Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Mhe. Zahara Michuzi amemtambulisha Mwanahabari mbobezi na mwandamizi katika maswala ya soka, Hemedy Kivuyo kuwa Msemaji Mkuu wa timu hiyo wakati Kikosi chao kikijiandaa na Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la ASFC msimu wa 2021-2022.

Kivuyo ametambulishwa leo katika Tamasha la Geita Gol Day 2021 sambamba na kutambulishwa Wachezaji wapya watakaotumikia timu hiyo kwenye msimu huu wa mashindano.

Akizungumza kwenye tamasha hilo, Mhe. Zahara amesema ni rasmi Kivuyo atakuwa Msemaji wa Mabingwa na matajiri wa dhahabu (GGFC) wakati tukijiandaa kucheza Ligi Kuu na Mashindano mengine hapa nchini.

“Karibu sana kwenye familia ya Mabingwa Mr. Hemedy Kivuyo, Wanageita wana imani kubwa na wewe na wasubiri makubwa toka kwako”, ameeleza.

Kikosi cha Geita Gold FC kinachonolewa na Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije kimepanda Ligi Kuu msimu huu wa mashindano wa 2021-2022 kwa mara ya kwanza wakitokea Ligi daraja la kwanza ambayo kwa sasa itatambulika kama Championship.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...