- Awataka LATRA kusimamia Level seat.

- Aelekeza Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya kusimamia Utekelezaji wa Mwongozo wa Wizara ya Afya.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona ambapo amepiga marufuku Wananchi kuingia kwenye vyombo vya usafiri na sehemu za kutoa huduma pasipo kuvaa barakoa.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia Mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya ambapo amesema watafanya ziara za kustukiza kwenye Vituo vya Daladala, Feri, Stendi, Mabasi ya Mwendokasi, maeneo ya Masoko na sehemu zote za kutoa huduma ili kuangalia Utekelezaji wa agizo hilo.

Aidha RC Makalla amesema Serikali imejipanga kutoa huduma Bora za matibabu kwa wagonjwa wote watakaofika hospital na kuwataka Wananchi watakaoona dalili za Corona kuwahi vituo vya Afya.

"TUNAKULINDA NA WEWE UTULINDE, VAA BARAKOA KWA MUSTAKABALI WA AFYA YAKO NA WENGINE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...