NA HERI SHAABAN( ILALA)

DIWANI wa Kata ya Kivule Nyasika Getama amewataka wakazi wa Kivule kushiriki SENSA ya Makazi kwa ajili ya kuhesabiwa ili waweze kuletewa Maendeleo ndani ya Kata Kivule.

Diwani  Nyasika alisema hayo wakati wa kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Desemba 2020 mpaka Agosti 2021.

Diwani Nyasika alisema Serikali inatarajia kufanya sensa ya Makazi mwakani 2022 kwa Wananchi wake hivyo wananchi wa Kata Kivule wote watumie fursa hiyo wahesabiwe watambulike waweze kuletewa Maendeleo.

" Maendeleo ni muhimu kwa nchi yoyote nawaomba Wajumbe wa mashina Wenyeviti wa Serikali za mitaa wote mtoe elimu katika kuwaeleza umuhimu wa SENSA wananchi wetu Kivule ilizaa Kata ya Kipunguni awali na sasa Idadi ya wananchi wameongezeka hapa Kivule hivyo lazima tuwatambue" alisema Nyasika

Alisema SENSA wakati ukifika kila MTU lazima awepo itamtamburisha yupo wapi kutokana na Giografia ya Kata yetu kwa sasa kutokana na Changamoto za Mipaka eneo la Magole na Vikao vya Ushauri ngazi ya Wilaya ILALA RCC vitatoa maamuzi yake .

Akizungumzia Maendeleo ya Kata Kivule alisema sekta ya Elimu kuna shule za msingi mbili za sekondari nne amejenga madarasa mawili kwa upande wa shule za msingi sekondari amejenga madarasa kumi na kununua madawati 58 .

Mikakati yake katika utekelezaji wa Ilani ya CCM 2122 kuongeza kidato cha kwanza mpaka kidato cha sitq katika shule za Ally Jumaa na Misitu ili watoto wasome karibu na Kata yao kuwaondolea usumbufu awali ili kuwa mwisho kidato cha NNE.

Mikakati yake mingine kwa mwaka 2122 Kuboresha Barabara na kuanzisha safari za ruti ya Daladala mpaka mjini kwa ajili ya kuwaondolea kero Wananchi.

Akielezea changamoto kubwa iliyopo Magole ukosefu wa shule inapelekea wananchi wake kupata shida ya Wanafunzi kwenda umbali mrefu kutokana na Giografia ya Mipaka na mgogoro wa Kivule na Msongola.

Aliwagiza Wajumbe wa Mashina kuwaorodhesha wananchi wake waliopo katika kaya masikini ili waweze kupitiwa na mradi wa Serikali wa TASAF wasiweke watu wenye sifa katika mradi huo wakaacha watu wenye Vigezo.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Kata hiyo Isac Kibiti aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kumaliza changamoto zao na kuisaidia Serikali katika kuleta Maendeleo ikiwemo kusimamia miradi ya Maendeleo na Utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Diwani wa Kata ya Kivule Nyasika Getama (katikati)akikabidhi Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani 2021 leo September 17/2021 kwa Mwenyekiti wa CCM kata Kivule Hemed Nyangum
Diwani wa Kata ya Kivule Nyasika Getama akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salam Jana wakati wa kuwasilisha Taarifa za utekelezaji wa Ilani
Diwani wa Kata ya Kivule Nyasika Getama akiongoza Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata leo katika Chakula cha Mchana Mara baada kusoma Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani 2021 leo September 17/2021.

(PICHA NA Heri Shaaban)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...