niko hapa kwa watani wa jadi kwa muda. jamaa wana bonge la bustani wanaiita uhuru pak. watu kibao, sio kama mnazi mmoja imefungwa saa zote, bwawa la samaki limekauka, mpiga ngoma hana mikono na korongo hawana midomo na bembea watu wamekunywa...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Mambo ya kuwa eksipati baada ya jambo kutokea ni dalili ya ufinyu wa mawazo. Mbona wazo hili hukulitoa wakati hujafika Nbi, yaani ukiwa Dar?

    ReplyDelete
  2. Michuzi, pengine upo Nbi kwa ufunguzi wa mfuko wa Mo Ibrahim. Kwa wale wasiojua nasema nini, kuna habari ambazo ziliandikwa kwa mara ya kwanza na shirika la mtandao la Yahoo kuhusu Msudani mmoja bilionea (aliyeanzisha kampuni ya Celtel), Dr. Mo Ibrahim, aishiye huku New Jersey, Marekani, mfuko (foundation) - utakaojulikana kwa jina la Mo Ibrahim Prize for Achievement - wa zawadi kwa viongozi wa Kiafrika ambao ni mifano mizuri ya uongozi bora ikiwa ni pamoja na kusaidia vita dhidi ya rushwa. Mfuko huu amezinduliwa mjini Nairobi. Zawadi hii ni dola milioni 5 kwa kipindi cha miaka10 na baada ya kipindi hiki dola 2000,000 maisha kuanzia Oktoba mwakani.
    Ni pesa zake; anaweza kuzitumia atakavyo. Je, kuna haja ya kuwazawadi viongozi wa namna hii? Kwa nini zawadi ya namna hii isitolewe kwa minajili ya kununua vyandalua kwa wananchi walala hoi wa nchi za viongozi washindi ili kupambana na ugonjwa wa malaria!
    Kati ya wana-Bodi wa mfuko huu ni pamoja na Katibu Mkuu wa zamani wa OAU, Balozi Salim Ahmed Salim, ambaye pia ni mwana-Bodi wa Celtel, Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Michuzi mbona husemi kitu kuhusu mechi ya yanga na simba?

    ReplyDelete
  4. Michuzi, Vipi watani wa Jadi..? Yanga na Simba?Sisi tulio Ugaibuni tegemeo letu la nezi ni hii blog yako?
    Kama itakuwa ni kama Manchester na Liverpool basi sema?

    ReplyDelete
  5. hivi Michuzi wewe ni mwenyeji wa wapi, yaani kabila gani? Inaonekana ni mtu mcheshi sana na mchekeshaji kiasi ya kwamba wale waliokalibu yako muda wote wanacheka!

    ReplyDelete
  6. wee anoy 7:12:59 naona umeanza mambo ya ushoga unamtamani huyu kaka. Ameoa na hapendi uchafu wa ku cheat na wanaume. naona unataka akutandike na mshedede lakini nakwambia pamoja na kuwa mwislamu lakini hapendi kikalio acha tabia wewe anoy ya kutongoza wanaume kwenye blog!!

    ReplyDelete
  7. hiyo ndio nairobi,watu wanamewiva wanapumzika uhuru park,pembeni kidogo ya hapo kwenye barabara inayoelekea capital hill kuna chokoraa kibao wananusa gundi,wana njaa na hawana makazi.

    ReplyDelete
  8. anony wa 1:17:08, uislamu unahusiana nini na hayo amoni yako? last time i checked father Massawe hakuwa muislamu!!

    ReplyDelete
  9. Born again Pagan, Mo Ibrahim, sudanese with British nationality, worked for BT before engalfing into his venture. quotes from the Indepent 27th oct 06 naf said.







    I'M THE VICTIM OF MY OWN MAKING

    ReplyDelete
  10. Pakamcheshi, thanks for info. I have checked it and other useful inf, too.

    ReplyDelete
  11. Zemarcopolo, LOL! Umelenga, jamaa maneno mengiii, wanajitahidi lakini mitaani Nairobi wanakutupia mavi ukisimama kwenye traffic lights hahahahahah! What a JOKE!! Thatz Sucks!

    ReplyDelete
  12. Michuzi huendi na JK kwenye hii ziara yake ya China, Japan, South Korea na Uarabuni?? Picha za huko atatuletea nani?? Au nikuletee mimi tokea huku.

    ReplyDelete
  13. Michuzi siku hizi una kitambi!

    ReplyDelete
  14. Mweeh,mbona Rais Kikwete inafanya siara mara kwa mara?Hii Rais tumiichagua sisi lakini muda mingi iko nje ya nchi na tena inakaa huko siku mingi.Rais kama ilivyo baba wa nyumba inabidi ikae nyumbani itulie na ihakikishe kasi sote sinafanyika mzuri.Michusi wewe haijaenda huko masariki ya mbali?

    ReplyDelete
  15. Michuzi hao wenyeji wako wasikudanganye hapo nrb kuna sehemu hata kichaka chui na uwanja wa fisi kabla ya fagio la kandoro kupita ni ahueni wachokoze tu wakupeleke ujionee vituko!Vilevile hata Tz hususan dar kuna maeneo mandhari yake bomba kabisa yaani kanyaga twende na wewe kama mtanuaji unafahamu au unawachokoza kiaina yake hawa watani wetu wa jadi kwi,kwi,kwi unjua tena simba na yanga!

    ReplyDelete
  16. Born Again,kuhusu maoni 12:53

    Huyu bwana hapigi vita maleria anapiga vita umasikini kwa kuwazawadia viongozi ili wajitahidi kwenye ongozi zao kuinua africa kutoka umasikini,umasikini unacover vyote kuanzia maleria hadi takataka zote ambazo zinakumba Africa,anaamini uongozi bora ndio utaweza kusafisha hayo yote ndio mana ameamua hivyo,anasema NOthing,simply nothing is more important to African development than good governance, ambacho hujaelewa ni nini?
    Viongozi wa africa hiyo ni challenge kwao wajitahidi waache kutegemea misaada na kutia mfukoni kilicho chema kinapokuja..nadhani waelewa..

    ReplyDelete
  17. Michuzi unaanza kuonekana kama Shuga Dedi.

    ReplyDelete
  18. Hatutaki kuhonga viongozi! Zawadi kwa viongozi wazuri ni kuwazawadi kwa kura nyingi. Sitaki peer review ya NEPAD, pia. Sawa na ma-Profesa kupandishana vyeo.

    ReplyDelete
  19. WATANZANIA TUWACHENI WIVU BWANA!! TUMEWASEMA VIBAYA SANA WAKENYA KWA MIAKA MINGI NA NI OBVIOUS KUWA TUNAWAONA WIVU KIBAO KWA MIJI YAO MISAFI, UMAHIRI WAO WA BIASHARA, UWEZO WA KIKATA LUGHA KIBAO ZA KIMATAIFA KAMA KIJERUMANI, KIFARANSA, KIJAPANI, SPANISH NA NYENGINEZO AMBAZO ZIMEWAWEZESHA KUINUA UCHUMI WAO KUWA BORA ZAIDI YA HII BONGO YETU INAYEONDELEA KURUDI NYUMA KILA SIKU.

    HAO CHOKPRAA TUSEMAO KWANI HAPA BONGO HAKUNA? WACHENI STORI NDUGU! HUKU MITAANI DAR NA IRINGA WEVI WA VIKAPU NA MIFUKO NI TELE KAMA NINI, MBONA HATUSAFISHI UFISADI WETU KABLA KUWAONA WIVU JIRANI ZETU.

    KWANINI MICHUZI AKIWEKA PICHA ZA MAREKANI NA MATAIFA YA ULAYA HATUSEMI POROJO? AMA NI VILE KENYA WAAFRIKA WENZETU WAMESONGA MBELE SASA NI CHUKI!?!?

    POLENI KWA HERUFI KUU, COMPUTER ZETU ZA KUOMBA HIZI ZINA SHIDA NA KKEYBODI!!

    JOHAN KIPEKO -DAR

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...