The Oxford dictionary defines the term xenophobia as "hatred or fear of foreigners."

There is a new wave of xenophobia that is slowly creeping into the East African region that if not nipped in the bud, could undermine the ongoing efforts at political federation, the much cherished goal of our region.

Click here to read more.....

http://www.habaritanzania.com/articles/1595/1/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. hakuna xenophobia yoyote hapo,labda angesema paranoia.je jumuia ya ulaya kuzicheleweshea uanachama nchi za ulaya mashariki pia ni xenophobia.hili swala ni sensitive na tunahitaji kuwa very discreet katika kufanya maamuzi.

    ReplyDelete
  2. MIMI NAONA TUJIUNGE TU NA HUU MUUNGANO WA KENYA NA UGANDA NA TANZANIA, SIONI SABABU YA KUWA WAOGA ETI KWA SABABU HATUJUI KIMOMBO, AMA TUTAPOTEZA KAZI? SASA KIMOMBO TUTAKIJUA LINI WABONGO? MSILAUMU MUUNGANO MUMLAUMU NYERERE AMBAYE YEYE ALIPATA ELIMU NZURI YA MKOLONI AKAJUA KIMOMBO LAKINI AKAWA MJANJA AKAWAFANYA WATANZANIA WOTE WENGI WAO WAWE MAMBUMBUMBU KWA KUANZISHA KISWAHILI NA KUJAZA WALIMU WA UPE MASHULENI NA SASA MATUNDA MNAANZA KUYAONA, ELIMU YA PUMBA MAMBUMBUMBU WENGI NA USWAHILI NDIYO TULICHOJALIWA, SASA TUNAOGOPA HATA HAWA NEIGHBOUR HATA UGANDA JAMANI ILIYO KUWA KWENYE VITA VYA MUDA MREFU? AIBU AIBU TUPU WATANZANIA UMBEYA NDIYO TULICHOBAKIA NACHO...!

    ReplyDelete
  3. Muungano huo una faida gani? Eti, kwa sababu Ulaya imeungana! So what!

    Tulipoteza Ujamaa wetu eti kwa sababu Urusi ilisambatika!

    lazima kuzingatia ukweli wa kimantiki kuwa pale palipo na matabaka katika umma, mwelekeo wa mkono wa kushoto (ujamaa) ndio dawa! Ubepari utazaa Ujamaa tena...yaani vyama vya siasa vyenye mkabara wa kushoto vitakapoanza kuongoza nchi za Ulaya na Amerika...sijui nasi tutageuka mkono wa kushoto...sijui!

    ReplyDelete
  4. Kwanza watu humu mnachanganya mambo,watu hutupingi economic integration tunapinga uharakishwaji wa political federation,wakati hata masuala ya customs union bado yana tusumbua. Mimi nadhani kwamba political federation au shirikisho linahitaji muda na tena muda wa kutosha , labda baada ya kujaribu jumuiya ya uchumi na kufanikiwa. Tukiwa tunategemea nchi yetu iendeshwe na makampuni madogo , yaani small medium enterprises, sidhani kama suala la kiingereza litakuwa lina umuhimu sana, tunaweza kubaki kama tulivyo sasa, kiingereza ikiwa kama corporate language. Kutokujua kiingereza siyo ujinga, ulaya kuna nchi tatu zinazo zungumuza kiingereza, UK,IRELAND NA NORTHERN IRELAND wengine wotw wanatumia lugha zao na bado wameendelea, hili swala linahitaji kuzungumiziwa zaidi watu wajue, kiswahili hakina ujinga wowote. Shirikisho liwepo lakini lije baada ya muda wa kutosha.

    ReplyDelete
  5. GURU ufafanuzi wako ni mzuri sana,shukrani kwa kuweka mada sawa.

    ReplyDelete
  6. Nakubalina na Msami. Nyerere alikuwa anongea QUEEN'S ENGLISH! Lakini katufanya wajinga na kufanya watu wadharau English kwa kusemaa eti KASUMBA.
    Matunda tunaona leo. Broken English! AIBU!

    ReplyDelete
  7. Guru I fully support u, umetoa comments iliyoenda shule. Tell them.... Japan and other European countries are not using English and they are doing better economically.

    ReplyDelete
  8. Naomba mdau mmojawapo atueleweshe wale ambao hatuna taarifa za kutosha kuhusu huu muungano wa jumuiya ya africa masahriki
    1) je ni uchumi tu?
    2) au tunaungana kila kitu kama Tanzania na Zanzibar, yaani kuwa na rasi mmoja, pesa moja n.k.?

    Hii itasaidia kutoa maoni yaliyoenda shule. Au kama kuna tovuti zinazoelezea hili swala naomba uzitume.
    Ahsante kwa mchango wako!!

    ReplyDelete
  9. Muungano unaotakiwa africa mashariki na africa kwa ujumla ni muungano wa kila kitu,yaani kila nchi ifikie wakati iwe na uhuru mdogo wa maamuzi ya mambo ya ndani kiutawala(cessetion of territorial and state sovereignity? na badala yake EAC kwa africa mashariki na AU kwa africa hapo baadae ndio ziongoze. lakini hii ni nadharia zaidi ya vitendo maana hadi leo kuna nchi zenyewe tu bado hazijaungana . suala la rwanda na burundi ni tete lakini naamini bado liko awali sana hata kuliongelea,Afrika mashariki bado haijafikia muafaka wa kuungana,bado tuko kwenye maongezi,hawa watu wanataka kujiunga kwenye muungano wetu... upi huo?si bado hatujaungana? ngoja tuungane kwa nafasi ambayo haitakua na mikwaruzano na migogoro then tuangalie vigezo vya kumpa mtu wa nje anayetaka kujiunga.charity starts at home.

    ReplyDelete
  10. TULIWAAMBIA HUYU KIKWETE ATAWALETEA SHIDA SHIDA SAAANAAA MKANIBISHIA SASA ONENI AMEKAA MADALAKANI LESS THAN 200 DAYS ONA ALIVYO PUSH HII KITU WAKATI AKIJUA KUNA MAREKEBISHO MENGI YANATAKIWA LAKINI KATIKA KUONESHA AMEDHAMILIA ALIANZISHA HATA WIZARA YA AFRICA MASHARIKI NA KATI. HUYU JAMAA NA RAFIKI YAKE LOWASSA NYERERE ALITAMKA TANGU ENZI ZILE HAWAFAI SASA LEO MTAKOMA WATANZANIA SISI TUKO MBALI HUKU NAWASIKITIKIA NDUGU NA WAZAZI WETU NAFIKIRIA JINSI YA KUWATOA HUKO KWENYE GIZA TORORO LINALOSABABISHWA NA NJAA ZA WATU MPAKA WATOTO WA VIGOGO KUTUAGIZIA MAJENERETA KIBAO ILI WAPATE CHOCHOTE CHA KUSHIBISHA VITAMBI VYAO. SASA HUU MUUNGANO KESHO UTASIKIA SUDAN, SOMALIA NA CONGO WAMEJIUNGA HAPO SASA KAZI INAKUJA. LEO WAPO BULUNDI NA RWANDA KENYA NA UGANDA TUSUBIRI KESHO TUTAONA. NA WABONGO MTAKACHO FAIDIKA NACHO NA AMBACHO MMEONESHA UMAHILI MKUBWA NI USWAHILI NA UMBEYA LAKINI NDUGU ZANGU HIZI NCHI KENYA UGANDA BURUNDI NA RWANDA NI MASOMI NA MAJANJA KIAKIRI NA MALI!MTUSI MKIKUYU NA BAGANDA? WALLAHI MTAKOMA, HAYA KWA UPANDE WA MIFUGO MASOMALI YATAMALIZA ZOTE. KAMA RAIS ALITAKIWA MWISLAMU KWA NINI MLIMWACHA SALIM AHMED SALIM? MTAMKUMBUKA KAKA SUMAYE TENA YUPO KAJITULILIA HAVARD HATAKI SHWALI NA KIKWETE....POLENI NDUGU ZANGU ANZENI KWENDA TUTION ZA KIMOMBO!

    ReplyDelete
  11. Muona Mbali Finland
    kwa mawazo yangu ya juu juu,Swala la nchi kuungana kiuchumi au kuwa kama shirikisho linaweza kuwa la faida,lakini je unaungana na nani?na utafahidika na lipi?Tannzania kama nchi lingetafuta njia ya kujikomboa kiuchumi yenyewe bila ya kufikiria muuungano utaisadia,angalia demokrasia ya Tanzania na hizo nchi,angalia uwezo wa ushindani wa bidhaa za Tanzania ktk hilo soko,je ni hafifi au zinauzika,hili jambo tukikurupuka tutakuja kujutia,kwanza inawezakuwa gharama za kujiendesha kwa hilo shirikisho likawa ghali na bajeti ya nchi baada ya kufanya vitu vingine itakatumika,Tanzania ikae chini ifikirie nini cha kufanya kutatua matatizo sugu ya umeme,huduma duni za afya,mlundikano chuo kikuu na elimu inavyodorola,hili jambo la kuungana lisiwe la kisiasa tu ila lizingatie hali halisi,tumejifunza nini kuvunjika kwa shirikisho la East afrika 1977?kuna kitu tulijifunza,kweli kila siku naamini uharibifu mwingine anaoupata masikini unatokana na umasikini wake mwenyewe,inawezekana historia ikatusuta,Tanzania inahitaji kiongozi muona mbali na sio mfanya maamuzi kwa kukurupuka.Muona mbali Finland

    ReplyDelete
  12. Tanzania tuna kero za muungano harafu tunataka kuungana na kenya na Uganda!!!! Tumalize Mambo Zenji hasa pemba writeoff U-CUF uliojichimimbia mzizi then tuulizana kama Tuungane na Majirani Zetu!! Mheshimiwa Mjomba.....!!! Ukienda msiba aliyefiwa utamjua atakuwa amevaa.....!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...