Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko (wa pili kushoto) akimsikiliza Mtumishi wa Mamlaka, Yohana Goshashy (kulia) akieleza majukumu ya Mamlaka na lengo la ushiriki wa maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini mkoani Geita baada ya kutembelea banda la Mamlaka kwenye maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji, EPZ Bombambili mkoani Geita. Kushoto ni Mbunge wa Geita Vijijini, Mhe. Kasheku Musukuma ambaye aliambatana na Waziri katika kutembelea maonesho hayo leo.

Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Geita, John Paul Wanga (aliyevaa kofia) wakimsikiliza Mtumishi wa Mamlaka, John Wanjala (kushoto) baada ya kutembelea banda la Mamlaka kwa ajili ya kufahamu majukumu ya Mamlaka na namna wanavyoweza kuwasaidia wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Mkoa wa Geita hasa kwenye matumizi salama ya kemikali.


Mtumishi wa Mamlaka, Eunice Mbata (kulia, picha ya kwanza) na Hadija Makurunge (kulia, picha ya chini) wakiongea na wananchi wa Geita waliotembelea banda la Mamlaka kwenye Maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaii kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji, Bombambili mkoani Geita.


Watumishi wa Mamlaka, Leah Kalinga (kushoto, picha ya kwanza) na Lowasa Kerika (kulia, picha ya pili) wakiongea na wadau waliotembelea banda la Mamlaka katika maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayofanyika katika Kituo cha Uwekezaji (EPZ) kilichopo eneo la Bombambili mkoani Geita.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...