Na Jane Edward, Arusha

Wakandarasi wanaofanya usafi na uzoaji wa taka katika Jiji la Arusha wamemwomba Mkuu wa Wilaya ya Arusha kuingilia kati mgogoro kati yao na mkurugenzi wa jiji la Arusha kwa kile walichodai kutokuepo maelewano kati yao

Wakandarasi hao zaidi ya 30 ambao walikusanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wakizungumza na waandishi wa Habari wanasema wanasikitishwa na hatua ya Mkurugenzi huyo wa Jiji kuwataka kuingiza asilimia mia moja ya makusanyo tofauti na Asilimia 30 iliyoko katika mkataba....

Akizungumza kwa niaba ya wakandarasi hao Alipha Mrutu anasema wanasikitishwa na hatua ya mkurugenzi kuwataka kuingiza asilimia mia moja ya makusanyo tofauti na Asilimia 30 iliyoelezwa katika mkataba

Mrutu amefafanua kuwa awali walikuwa wakitozwa asilimia 15 na baadae 30 ila kwa sasa Mkurugenzi anawataka kuingiza makusanyo yote asilimia mia moja jambo linalopelekea wao kushindwa kutekeleza Majukumu yao ya kila siku

"Ukiangalia sisi tuna matumizi ya pesa ya kila siku huezi kuwaambia vijana wazoa taka kuwa hakuna hela,magari yanahitaji mafuta kila siku ila tunasikitika Mkurugenzi yeye hajali hayo" Alieleza Mrutu.

Alieleza kuwa endapo Mkurugenzi wa Jiji hatakuwa tayari kukaa na sisi na kuzungumzia kuhusu hatma ya makusanyo hayo watagomea kuendelea kuifanya kazi hiyo.

Hata hivyo mkurugenzi wa Jiji la Arusha Daktari John Pima alipotakiwa kuzungumzi suala hilo alikiri uwepo wa changamoto hiyo na kutoa masharti ya kutorekodiwa na kwamba tayari alikwisha mwelekeza mweka hazina wake kulitatua

Pima alifafanua kuwa si kweli kuwa wakandarasi hao makusanyo yao yanachukuliwa kwa asilimia mia moja kama wanavyodai ila ni kwa baadhi yao ambao wana madeni

"Hao wanaotishia kugoma ni kuwa tunawadai ila sio kweli kwamba hela za wakandarasi tunazichukua zote asilimia mia moja,mkataba unasema sisi tunachukua asilimia 30 ya makusanyo na ndivyo tunavyofanya"Alifafanua John Pima.

Mkataba kati ya mzoa taka ngumu ndani ya Jiji la Arusha hufanyika kwa kipindi cha miezi Tisa ambapo katika mkataba huo mkandarasi anapata asilimia 70 ya makusanyo Huku asilimia 30 ikichukuliwa na halmashauri hiyo.

Moja ya gari la taka linalosafisha Jiji la Arusha
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Daktari John Pima
Alipha Mrutu mmoja kati ya viongozi wa wakandarasi wa usafi Jiji la Arusha Akizungumza na waandishi wa Habari.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...