TIDO MHANDO ASTAAFU BBC

Mwandishi wa habari wa siku nyingi lTido Mhando leo amestaafu rasmi katika shirika la Utangazaji la Uingereza BBC kama mhariri wa idhaa ya kiswahili baada ya kushika wadhifa huo i tangu mwaka 1999.

Tido Mhando, ambaye amefanya kazi na idhaa hiyo ya kiswahili kwa miaka kumi na sita, ni mwafrika wa kwanza kushikilia nafasi hiyo ambayo muda wote ilikuwa ikishikiliwa na waingereza kutoka idara za utawala.

Wafanyakazi wa idhaa hiyo wakiongozwa na bosi wao mpya Solomon Mugera walipata fursa ya kumuaga Tido Mhando katika hafla iliyofanyika mara baada ya matangazo ya jioni siku ya Ijumaa.

Awali katika mahojiano na mtangazaji Ali Saleh kwenye kipindi cha dira ya dunia, Tido alisema anajivunia sana kuondoka akiwa ameiacha idhaa ya kiswahili ikiwa imevunja rekodi kwa idadi ya wasikilizaji ambayo imeongezeka kutoka milioni tisa na nusu alipoingia hadi kufikia milioni ishirini kwa wiki hivi sasa.

Katika tafrija hiyo, Tido Mhando aliwashukuru wafanyakazi hao kwa ushirikiano mkubwa waliompa kiasi cha kuweza kufanya mabadiliko makubwa katika idhaa hiyo.

''Katika kipindi cha miaka saba niliyokuwa katika nafasi hii tumefanikiwa kufanya mabadiliko makubwa sana ikiwemo kuweza kuwa ni radio ya kwanza BBC World Service kuweza kutangaza mpira wa Uingereza moja kwa moja, tumeongezewa muda wa kuwa hewani kwa kuwa na vipindi vingi sana.

"Lakini pengine mabadiliko nitakayoyakumbuka sana ni kuweza kuhamisha kabisa matangazo ya asubuhi na kuyahamishia Nairobi, yote haya yasingewezekana bila ushirikiano wenu'' alisema Bwana Tido.

Kumbukumbu: Tido Mhando ni mmoja wa watangazaji mahiri na wakongwe Tanzania imewahi kuwa nao.Alianzia redio ya taifa, Radio Tanzania Dar Es Salaam (RTD)kabla ya kuelekea Kenya ambako alifanya kazi kwa miaka mingi kabla ya kujiunga na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC.
Baada ya kuhamishia makazi yake London, Tido Mhando alipewa majukumu ya ukuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC mwaka 1999.Katika muda wake madarakani, Idhaa ya Kiswahili imepata mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na idadi ya wasikilizaji kupanda mpaka milioni 19.

Umbea: Baada ya kustaafu anatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania ambako haijajulikana atapewa majukumu gani. Kuna habari kuwa atakabidhiwa Tume ya Utangazaji Tanzania (TUT) inayojumuisha RTD na TVT, ili aindeshe kwa kutumia umahiri wake na kuifanya iendane na matakwa ya karne ya 21, kinyume na ilivyo sasa...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Bring home your massive experience kaka, our nation media need revemping big time!

    ReplyDelete
  2. Katika mahojiano ya BBC leo jmosi asubuhi, alisema kwamba mkataba haujaisha na wala hajafikia umri wa kustaafu ila ameamua kurudi nyumbani, kwa hiyo unachokisema michuzi inawezekana kina ukweli ndani yake kwamba ameitwa nyumbani ili kuliendeleza jahazi la habari, kama ni kweli nitampongeza kwa uamuzi wake wa busara welcome home Bro

    ReplyDelete
  3. Wishing you all the best Tido. I hope you will use your experience to try and help our falling RTD and TVT to come to life again.

    ReplyDelete
  4. Si astaafu tu kwani mpaka aendelee na madaraka?
    Bongo bwana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...