mkufunzi wa ngono salama akielekeza matumizi ya kondom za kike kwenye banda la unaids leo.
wiki ya umoja wa mataifa imeanza rasmi leo na kila taasisi ya umoja huo imeanda maonesho kwenye viwanja vya jumba la makumbusho, dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. wacha tufe tu lakini hiyo kondom ya kike haitafanya kazi.

    ReplyDelete
  2. Naona hao wanafunzi kwa nyuma kule wanacheka kama vile kuna kichekesho kinafanyika hapo. Hii ndio tabia inayopelekea kutozingatia hata kile wanachofundishwa hapo. Hili jambo la kujikinga maabukizi si la mchezo kabisa, huu ugonjwa ni hatari na hauchagui. Sasa sitegemei wanafunzi kama hao watatilia maanani kweli na kuwa na msemo wa kutaka kitu kama hicho kitumike kama wakibanwa kwenye 'kona'.

    ReplyDelete
  3. Kaka Michuzi,hii sasa kali,naogopa hata kuchangia mada.

    ReplyDelete
  4. Inapendeza kuona watu wakitoa hamasa juu ya mapenzi salama hadharani, kwa wale walioko serikalini watakuwa wananielewa juu ya matumizi ya pesa ya TACAIDS katika kueneza VVU. Inauma kuona budget ya kuhudumia nchi nzima katika VVU inakaliwa na watu wawili na bila kujali umuhimu wake kwa watu wengine.
    Michuzi nadhani unanielewa juu ya hili, kwa ufupi ni seminar za ukimwi na matumizi yake maofisini najua nawe ni mmoja wa watafunaji hapo kwenu daili nuez.
    KIJU

    ReplyDelete
  5. Eh! Anaelekeza matumizi ya kondomu ya kike kwa wanaume! Na labda ni mkakati sahihi.

    ReplyDelete
  6. ngono salama!! mmhhhhhhhhhhhh
    Naona huyo mwanaume naye anasikiliza kwa makini juu ya hiyo kondom ya wanawake. Mie nafikiri hii ni vizuri, ila nina wasiwasi hawa wanaume wanaweza kukataa ngono wakigundua kuwa mwanamke amevaa hiyo kondom-

    cha maana zaidi katika hii vita ni kuwaelimisha akina mama kujua kusema hapana kwa ngono ambazo hazina mipira-mara nyingi akina mama wanalazimishwa kufanya ngono zisizo salama sababu za kiuchumi. wanaume ambao hawapendi kuvaa mipira ya kiume nafikiri hawatapenda mipira ya kike pia.......

    ReplyDelete
  7. Hata mimi nacheka kuona anatumia mboo bandia katika demonstration! Tena ina mapumbu.

    ReplyDelete
  8. UKIMWI unatufundisha kuzingatia uaminifu, ukweli, uwazi, kuepukana na unyanyapaa na kulinda afya zetu na jamii yetu. Kondomu ya kike ni nzuri hasa kwa kuwa wanawake wananyanyaswa sana na wakati mwingi wanashinikizwa kufanya ngono zembe. Hivyo wakichukua uamuzi wa kulinda afya zao, basi tuwapongeze na kuwasaidia. Tatizo ni kwamba huyo mkufunzi amekosea kidogo katika kuonyesha vielelezo vyake. Pengine ingesaidia angemwachia mwanamke atoe mafunzo hayo.

    Jambo la kusikitisha ni kwamba UKIMWI umefanywa mgodi wa watu wengi[Sina maana ya kuwa huyo pichani ni miongoni mwao]. Na hizo kondomu za kike zinawafikia akina nani kwa bei gani? Mama, dada, bibi, na shangazi zetu huko vijijini wanaziona hizo? Je walala hoi wanaziona hizo/ Watazipata kwa bei gani? Kweli tusipoangalia UKIMWI utawaangamiza zadi watu wenye maisha duni! Mungu kaibariki sana Tanzania na Afrika kwa ujumla. Sasa tubadilishe na wimbo wa Taifa tuseme Mungu Iokoe Tanzania na Afrika!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...