo na kuziongeza thamani kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.

Makamu wa Rais amewapongeza wamiliki wa kiwanda hicho kwa kuitikia wito wa Serikali kwa kuifanya nchi kuwa ya viwanda na kusema serikali ya awamu ya sita itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji na wafanyabiashara hapa nchini. Amesema uwepo wa viwanda unasaidia kuongeza thamani ya zao la korosho hivyo kupata bei nzuri zaidi.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa watafiti hapa nchini kuanza kazi mara moja ya tafiti juu ya bidhaa zingine zinazoweza kutokana na zao la korosho. Amesema kilimo cha korosho kinategemea na takribani kaya laki 7 hivyo serikali itaendela kutoa kipaumbele katika zao hilo tayari imetoa ruzuku kwa wakulima kwenye pembejeo kama vile Salfa pamoja na dawa za maji za kulinda mikorosho.

Aidha Makamu wa Rais ameaagiza viongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara kuendelea kuwaunganisha wakulima wa korosho katika masoko ya nje ya nchi kupitia balozi za Tanzania ili kuendelea kuleta tija ya uzalishaji wa zao hilo.

Akiwa Wilayani Newala Makamu wa Rais amepokea changamoto ya uwepo wa kiwanda cha korosho kilichoshindwa kufanya kazi kwa miaka 20 na kumuagiza msajili wa hazina kumaliza suala hilo haraka iwezekanavyo .

Awali akitoa taarifa ya kiwanda cha kubangua korosho,Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Haroun Maarifa ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuweka mikakati itakayolazimu taasisi za kifedha kama TIB na TADB kuongeza sehemu ya uwezeshaji wa kifedha wa viwanda vya uongezaji thamani ya mazao kama korosho ili kuchagiza mtazamo wa serikali ya kukuza viwanda na kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa hapa nchini.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea maelezo kutoka kwa Haroun Maarifa ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kubangua Korosho cha kampuni ya Prosperity Agro Industries kilichopo wilayani Newala mkoani Mtwara Julai 25,2021.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kiwanda cha kubangua Korosho kinachomilikiwa na mwekezaji mzawa wa kampuni ya Prosperity Agro Industries kilichopo Wilaya ya Newala mkoani Mtwara. Julai 25,2021.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizindua kiwanda cha kubangua Korosho cha kampuni ya Prosperity Agro Industries kilichopo wilayani Newala mkoani Mtwara. Julai 25,2021.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akisikiliza kero mbalimbali za wananchi wa eneo la Chiungutwa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.walisimama barabarani kutaka kueleza kero hizo.Julai 25,2021.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasili katika eneo la kiwanda cha kubangua Korosho kinachomilikiwa na mwekezaji mzawa wa kampuni ya Prosperity Agro Industries kwa lengo la kuzindua kiwanda hicho. Newala ,Mtwara Julai 25,2021
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...