MDAU KANITUMIA TANGAZO HILI NILITOE KWENYE BLOGU YETU. NAMI, HUKU NIKIKARIBISHA VITU KAMA HIVI, NALITOA KAMA LILIVYO. MDAU YEYOTE ANAKARIBISHWA KUTOA LAKE JAMBO KWENYE BLUGO HII YA WATU WA AFRIKA MASHARIKI


FIRST AIR TRAVEL
7699 BATH ROAD MISSISSAUGA ONTARIO L4T 3T1 CANADA


TOLL FREE 1-866-861-6584
TEL 905-461-1139/1140
FAX 905-481-2445
EMAIL: mkermali@firstairtravel.net



WE ARE SPECIALIZED FOR TRIPS TO AFRICA AND AROUND THE GLOBE OUR MAJOR DESTINATIONS ARE:

*DAR-ES-SALAAM* *KILIMANJARO* *ZANZIBAR* *ENTEBBE* *NAIROBI* *MOMBASA* *ACCRA*
*LAGOS* *JOHANNESBURG* *CAPETOWN* *DURBAN* *LILONGWE* *LUSAKA* *ADDISABABA

WE ALSO COVER PART OF MIDDLE EAST, ASIA, EUROPE AND INDIA SUB - CONTINENT

OUR QUOTATIONS HAS NO HIDDEN CHARGES.


DO TRY US AND JUDGE BY YOURSELF THE DIFFERENCES FROM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Michuzi kaka, are u getting paid na hawa jamaa? If not, I would advise uanze kuwachaji watu wanaotoa matangazo ya biashara. Hakuna free promo dunia hii.

    ReplyDelete
  2. Michuzi hawa gabachori wametuliza kwa kutuingiza mkenge na mikataba feki ya generreta RICHMOND ECONOMY SABOTAGE COMPANY LIMITED...tehe...tehe...tehe..sasa naona unamtangaza tena Kermali hapo juu, au unataka tena baadae aje kupewa tenda ya kununua ndege za Air Tanzania kwa kigezo kwamba ana uzoefu wa Air Travel???.Wahindi wanamaliza uchumi wa Tanzania jamani.

    ReplyDelete
  3. michuzi sasa naona unaharibu editorial space yako. hebu waambie walipie banner. Mimi nimeanza kupokea matangazo kwangu tena nalipwa. iweje wewe femasi namna hiyo unafanywa bure?

    ReplyDelete
  4. Sasa hii ni blog ya picha au maelezo na matangazo?

    ReplyDelete
  5. Ni jambo la kusikitisha kuona ubaguzi dhidi ya wananchi kwa kuwa sio Waafrika kirangi. Mara nyingi Ulaya na Marekani, Waafrika wanalalamika wanabaguliwa na wazungu lakini sisi tunafanya ubaguzi huo huo dhidi ya wahindi wa Africa. Niger inawafukuza Waarabu walioishi huko zaidi ya miaka 30 kwa kuwa sio Waafrika wa Kiniger bali ni Wachadi waliokimbia vita. Je, kama Watanzania 150,000 wakifukuzwa Canada kwa kuwa ni wakimbizi feki hata kama wengine wana uraia wa Kanada, Utajihisi vipi kama Mtanzania. Wachadi wengi wa Kiarabu wamezaliwa huko Niger lakini wanafukuzwa na biashara yao kuchukuliwa na Serikali. Wale ambao wanataka uchumi wa Tanzania uwe chini ya Waafrika basi wafanye kazi ya kuiweka uchumi huo chini yao, lakini wasilalamike wageni wakichukua uchumi huo kwa kuwa wao aidha hawana ujuzi, wavivu, au hawana fedha za kuanza biashara. Pia, kwa wale ambao kisomi ni kidogo, sheria za kiimataifa hairuhusu Tanzania kumnyima mgeni kufanya biashara awe Mhindi au Mzungu la sivyo Tanzania pia itanyimwa kuuza mauzo yake nje. Pia, Tanzania kama nchi masikini haina ubavu wa kunyima mfanyabiashara atakayeleta fedha na kazi katika uchumi wa Tanzania, awe Mhindi, Mwaafrika au Mzungu. Kwa wale wanaolalamika uchumi unachukuliwa na wageni, aidha wafanye bidii kufanya kazi au wasome sheria za kimataifa za kibiashara kabla ya kuanza kubagua watu bila ya sababu za kimsingi.

    ReplyDelete
  6. Tunakuheshimu KERMALI,acha maneno na mambo haya.Misafara ile ni ya MAMBA nyie KENGE haiwahusu!!!

    ReplyDelete
  7. Kermali huwa na deals nzuri sana za tickets kutokea USA. Mbona watu wengine mnaleta ubaguzi wenu hapa.

    ReplyDelete
  8. Kaka Michuzi naomba huu uwe ndo mwanzo na mwisho wa matangazo otherwise this lovely blog of yours will be inundeted with ads from all over the world(by the way na mimi nina ka kwangu) na huo ndo utakua mwanzo wa kupoteza ile ladha yake halisi inayotufanya sote tuwe tuna visit daily.

    Watanzania tu wabaguzi na cha kusikitisha zaidi hatujijui kuwa tuko hivyo. If hadi leo hii unaweza kukataliwa na wazazi wako usimuoe umpendae eti kwa kuwa ni kabila/ukoo fulani au dini fulani-huu ni ubaguzi. Wapo watu ambao wana elimu zao lakini wamekosa kazi kwa kigezo cha jinsia zao-eti kwa kuwa ni wanaume/ wanawake au wasenge-huu ni ubaguzi. Na ni wangapi wamebaguliwa kwa kigezo cha umri wao? Tunalia sana kwa ubaguzi wa rangi tunaofanyiwa lakini hata sisi pia tumo kwenye hili-hundreds of tourists are being attacked and robbed-and they continue to be targeted on a daily basis just bse of their skin colour-bila hata kujua wamebeba nini! Huyu muhindi (im not sure kama ni kweli?) kuweka tangazo lake hapa naamini ni kwa nia njema na anataka kusaidia tu, and after all most of ads unazoziona kwenye luninga unapokuwa home ni za kina nani?????

    ReplyDelete
  9. Sidhani kama kuna ubaguzi wowote uliozungumzwa hapa,suala ni kwamba kuna jamii ya watu mostly INDIANS wanawaona Waafrika kama maisha yao hayana thamani, wakiwaajiri waafrika wanawalipa as little as Tsh 35,000 per monthy.Hili suala liko wazi wala halihitaji utafiti, sasa huu tuuite ni utumwa, ubaguzi au kutokuthamini maisha ya binadamu wengine??? Ndugu zangu Watanzania/Waafrika/Asians/Europeans naombeni mchango wenu kwenye hii mada.

    ReplyDelete
  10. Africa is for africans just as India is for Indians.Hakuna mtu mbaguzi duniani kama mhindi.Akibaguliwa na mzungu huwa anajidai kumpenda mwafrika wakati yeye ni mbaguzi wa mwafrika kuliko mtu mwingine yeyote duniani.Kule India weusi ambao wanaaminika kuwa wanatokea Afrika mashariki,zanzibar na maeneo ya mwambao wa Tanga wanaitwa "untouchables".Wanafanywa kama wanyama,wanabaguliwa kwa sababu ni weusi.Sasa nani amfunge paka kengele?Mhindi ni mbaguzi kwa hiyo asishangae anapobaguliwa.Majuzi ripoti ya bbc imetoa takwimu kwamba India na China ndio nchi zinazoongoza duniani kwa kutoa rushwa nk.Huo ni uongo?Sasa jiulize nani ni chachu ya rushwa barani nchini Tanzania kwa mfano?Hapo ndio kesi kama hizi za Richmond ambayo serikali ya Tanzania haioni hata sababu ya kuulezea umma kinagaubaga juu yake zinapokuja.Wahindi lazima mjirekebishe kama mnataka kuonekana waungwana.Ningependa kuona wahindi wanashiriki kwenye ujenzi wa nchi.Niwaone wahindi wakiwa polisi nchini Tanzania,wakiwa wanajeshi nk.wajichanganye na watanzania na sio kuunda little india in Tanzania.Hapo mambo yatakuwa mswano.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante kwa maoni yako---maoni yako hayakunishangaza. Mimi ni mhindi, mzaliwa wa Tz, na tokea utotoni tabia za wahindi wenzangu zilinisikitisha; Wengi ni marafiki, na ndugu zangu hata! Kwa upande wangu, najaribu kuwaelimisha, na kuwaonyesha kwa mifano, jinsi ya kuonyesha utu kwa wote. Kwa nini? Sisi wote ni bin-adam, na siku ya Kiyama mbele ya mwenyezi tutajitetea vipi? Pia, nawajua wengi wenye fikra sambamba nami

      Delete
  11. Napenda kutoa maono yangu kuhusu pointi alizozitoa Covert na Anony wa Octoba 28 (6:22). Mimi ni anony 3:59 na si Kermali.
    Covert ana pointi kuhusu mishahara ya wafanyakazi wanaolipwa ni midogo lakini si kosa la Wahindi bali ya serikali. Serikali ndio inayopanga mishahara ya chini na wafanyakazi wa nyumbani hawapo katika hii sheria wa mshahara wa chini kwa kuwa wananchi wengi wanawategemea hawa wafanyakazi nyumbani kwao na hawana uwezo wa kuwalipa mshahara wa kima cha chini kwa kuwa wao wenyewe wanalipwa mishahara midogo. Kama issue ya mishahara basi wote tumekosa kwa kuwanyima haki wafanyakazi wa nyumbani wengi wakiwa kutoka familia masikini huko shamba. Tunalotakiwa kufanya ni kuitaka bunge ipitishe sheria ya kuwapa wafanyakazi wa nyumbani mshahara wa kima cha chini kama wenzao kama kianzio sio TSHS 10,000. Hauwezi ukalalamika kwamba mhindi halipi mshahara zaidi wakati waafrika pia wanafanya hivyo hivyo. Walmart ya Marekani ni kampuni kumbwa duniani, ilifanya biashara ya bilioni 200 dola mwaka jana lakini inawalipa wafanyakazi wake kima cha chini, Je, mbona serikali ya marekani haimpeleki kortini walmart au watu hawaachi kwenda walmart? Je, convert unaweza kusema kwamba walmart wanawabagua wafanyakazi wao? Historia inaonyesha kuwa sheria kali ikitungwa inawabadilisha tabia za watu. Ubaguzi umepungua mno Marekani kutokana na sheria zake za kuwalinda watu dhidi ya ubaguzi wa kila aina. Kama majaji wanachukuwa rushwa Afrika basi tuwafukuze kazi sio kulalamika mhindi anatoa rushwa. Pia, Wahindi na Waarabu Tanzania wanasaidia kiuchumi, tujaribu kutoa pointi kwa kutumia data sio feelings zetu. Leo, kina bakhresa na gulamali na dewji wanalisha nchi, maelfu ya wafanyakazi na wakulima wanawategemea kwa biashara yao. Si jambo la msingi kusema kuwa waafrika peke yao wanasaidia uchumi wa Tanzania bila ya kutoa sababu za kimsingi kama data za kodi za TRA.
    Anoni 6:22:25, naelewa kwa kusema kwamba Afrika ni kwa Waafrika, lakini hatuwezi kuichukua na kuiendesha Afrika peke yetu. Hatuna fedha, utaalamu au elimu ya kufanya hivyo. Kama nchi masikini mpaka leo tunategemea nchi za ulaya kulipa bili ya nchi. Tunawaomba Wahindi watuelimishe na kututibu wananchi wetu, tunawaomba Wajapani watujengee barabara zetu, tunawaomba Wachina watujengee treni, na kadhalika.
    Rushwa ipo kote duniani na haitaondoka. La muhimu ni kujiinua kiuchumi ili tuweze kujiendesha kiuchumi na kuwa na sheria ya kuwalinda wananchi dhidi ya ubaguzi na rushwa. Kuhusu Wahindi kuwa jeshini, nilishawaona pale Upanga lakini ni wachache, hauwezi ukamlazimisha mtu kwenda jeshini au polisi wakati mshahara wake ni mdogo. Hii haimaanishi kabisa kuwa hapapendi nchi yake, ingekuwa hivyo basi canada ingewafukuza wananchi wake kwa kuwa jeshi lote ni la kizungu japokuwa nchi ina wakanada asilimia 50% waliozaliwa nje au wazazi wao wamezaliwa nje ya Kanada. Pia, nchi kama marekani, watu wanaojiunga na jeshi ni masikini wa hali ya chini, wengi wao, asilimia 70, wana elimu ya sekondari tu na aidha ni waafrika au waspenishi wa kimarekani. Sasa, anony anataka matajiri au wananchi wengine wasiowapeleka jeshini au polisi watoto wao wafukuzwe marekani?
    Wananchi wote tunatakiwa tujirekebishe kwa kuheshimu watu wote, ubaguzi hautakwisha duniani, ikiwa tutakaa na malalamiko yetu basi tutazidi kujikuta tunatawaliwa na kulishwa na dunia. Action speaks more than words.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...