mwandishi mwandamizi alfred ngotezi ametoa hii leo. mie inglishi iz noti richebo. azawaizi ningetafsiri. ila nnachoweza kusema ni kwamba vita ya kalamu imeumuka katik ya waandishi wa bongo na watani wa jadi. endelea kwa muda wako...na wakaribishwa kuchangia mustakabali wa mjadala kuhusu jumuiya ya afrika mashariki,

Thinking Aloud:
Obbo's anti-Tanzania article misguided

ALFRED NGOTEZISunday News; Sunday,October 29, 2006 @00:05

HARDLY one month after the Tanzanian media was assailed by Kenyan journalists and Nairobi-based Tanzanian cartoonist as boot-leaking President Jakaya Kikwete; the attack has been joined by a Ugandan journalist based in Nairobi, Charles Onyango-Obbo.

He spits fire at the Tanzanian media in the 'EastAfrican' Newspaper of last week (October 23-29) titled "let's face it, the Tanzanian media is not being very neighbourly".

One wonders what forms the basis of his serious allegations. Unless his sources are implicit, which is most unlikely, the ones that are explicit in the commentary do not justify his stinging criticisms.

He cites weird contents from a private website, www.habaritanzania.com and concludes..."popular Tanzanian attitudes toward the (East African) Community seem to be growing decidedly hostile." Charles, who should know better, can easily access official websites in Tanzania with regard to the country's official position on the community.

He should also go the full hog by disclosing how many Tanzanians actually visit the said private website.

Without such critical information, he would be mudslinging us for no apparent reason. Charles claims that a section of the Tanzanian media takes exception to "the most mildly critical articles or cartoons, appearing in the Kenyan press," and, surprisingly, the Ugandan press.

Surprising because he fails to cite an example where the Ugandan media have traded harsh words with their Tanzanian counterparts, a factor he concedes in the next sentence: "These articles invite sharp responses and calls to expel Kenyans".

Yet again he fails the test by not disclosing why Ugandans are not targeted for expulsion from Tanzania, if at all. Communication experts concur that such implied insinuations carry strong messages. As such, he has a hidden agenda here.

He is attempting to suck in the Ugandan media, to spark off a bigger, two-against-one, regional problem. This is dangerous and must be condemned in the strongest terms possible.

Further, Onyango blows his own trumpet by claiming to be 'part-time-patriot,' to the two governments of Kenyan and Uganda and being tolerant to African criticisms.

Yet Obbo does the opposite by not opposing the two countries' membership to two economic groups, COMESA and EAC, because it is technically unworkable for a country to belong to two customs unions. He chooses to turn a blind eye on it.

On the contrary, we have made it plain before to the Tanzanian government that sooner or later they have to choose between SADC and the EAC.

Again, it is not difficult to see why Charles claims to be half patriot, since wisdom dictates that you don't bite the hand that feeds you; Kenya is his new home while Uganda remains his ancestral origin.

At a time when East Africans have just started a de-facto referendum on the future of the EAC, it is difficult, and rather unfair, to see a man of Onyango's standing blaming Tanzania for a decision that is yet to be made.

It must be recapped that the collapse of the former EAC was fuelled by such hate media campaigns of the 70s between Tanzania and Kenya. It was the 'man-eat-man' bombshells from Tanzania, against the 'man-eat-nothing' rockets from Kenya.

The hate campaign, doubtlessly, put the last nail in the coffin of the former EAC.

Now, even before the new East African federation baby has been born, a career journalist of Onyango's stature is already inducing forced abortion on it. Yes, Tanzanians may need more time to think the federation over, but certainly it is a matter of time, not of outright rejection.

It is their right to give it serious thought with a view to negotiating a better deal.

If industrialized Britain and other Western monarchies are yet to endorse the European Union's single currency, for whatever reason, why shouldn't poor Tanzania think twice before endorsing an all-engulfing political federation? British Prime Minister Tony Blair's well-known euro-centrism notwithstanding, his remaining days at 10 Downing Street may not be enough to approve the euro.

Likewise, forming or not forming a federation is a decision that must be taken by 80 million East Africans, not by the region's three state house tenants.

Charles may wish to be reminded further that only last week Australia rebuffed the signing of the Kyoto Protocol against global warming, claiming it could hurt its coal-dependent economy. It is all about sovereignty and each country's economic well-being.

Trade statistics between Kenya and Tanzania depict a gloomy economic situation for the latter.

Only focused and down to earth negotiations can open the way forward. Tanzania's balance of trade with Kenya for the last five years is a tale of chronic deficits, which grew from 48.9bn/- in 2000 to an alarming 89.1bn/- last year.

The ideal situation, as Obbo knows, is to have no more imbalances. For now, however, it is loud and clear that Tanzania is a perpetual market for Kenyan manufactured goods and services and for sure, Kenyan industrialists would love it to continue forever.

In the eyes of Onyango, the biggest folly of Tanzania's scribes is to disclose the negative economic performance and interpret it as unfavourable to the country. But the journos only want to turn around the imbalances by either increasing exports to Kenya, reducing imports from there, or some other feasible economic terms that would be responsive to Tanzania's future growth.

On the other hand, hardly 20 per cent of Tanzania's arable land is tilled today, while almost half of all Kenya is arid, meaning a hasty political framework could give away Tanzania's land. Certainly, a safety-mechanism of sorts is required here. On the other hand, the tribal politics across a section of Kenya's body politic are a potential threat to a cohesive people Tanzanians have become over the years.

Needless to say, Kenya has six public universities as compared to Tanzania's only three, suggesting that in the event of a fully-fledged Common Market, Kenyans would land most white-collar jobs in the region.

It is a whole range of sticking points in view of which, it is only fair that Tanzanians negotiate a better deal that would respond to most, if not all of these fears. Frankly, some of us opposed from the word go the abstract idea of fast-tracking an economic entity that is the EAC, on a political roadmap.

We know that officials proceeded to spend over US dollars 60,000 on Amos Wako's team. The-quickly-arranged mission was aimed at seeking public views on the federation. It is public information that it was a flop, necessitating a fresh but expensive round of views that is afoot today.

We only need to look back at past Libyan-engineered political unions across Africa, to realise how hurriedly arranged political unions are nothing but a waste of time and resources. Where is the Egyptian-Libyan union today? It evaporated into thin air. It was easy come easy go. If the new EAC is indeed people-oriented, private-sector driven and modelled on the EU, it should be left to grow slowly. It can only develop on a gradual basis, metamorphosing from one stage to another.

The customs union has been the starting point in our case. But instead of it being left to oversee increased regional trade, it has a fixed political timetable lasting five years, at most, before we jump into a common market for an equally short period of time, then the single currency and, by all means, a political federation by 2013!

My friends in Arusha argue that intra-East African trade has been growing fast since the establishment of the regional customs union a few years ago. I say fine, show me how many court cases have been sent to the East African Court of Justice for arbitration, for that would be automatic in increased cross-border transactions. "Oh, no cases so far," they respond.

What about the trade's volume, is it growing? Well, nothing concrete at the moment, still compiling data...they tell me. There we are.

This is a nascent project that should not be rushed into. By all means, Charles should not penalize the Tanzanian scribes for these realities. The economic imbalances between Kenya and Tanzania are as historical as the other sticking points. They are older than most of us. On matters involving sovereignty and the well-being of the people, all countries are entitled to time and choice.

Tanzanians like Kenyans and Ugandans need a responsive framework in the new EAC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kwa kweli nimefuatilia huu mjadala Bw Michuzi kwa karibu sana. Na kwa kuweka columns za Bw Ngotezi na Bw. Obbo kwa pamoja, Obbo haoni ndani kwa sababu zifuatazo
    1. makala ya Bw. Ngotezi imetulia na imefanya uchambuzi yakinifu ktk kutazama hili suala EAC na pia kutoa mifano hai na hoja za nguvu za kuweza kutoa msimamo safi na nia njema ya Tanzania kujiunga na EAC. Ukiiliganisha na makala aliyoandika Bw Obbo, utaona kuwa ni uandishi ambao umejaa "emotions" na ni judgemental kwa mambo ambayo sisi kama watanzania wazalendo yanakera na yametoa sura halisi ya Waganda kwa kuwa na propaganda ya kujifanya wao ni ndugu zaidi na Kenya kuliko TZ, mgawanyiko ambao unafanya "undugu kati ya nchi za Afrika mashariki kuwa matatani" (hebu tuiite hii ni kama familia ya watoto wa baba mmoja).
    2. Nimefurahishwa na hatua ya Kikwete ya kuunda tume ya kuweza kukusanya maoni toka kwa wananchi ilikujua tunalifikiriaje hili suala la Muungano. Nchi za EU nazo zilifanya hivyo, kwa nini kitendo cha Watanzania kufanya hivyo kiwafanye WaKenya kuhofia? Na kwa nini Waganda wahofie ila hofu yao waielekeze kwa kutumia mgongo wa Kenya??
    3. Watanzania mara nyingi tunadharauliwa na wenzetu na tumekuwa tukiitwa kuwa "wasiojua lolote" kwa ukimya wetu na kwa kuweza kuwa na amani kwa kipindi kirefu..nachoweza kuona hapa ni kwamba tunaitwa hivyo na nchi ambazo hazijatulia "kisiasa" "nchi zenye kimuhemuhe wa madaraka" "Nchi zenye vita vya chinichini vya wenyewe kwa wenyewe" ambazo wanajaribu kutu-classify kwa kutokuelewa kuwa yote haya tuliyonayo ni matunda ya kazi ya muda mrefu wa 'undugu'. Falsafa ambayo japo inaonekana kufa ila huwa tukiwa na jambo lolote linalohusu utaifa, Tanzania tuna uwezo wa kuonyesha kuwa sisi ni taifa moja na yenye nguvu. Hilo ndilo linalowatia hofu hawa ndugu zetu, wanashindwa kuelewa sisi tuna falsafa ya aina gani kama nchi ndiyo maana wanatafuta mbinu za uchokozi, maana uchokozi ni kawaida yao.
    4. Ningependa kuwakumbusha kuwa, Mwai Kibaki alipoingia madarakani, alialikwa na rais Bush, hii ilikuwa habari ya kuvunjika (BREAKING NEWS) na magazeti ya Kenya yalihakikisha kuwa kila mtu duniani anaona hilo na amelisikia hilo, Tanzania hatukusema lolote, kulikuwa na maneno ya chini chini kuwa licha ya Mkapa kuwa kiongozi shupavu ktk nchi za kusini mwa jangwa la sahara Afrika, mbona hajawahi pewa mwaliko kama huo. Anyway no one commented NEGATIVELY FROM TANZANIA. Kama walituzungumzia kule White house hatujui na wala hatukufuatilia hata kidogo. Nadhani walipoona Kikwete kukaa na Bush, walitafuta kila neno baya kumzungumzia rais wetu, waliona sasa they are threatened, kwa nini Tanzania iwe hivi? After all talking to Bush is not a big deal!!! Kwa sababu wana hulka ya vimbelembele, kiliwauma. Tanzania hatuna vifrontifronti, ndiyo maana tunaonekana hatujui.

    Hebu tuwaangalie hawa watu kwa umakini mkubwa sana. Bwana ngotezi katukumbusha mambo ya muhimu sana.

    ReplyDelete
  2. Kwa maoni yangu huu muungano wa jumuiya ya Afrika mashariki hata sioni umuhimu wake, kama tunataka kujiunga tuuweke sawa kwanza muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wakati tanzania tuna tatizo la ajira bado tunataka kuruhusu na wakenya na waganda nao kuja kutafuta kazi nchini mwetu, hawa jamaa siwapendi kwa sababu ni wakabila sana halafu watatuletea na majambazi nchini mwetu. TUKAE NAO MBALI SANA

    ReplyDelete
  3. Sioni sababu ya kuwa na EAC.Tanzania ni nchi kubwa na ina rasilimali nyingi.mpaka sasa hatutumii hata asilimia 10 ya rasilimali zetu.sasa huko Kenya na Uganda tunafuata rasilimali gani ambazo hatuna.Kwanza tujiweke sawa kwa kuhakikisha tuna good control over our resources then tunaweza kuzungumzia kushirikiana.Pia ninasikitishwa na hatua ya wanasiasa wetu kuanzisha bunge na baraza la mawaziri wa afrika mashariki pamoja na mahakama bila kutuhusisha.katiba ya nchi ianeleza wazi kuwa ni wananchi pekee wanaoweza kuruhusu mabadiliko makubwa kama hayo.Hivi sasa hata kama kuna maoni yatachukuliwa itakuwa ni porojo tu kwa sababu kimsingi EAC tayari imeshaundwa.kitu kingine kinachonisikitisha ni viongozi(wanasiasa)wetu kuendelea kuheshimu mgawanyo wa bara la afrika ulioachwa na wakoloni.kwani ni lazima tushirikiane na kenya na uganda.kuna zambia,msumbiji,mauritius,madagascar,malawi(ingawa tuna beaf nao).kuna haja gani ya kukumbatia mipaka ya kaskazini tu,iwapo tunaona kuwa ni lazima kuingia kwenye wimbi la kugawana matatizo(maana EAC ni umoja wa kugawana matatizo).nani anaweza kuufikiria ugumu wa mgogo,mzaramo,mnyakyusa,mngoni kupata kazi nairobi mahali ambapo hata mkamba apewi kazi na mkikuyu!

    ReplyDelete
  4. three state house tenants.....thats exactly where the problem lies!

    ReplyDelete
  5. Haaa Sisi tunaleta utani na maisha. Tanzania yenyewe bado haijaungana ndani ya nchi halafu hapo hapo tunataka kuungana na Kenya na Uganda!!! Muda mwingine nawaza hivi kweli ni viongozi wetu au ndio suala la elimu na kuelewa ndilo linalotusmbua?

    Hakuna atakaye kataa humu ndani kwamba ndani ya Tanzania muungano hakuna. Wabunge na wananchi waliowateua kuwa wabunge hawana muungano, Raisi na mawaziri wake hawana muungano, Pemba, Unguja hawana muungano, Zanzibar na Bala hawana muungano, Tanga na Arusha hawana muungano yaani kifupi ndani ya nchi yetu hakuna muungano. Mjini kuna umeme vijijini hakuna, Masaki maji yanatoka temeke yamekatika, Wengine wanaweza kusoma wengine hawawezi kwa sababu hawana pesa.

    Sijuhi ni muungano gani wanaozungumzia hawa viongozi wetu??? KWa sababu nachafahamu mimi nia ya muungano sio sifa bali ni kupata faida ya muungano kuanzia elimu, siasa, uchumi na mengineyo. Sasa kama hayo mambo bado ni kitendawili ndani ya Tanzania sidhani kama yatatatuliwa na muungano zaidi ninachoona ni kuongezeka kwa matatizo yetu.

    Tuanze kwanza ndani ya nchi halafu ndio tuangalie nje.
    Mungu ibariki Tanzania......

    Halifa Mjengwa

    ReplyDelete
  6. Michuzi,

    Natoa maoni yangu hapa kwa sababu ninajua wewe una access na ikulu ! Tafadhali naoma uwaambie hao viongozi waliochoka kufikiri yafuatayo :-

    a) Kwanza Watanzania tumetukanwa sana na maamuzi yao mabovu ! Haiwezekani mtu ajifanye kutafuta ushauri wakati huo huo anataka kushauriwa jinsi anavyotaka yeye. Ashakum si matusi huwezi kuanza kujiuliza kama unataka mtoto wakati mke wako yuko hospitalini anatarajia kudeliver mtoto. Hiki ndio kiini macho kinachofanywa na hawa viongozi watatakaje ushauri sasa hivi wakati wameshaanzisha hiyo jumuiya bila ridhaa yetu , sasa Rais wetu katika kutaka kuwa political correct anajifanya kutafuta ushauri wa wananchi !


    b) Kama alivyosema mjumbe mmoja hapo juu bado tuna matatizo makubwa na muungano wetu ( Tanganyika na Zanzibar ) na mpaka leo kuna ishu nyingi hataujapatia ufumbuzi. Hata Rais aliadmit alipokuwa akifungua bunge kule dodoma sasa kama muungano unatupa shida kwa nini tusitafute ufumbuzi kwanza wa muungano huu muhimu sana kwetu kabla ya kukimbilia mwingine !

    c)Kusudi nchi ziungane lazima mwe na vitu vingi mnavyoshea in common ...Uganda museveni anaamini ya kuwa yeye anatakiwa kuwa Rais wa maisha , na jee tuna uhakika gani kama Uganda itaendelea kuwa stable once huyu bwana akistep aside. Kenya sasa hivi wanasalivate kila wakiangalia Tanzania na Economic potential yake in future na wanataka kutake over. Hivi kuna mtu yoyote amejiuliza kwa nini wakenya wanaataka sana huu muungano kwa nini hawakuutaka miaka ya 80 wakati tulipokuwa tunasubiri sukari ya mgao ? Jee ni kwamba wanatupenda sana au ?

    d)Mimi naamini huu muungano unakuwa catalyzsed na viongzi wachache ambao wana benefit kwa either kuwa wabunge au kupata nafasi fulani za uongozi , ila hauna faida yoyote kwa wazalendo !

    Mwisho ni lazima viongzi wetu wachague kati SADC na EAC , kwa mtazamo wangu naona tunaweza kubenefit sana toka SADC ............

    Wazanzibari ndugu zetu , mimi naaamini kabisa nyie mna uwezo wa kustopisha huu ujinga unaoendelea kwa kupingana na serikali ya bara , Mpango wenu kupata free port utakuwa ndoto na bandari ya mombasa itawasuck kabisa ... Zanzibar itakuwa wilaya katika huu muungano.

    ReplyDelete
  7. Ninafurahi sana kuona Ndugu zangu Watanzania mnajadili Maswala ya Muhimu Kama haya !!!!.Nakubaliana na mwandishi wa habari hiyo iliyoandikwa hapo juu.Kwanza ni lazima tuwe/tujitengenezee Ramani tunayoitaka ya Maendeleo yetu wenyewe sisi Wantanzania TU!!! bila ya kuhusisha nchi nyingine.
    Mimi binafsi ningependekeza tuangalie mifano mizuri kwa kuanzia na jirani zetu kama nchi ya Afrika Kusini; ni nchi pekee ambayo mpaka hivi sasa inaheshima kubwa Duniani hasa kiuchumi!! bado inabadili mifumo mingi ya zamani(enzi za ubaguzi wa rangi!) ili iweze kuwahusisha/kukidhi na kuwafaidisha wananchi wengi kama sio wote wa nchi Hiyo.Sisi wenyewe tunauwezo wa kuigeuza Tanzania kuwa moja ya nchi zenye nguvu kubwa Duniani, Watu tunao wenye vichwa, nia tunayo, na madhumuni pia tunayo !!!Kuna baadhi tu ya watu wachache bado wanaubinafsi walioiga kutoka wapi sijui ambao wengi wetu hatujui nia na madhumuni yao katika nyadhifa walizoko wakati huu. Tuwe makini/tukae chonjo!!! sana na watu hawa.
    Nchi itajengwa na sisi wenyewe Watanzani ndio tunauchungu wa maendeleo yetu wenyewe, tusipende kuiga kila kitu kinachoendelea sehemu nyingine duniani kwa sababu, sababu za hao walioamua kufanya mabadiliko hayo makubwa hatuzijui, au hata kama tunazijua wakati huo wa uamuzi unafaa katika nchi yao kwa kipindi na nafasi nchi hiyo/hizo zilipofikia kimaendeleo !!!.Kuna vitu vingi nchi yetu; wabunge lazima wakae kitako na kufikiri, kutunga, kupendekeza sheria zinazowanufaisha wananchi wa Tanzania; mfano hii habari ya kuruhusu "Dual citizenship" au "Raia wa nchi mbili" yaani Watanzania ambao ni raia wa nchi nyigine Duniani kuwa raia wa kudumu wa tanzania, maadamu wanahitimu kama 1) wazawa kwa kupitia wazazi wao, au wao wenyewe.hii ni hatua mojawapo ambayo itaharakisha maendeleo yetu sisi Watanzania.
    Ahsanteni, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania
    Ben.

    ReplyDelete
  8. Huu muungano hauhitajiki. Kuna jinsi nyingi tu za kushirikianan na kenya na uganda bila kuungana.

    Wakenya na Waganda ni washenzi sana. wakabila, wabinafsi na pia hatufanani kiustaalabu. Tukiunga itakuwa ngumu sana kuendana nao.

    Halafu hii serikali nayo imeshaunda bunge na baraza la mawaziri la EA bila ridhaa ya watanzania. Suala la kujiunda na jumuia ya EAC liltakiwa kupigiwa kura na watanzania wote.

    JK sijisha mambo yote ya EAC. Hii ni moja kali ya Kero za wananchi.

    ReplyDelete
  9. 1.Nakubaliana na maoni wa watanzania wenzangu jhapo juu wameongea mambo ya msingi sana.
    2.Nakubaliana na mchanganuo na mtanabaisho wa muandishi wa makala hiyo hapo juu aksante sana ndugu mwandishi.
    Kwa kuongezea tu hayo waliyosema wapenda nchi wenzangu ni kwamba:
    1.Sio Tanzania pekee haiko tayari kwa muungano hata Kenya na Uganda nao hawako tayari: nasema hivo kwasababu ukiangalia kwa undani utaona wakenya wana matatizo kede wa kede:
    i.Hawana "political stability" kupata katiba yenyewe wamerumbana mpaka wakapigana mawe
    ii.Wana ukabila uliokithiri wakikuyu kwa wajaruo sijui huyu mkamba! waungane kwanza wao ndani halafu waje watushawishi la sivyo wataeneza huyu mdudu wa ubaguzi kwetu "hatutaki"
    Waganda nao wamalize yafuatayo
    i.vita vya wenyewe kwa wenyewe "Lord resistance army" watokomezwe kwanza la sivo wataanza kutuletea masilaha huku kwetu tatizo la ujambazi lizidi
    ii. waimarishe demokrasia ya kweli nyumbani kwao
    Ni hayo tu mawazo yangu wadau tushirikiane kulipinga hili maana Tz ya leo siya wakati ule tulikua tunaburuzwa tu na viongozi wetu(sababu eti watz wengi walikua hawajaenda shule) wanafanya mambo kwa utashi wao tu bila ya kutusikiliza.

    ReplyDelete
  10. Naamini comment hapo juu kutoka kwa Ben ni kutoka kwa raisi wetu mstaafu,if so Asante raisi wetu kwa kutujali wananchi wako Mungu azidi kukubariki

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...