Jeshi la Zimamoto na Uokoaji leo tarehe 30 Machi, 2023 limepokea Magari (Mitambo) mapya matatu (03) ya Kuzima Moto kutoka kwa Shirika la Nyumbu lililopo Kibaha Mkoani Pwani. Shirika hilo lililopo chini ya Jeshi la Wananchi limekamilisha matengenezo ya magari hayo na yapo tayari kuanza kazi.

Magari hayo mapya yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2.7 yenye uwezo wa kubeba maji lita 5,000/= na Foam lita 500 kwa kila gari, yamekabidhiwa leo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini kutoka kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa.

Hafla hiyo ya Makabidhiano imehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kaspar Mmuya, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga, Meneja Mkuu wa Shirika hilo Brigedia Jenerali Hashim Komba, Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Maafisa na Askari kutoka Jeshi la Wananchi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Waandishi wa Habari.

Mara baada ya Makabidhiano, Kamishna Jenerali Masunga ametoa shukrani nyingi kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kuahidi kuyatunza Magari hayo na kuendelea kuwahudumia wananchi katika huduma za Kuzima Moto na Uokoaji.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...