Njombe

Diwani wa kata ya Yakobi halmashauri ya mji wa Njombe Michael Uhahula amewaonya wanaume kula viazi pamoja na pombe kisha kwenda kutafuta mtoto kwa kuwa hali hiyo inaendelea kuchangia upatikanaji wa Watoto wenye udumavu katika jamii na kuendelea kuisababishia hasara serikali kwenye udhibiti wa udumavu.

Amebainisha hayo katika zoezi la kutoa elimu ya lishe katika kijiji cha Limage kata ya Yakobi amapo Imeelezwa kuwa moja ya changamoto inayopelekea kushindwa kudhibitiwa kwa tatizo la udumavu Mkoani Njombe ni Lishe duni isiyo zingatia makundi makuu matano ya chakula pindi wazazi wanapo kuwa katika maandalizi ya kutafuta watoto Jambo linalo Pelekea mama kushika mimba ambayo tayari inachangamoto ya Udumavu .

“Huu uzembe huwa unajitokeza tangu mwanzo kwasababu ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema lazima kuwe kuna maandalizi kwa baba na mama katika lishe,sasa unakuta baba amekula kiazi kimoja asubuhi,kingine mchana halafu jioni anakutana na kingine cha kuchoma baada ya hapo anaenda kunywa pombe halafu akirudi anategemea aende kutafuta mtoto hii maana yake moja kwa atakuwa na udumavu”amesema Uhaula

Wananchi wa Kijiji Cha limage kata ya Yakobi wanakiri kuwepo kwa changamoto ya wazazi kushindwa kuzingatia aina sahihi ya chakula pindi wanapo kuwa katika mipango ya kuongeza familia hivyo kuchangia na kudidimiza ndoto za serikali za mapambano ya kukabiliana na Udumavu pamoja na kuzingatia usafi wa chakula kwa watoto.

Kwa Upande Wake Mratibu wa Huduma za Lishe Halmashauri ya Mji Njombe Maliselina Mtitu anasema Jamii ya Mkoa wa Njombe Imejikita Zaidi Katika Utafutaji na Uzalishaji na Kusahau Majukumu ya Malezi ya Watoto.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...