Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2007

    Atakoma na Kampuni yake. Anajifanya Mr. "Msafi" kumbe hakuna usafi wowowte! Usifanye mchezo na pesa bwana. Hakuna asiyependa pesa hapa. Hakuna usafi mbele ya pesa bwana. Ebo!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2007

    Kipanya huo sasa ni ugomvi, ulitegemea PCB wafanye nini? After all wao ni Protection of Corruption Bureau na sio Prevention of .... Mwacheni Mjasiriamali apumzike!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2007

    Jamaa aliyetinga BlueIce ana ''uwalaza'' familysize... Je ndiye Mjasiriamali?? nifahamisheni...

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2007

    Mimi uongo huwa sipendi na hupenda kusema straight.

    Acheni kumwonea Mkapa.

    Azimio la Arusha lilokuwa likikataa viongozi wasiwe na makampuni na kuwa wakurugenzi wa Makampuni lilishafutwa kabisa.

    Kwa sasa Sasa viongozi wanaruhusiwa kuwa na Makampuni binafsi na kuwa wakurugenzi wa makampuni binafsi na kufanya biashara.

    Sasa kama Mkapa ni mkurugenzi na anamiliki kampuni na ana jengo ambalo kafanya kitega Uchumi tatizo liko wapi? Ni haki yake.Ana uhuru wa kuamua nyumba hiyo akae au apangishe.

    Nadhani kuna watu au bado wanaota ndoto za Azimio la Arusha au wako kwenye uchafuzi wa majina usiokuwa na sababu.Mwacheni jamani apumzike.

    Kama kaiba mchukulieni hatua lakini oh kakopa benki! halafu kanunua Jengo !halafu jengo hilo kalipangisha!

    Kosa lake nini hapo? hilo deni atalipa.Shida iko wapi hadi aandamwe?Ingekuwa kachukua pesa hizo bure hilo ni jambo lingine.Mtu kakopa na ushahidi mnao,sasa kapangisha hilo jengo ili kodi ipatikanayo kwenye hilo jengo atumie kulipa deni hilo alilokopa kwa kodi anayokusanya.Tatizo liko wapi.

    Mabenki yanakopesha yakiona mradi utalipa.Kumkopesha hela za kununua jengo si ajabu ili mradi waliamini kuwa pesa hizo zitarudi kupitia kodi ya hilo jengo.Yeye ana haki kama raia mwingine.Raisi pia ni raia mwenye account benki na mteja wa benki kama mteja mwingine yeyote.Kule Benki ana haki ya kuweka fedha,kuchukua na kukopa akitaka.

    Hajaitia hasara benki.Na benki yoyote ya biashara iko tayari kufanya biashara na yeyote inayoona anaweza kulipa.Sasa mtu kama Raisi akienda kukopa kwa nini wasimwamini wakampa haraka.Raisi anajulikana ana mafao yake ya kustaafu mazuri tu ambayo benki yaweza tumia kama dhamana hata kama hana mali ya kuweka kama dhamana.

    Watanzania tuwe fair kwa viongozi wetu.False accusations si nzuri.Hebu tumheshimu pia.Tumpe nafasi apumzike.

    Na waandishi wa habari ni vizuri muwe na upeo mkubwa wa kuchambua na kuandika mambo.Waandishi wa habari ni walimu wa jamii ukiandika umbeya utakuwa na jamii ya wambeya lakini ukiandika vitu vilivyochambuliwa vizuri ukienda mitaani utakuta watu wachambua vizuri suala liloandikwa na chombo cha habari kwa upeo mkubwa.Katika hili la Mkapa na kampuni yake na hilo jengo lake alilopangisha waandishi mmetuangusha.You have shown us, that your understanding is stll below the sea level.Jitahidini tafadhali.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 31, 2007

    Mjasiriamali au mwizi?Na hosea jiangalie sana unastahili kitanzi kama sadam.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 31, 2007

    Kwanini tunaogopa hata kuwanunia viongozi wetu?

    Kitila Mkumbo



    KATIKA makala yangu ya wiki jana nilijenga hoja kwamba CCM si tu kwamba imeshindwa kukabiliana na maadui ujinga, maradhi na umaskini, bali yenyewe imegeuka kuwa ni sehemu na kiranja wa maadui hawa.

    Nikajenga hoja pia kwamba hatua ya kwanza ya kuwashinda maadui hawa watatu ni kuing’oa CCM madarakani.

    Nimepokea maoni kadhaa kutoka kwa wasomaji kwa njia ya simu na e-mail kuhusu hoja zangu hapo juu; kama kawaida kuna waliokubaliana na kupingana na hoja zangu hizi.

    Si kawaida yangu kugeuza maoni ya wasomaji wa makala katika gazeti hili kuwa ni mada za kujadili.

    Hata hivyo kuna maoni ya watu wawili ambayo nimeona niyawakilishe hapa na kuyajadili.

    Nimefanya hivi baada ya kutafakari na kujiridhisha kwamba maoni haya yanaweza yakawa yanawakilisha maoni ya Watanzania wengi kwa kiasi chake.

    Maoni ya msomaji wa kwanza yanasema hivi: “Nimesoma makala yako katika gazeti la Tanzania Daima na kwa kweli ulikuwa na ujumbe mzito. Mimi nimepita katika nchi mbalimbali lakini sijawahi kuona nchi yenye watu wapole na ambao wako mbali na serikali yao kama Tanzania, nchi ambayo waziri anaweza kusema watu wale majani ili ndege mbovu inunuliwe kwa ajili ya rais na watu wale wakakaa kimya!”


    Maoni ya msomaji wa pili yanasema hivi: “Kaka, mimi naikubali makala yako. Lakini je, wewe unafikiri kweli sisi Watanzania tunaweza kuitoa CCM madarakani? Kaka wewe inaonekana huijui CCM.

    Kwa taarifa yako, CCM ina mtandao mzito kuanzia wala rushwa na walinda wala rushwa kama vile PCB.

    CCM ina fedha za kumwaga. Kwa hiyo kupambana na CCM ni kujitafutia balaa na hatari kubwa.

    Basi kaka mimi naomba utushauri tufanyeje kuleta mabadiliko katika nchi hii bila sisi wananchi kuathirika kimaisha.”


    Kama nilivyosema, maoni yote haya ni ya msingi na kwa kiasi fulani yanawakilisha maoni ya Watanzania walio wengi.

    Ni kweli kabisa sisi Watanzania tupo mbali na serikali yetu kama alivyosema msomaji wa kwanza hapo juu.

    Tukishawachagua viongozi wetu tunafikiri tumemaliza kazi na yote watakayofanya ni juu yao.

    Kwa hiyo ukiwa kiongozi Tanzania una uhuru wa kufanya jambo lolote bila hofu ya kuulizwa wala kununiwa na mtu yeyote.

    Katika nchi nyingi hapa duniani zikiwemo za kidikteta, isingewezekana waziri awatukane wananchi kwa kiasi alichosema msomaji hapo juu na bado akaendelea kuwa waziri.

    Tumeshuhudia pia jinsi ambavyo viongozi wa serikali ya CCM wamekuwa wakitoa ahadi hewa kila kukicha lakini hakuna wa kuwauliza.

    Hivi karibuni, kwa mfano, tuliahidiwa umeme wa dharura kwa mbwembwe na kila kiongozi wa nchi hii, lakini tuliendelea kubaki kwenye giza hadi mvua iliponyesha.

    Ukiacha magazeti machache yaliyoonyesha kukerwa na utapeli wa serikali na Richmond kuhusu umeme wa dharura, Watanzania tulio wengi wakiwemo wabunge wetu tulikaa kimya kama vile hakuna kibaya kilichofanywa na serikali.

    Wakati mwingine ni vigumu kujua ukimya na upole wetu ni kwa sababu kwamba tunawaamini sana viongozi wetu au kwa sababu tunawaogopa!


    Maoni ya msomaji wa pili yanasikitisha na kutia moyo vilevile; yanasikitisha kwa sababu yanaonyesha jinsi Watanzania tulivyojikatia tamaa na tusivyojiamini linapokuja suala la kukabiliana na madhila ya viongozi wa CCM.

    Kwa maoni ya msomaji huyu ni kama vile haiwezekani kuitoa CCM madarakani, kwa hiyo tuendelee kuvumilia tu. Kwa upande mwingine maoni ya msomaji huyu yanatia moyo kwa sababu ameuliza tufanyeje ili sisi wananchi tuweze kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko katika nchi yetu.

    Swali hili limenisukuma niandike makala hii na kukatisha mfufulizo wa makala niliyoianza wiki iliyopita.

    Kwa hiyo katika makala hii ninajadili baadhi ya njia ambazo wananchi tunaweza kuzitumia katika kushinikiza mabadiliko na hata kubadili uongozi katika nchi yetu.

    Hakuna fomula ya namna ya kushiriki kuleta mabadiliko. Jambo muhimu la kuzingatia katika kuleta mabadiliko ni kuwa wanasiasa huwa wanaweza kubadilika pale wanapogundua kuwa idadi kubwa ya wale wanaowaongoza wanataka mabadiliko.

    Kwa maana nyingine ni kuwa mabadiliko ya kisiasa huja kwa shinikizo na si kwa hiari ya viongozi waliopo madarakani.

    Kwa hiyo cha msingi ni kujaribu kushiriki katika kufanya kila liwezekanalo kuwaonyesha watawala kuwa wanachokifanya hakipendezi.

    Kuna njia nyingi rahisi na ngumu za kushinikiza mabadiliko.

    Njia rahisi kabisa ni ya kuwanunia viongozi pale wanapofanya jambo lisilopendeza.

    Jenerali Ulimwengu aliwahi kuandika katika moja ya rai zake enzi hizo kuwa Watanzania tunaogopa hata kuwanunia viongozi wetu.

    Nafikiri kauli ya Ulimwengu ina uzito zaidi leo kuliko hata kipindi alipoitoa.

    Watanzania hatuna tabia ya kuwanunia viongozi wetu.

    Tunawaona viongozi wetu kama vile ni miungu watu, wasioweza kukosolewa.

    Lazima tubadilike kama tunataka mabadiliko, maana haitakuwa rahisi kwa viongozi wetu kubadilika kama watakuwa wanafanya mambo ya ovyo na sisi tunawachekea tu.

    Mwandishi Jonathan Maitaland katika kitabu chake ‘Vote for Who?’ anasema kabla ya kuwalaumu viongozi kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao, inabidi wananchi wajilaumu kwanza wao kwa kushindwa kuwafanya viongozi hao watekeleza wajibu wao.

    Kwa hiyo, kwa kuwachekea tu viongozi wetu bila kuwashinikiza kutekeleza wajibu hatuwasaidii, na wanaposhindwa tunapaswa kujilaumu zaidi sisi kuliko hata tunavyowalaumu wao.

    Hata hivyo kwa jinsi viongozi wa CCM walivyokwishageuka sugu wa malalamiko ni wazi kuwa kununa peke yake haitatosha.

    Kwa hiyo lazima kutumia njia zingine za kushinikiza.

    Moja ya njia ya shinikizo ni kutia saini nyaraka za malalamiko na shinikizo kutaka serikali ifanye jambo fulani; nyaraka kama hizi kwa Kiingereza huitwa petition.

    Kwa mfano, hivi sasa kuna waraka unaopita sehemu mbalimbali hapa nchini ukiomba wananchi waweka saini zao ili kumshinikiza Waziri Msolla ajiuzulu kwa kuwatelekeza vijana wetu waliokwenda kusoma nchini Ukraine.

    Kwa hiyo kusaini waraka huu utakuwa umeshiriki si tu kuonyesha kwamba umekerwa na maamuzi mabaya ya serikali kuhusu kushindwa kutekeleza wajibu wake lakini pia kutaka mabadiliko ya uongozi katika wizara husika.

    Njia nyingine ya kushinikiza ni kushirika katika maandamano. Njia ya maandamano ni ya uhakika zaidi maana huonekana zaidi kupitia vyombo vya habari.

    Hata hivyo nguvu ya maandamano ni umati wa watu. Wakiandamana watu kumi tu au hata ishirini, haitoi picha kwamba jambo husika ni kero kwa watu wengi.

    Kwa hiyo njia moja ya kushiriki katika kuleta mabadiliko ni kushiriki katika maandamano pale yanapoitishwa na wanaharakati mbalimbali, wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani.

    Njia kubwa kabisa katika kushinikiza mabadiliko ni upigaji kura.

    Kwa asili yake, lengo kuu katika siasa ni kupata na kutunza madaraka.

    Kwa hiyo kitu pekee ambacho viongozi wa siasa wataweza kuwasikiliza wananchi ni pale watakapojua kwamba wasipowasikiliza watapoteza kura katika uchaguzi mwingine.

    Ndiyo kusema kuwa adhabu kubwa kwa mwanasiasa asiyetekeleza wajibu wake ni kumfukuza madarakani kwa njia ya kura.

    Ni bahati mbaya kwamba Watanzania hatujaitumia nguvu yetu ya kura vizuri.

    Pamoja na kwamba CCM wametuangusha sana katika maendeleo ya nchi yetu, tumeendelea kuwachagua kila mara uchaguzi unapokuja.

    Kwa maoni yangu, hapo CCM walipofikia wanastahili adhabu kubwa kabisa, ambayo ni ya kuwafukuza katika madaraka kwa njia ya kura.

    Bila kuwafukuza CCM madarakani tutaendelea kukabiliana na kiburi na vituko ya viongozi wake na upatikanaji wa mabadiliko ya kweli utaendelea kuwa ndoto.

    Njia ya mwisho na pengine ya umuhimu zaidi katika kushiriki kuleta mabadiliko ni kuongeza uelewa na umakini katika mambo ya siasa na ya kijamii.

    Mwandishi Max Hastings, akiandika katika kitabu cha “The new protective state-government, intelligence and terrorism”, anasema kwamba viongozi katika jamii yoyote si wengi, na hivyo ni kazi ya wanajamii kuhakikisha kuwa uongozi wa nchi hauangukii mikononi mwa wanaume na wanawake wababaishaji, wahuni na majizi.

    Mwandishi huyu anaendelea kusema kuwa ili kuweza kuwatambua viongozi makini ni lazima jamii iwe ina uelewa na ujuvi wa msingi wa mambo muhimu katika jamii yanayohusu siasa, uchumi, utamaduni, n.k.

    Sasa swali la kujiuliza ni je, baada ya Mwalimu Nyerere, Watanzania tumekuwa makini kiasi gani kuhakikisha kuwa uongozi wa nchi yetu hauangukii mikononi mwa wanaume na wanawake wababaishaji, wahuni na mijizi kama anavyoonya mwandishi Max Hastings?
    Ni maoni yangu kuwa Watanzania hatupo makini linapokuja suala la kuchagua viongozi.

    Wengi wetu wakati wa uchaguzi tumekuwa tukijali mambo madogomadogo yenye masilahi ya muda mfupi kwetu binafsi bila kujali masilahi ya muda mrefu ya taifa letu.

    Kutokuwa kwetu makini katika uchaguzi kumewawezesha watu wababaishaji na wahuni kujipenyeza katika uongozi wa nchi yetu.

    Mfano wa karibu kabisa ni kampeni zinazoendelea katika uchaguzi wa ndani wa CCM.

    Tumesikia jinsi wagombea mbalimbali ambavyo wamekuwa wakilumbana kwa minajili ya ukabila na umakundi katika chama chao.

    Kwa chama makini kipindi cha uchaguzi wa ndani ni kipindi cha kulumbana kiitikadi na kisera ili kuhakikisha kuwa wale wanaochaguliwa katika chama hicho ni wale wanaoelewa vizuri na wapo tayari kuzisimamia na kuziendeleza itikadi na sera za chama chao.

    Badala yake CCM imegeuka kuwa chama cha ujanjaujanja; hakina nafasi kwa watu wanaoamini umakini na usafi katika siasa.

    Matokeo yake watakaochaguliwa ni watu wababaishaji na wahuni wanaoamini ujanjaujanja katika maisha na siasa.

    Na hawa ndio watakaokuja kutuomba kura tuwachague katika uchaguzi wa mwaka 2010.

    Wito wangu ni kuwa tujibidishe kujifunza mambo ya jamii ili tujenge uwezo wa kuchuja pumba na mchele katika mambo ya siasa na uongozi; ili uchaguzi ukija tuweze kuwatambua na kuwachagua viongozi makini ili tuepukane na ubabaishaji, uhuni na ujanjaujanja katika siasa na uongozi wa nchi yetu.

    kitilam@yahoo.com
    +44 7942 027067

    ReplyDelete
  7. Safi sana koloboi@yahoo.com!!

    Rais mstahafu, kama mtu yoyote anayeaminika ahayo haki kukopa. Mimi sioni tatizo lolote kama alikopa, na kisha akarudisha. Au watu wengine mlitaka Mkapa aibe mpate maneno ya kusema!

    Mimi nina mpa hongera mzee Mkapa kwa kutoa mfano mzuri. Mtu unakopa na kurudisha!! Watanzania wengi tunafikia kukopa, lakini hatuwazii njisi ya kurudisha mkopo!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 31, 2007

    Nyie nguchiro acheni ushabiki wa kipumbavu. Chenkapa amekopa akiwa madarakani na wala si baada ya muda wake wa uraisi kuisha. Ndio maana watz hatutaendelea kwa sababu watu wanaongea na kuandika vitu kwa ushabiki.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 31, 2007

    halafu tunashangaa kwamba hatusogei mbele. Bado akili yetu inataka kumwona rais akitoka uongozini awe kwama sisi tu wa kawaida. Vimeisha hivyo. Kama mmeukabali Capitalism acheni kulia lia. Yaaani Rais ashidwe kupata mkopo was hizo chengi wakati wahindi wanavuta mikopo ya billioni. Wake up wabongo

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 31, 2007

    Bravo Kitila! Raisi wa Daruso wa zamani! ninapenda watu wenye maneno mengi kama wewe ila kuingiza mguu wako kazi kufanya kazi, kugoma kazi, mobiliza wa maneno, hiyo ni tabia nyingine ya watanzania! siasa ila vitendo kasheshe, hivyo ndivyo walivyo viongozi wetu. Inasemekana mtu asidai hawezi kuiba hata siku moja hali hajafikia level na kupewa nafasi ya kuiba ninamaana asiye mwizi ni yule alipewa nafasi ya kuiba na still hakuiba! wewe bado ni mchanga katika siasa, ukipewa nafasi ya kuiba utaiba tena zaidi yao.tena ninaona uchanga wako wa siasa umeanza vinaya maana umeanza kwa maneno kama walivyo viongozi wetu!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 01, 2007

    Michuzi acha ukereketwa wako wa CCM wa kutupa maoni ya watu, usiogope kufukuzwa kazi Daily News, Kwa nini maoni ya watu unayatupa wakati hayakutakana mtu acha hizo watu tunakuja kwenye blog kwa sababu inaburudisha na kuelimisha sasa wewe ukiona maoni hayaendani na itikadi yako unayatupa, deligate kwa mtu basi blog kama unaogopa wakubwa.

    Mara nyingi tu nimemezea leo nimeona nikwambie ukweli hata kama hutaitoa nakulenga wewe binafsi si wadau.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 01, 2007

    Naona ni vizuri tusaidieni kuna Anoy mmoja (31 May)anasema tatizo la Mkapa ni kukopa akiwa bado Raisi.Angekopa akishastaafu! Makubwa!

    Namhurumia huyu ndugu nadhani hajawahi kwenda benki kutafuta mkopo au huenda huyu ndugu anaishi dunia ya peke yake! Dunia ya kijiweni!

    Ukienda benki ni rahisi kukopa ukiwa mfanyakazi kuliko ukiwa umestaafu.Mapato ya mtu aliye kazini ya kila mwezi ni makubwa kuliko pensioni za kila mwezi ukistaafu.Mikopo ya watu walioko kazini iko kibao kwenye mabenki.Na watu walioko makazini wanapewa kipau mbele cha kukopeshwa kuliko wastaafu! Hata mitaani si unajua ni rahisi kumkopa jirani ukiwa na kazi kuliko ukiwa umestaafu.

    Ukiwa umestafu ukienda kumkopa mtu hata uape viapo vyote kuwa utamrudishia ukimkopa jirani si rahisi jirani akakupa.Haamini uhakika,uwezo na mtiririko wa mapato yako.Sasa sembuse mabenki?

    Kama wewe unafanya kazi kakope sasa haraka ukiwa kazini. Usisubiri ustaafu.Ukisubiri hadi ustaafu utakanyaga mguu wa nenda rudi benki hadi ndala zichakae na mkopo usipate.

    Mkapa Msomi yule na Kichwa chake kinafanya kazi sawasawa ndiyo maana hakuona asubiri astaafu ndio akope kama ushauri wa kijiweni wa huyo anoy!

    Nakushauri wewe kama unafanya kazi wahi haraka tafadhali.Nenda benki yoyote iliyo karibu nawe waeleze wewe kama wewe ni mfanyakazi kuwa bado uko kazini unahitaji mkopo. Waambie wakueleze fursa za mikopo iliyopo.

    Changamka.Acha kuzubaa na kushinda kijiweni unapiga kelele za chenkapa,chenkapa!


    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 01, 2007

    ni kweli anony hapo juu huyu jamaa michuzi kuna comments tunazituma anazibania ...wakati mwingine tunamtumtumia mail za maana azipost but hazipost anazibania ..au kwa kuwa sisi hatuishi ulaya maana naona watu wa ulaya na mapedejee wa nchini ndo anawapostia ila sisi huku mbagala charambe anatutusa...poa lakini

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 01, 2007

    MKAPA HAJAVUNJA SHERIA YOYOTE.NAYE ANA HAKI YA KUKOPA KAMA MTEJA MWINGINE YOYOTE WA BENKI.HIKI NI KIPINDI CHA KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM KAMATI ZA FITINA ZIPO KAZINI. INGAWA HAGOMBEI MZEE BM BADO ANA WAFUASI KIBAO CCM USHAHIDI NI JINSI ALIVYOSHANGILIWA KWA NGUVU ALIPOINGIA UWANJA WA TAIFA SIKU YA MUUNGANO.MAJUNGU YOTE HAYO YANAPIKWA NA KAMATI ZA FITINA ILI WAFUASI WAKE WACHEMSHE. MAMBO YA KAMPENI HAYO WAACHIENI WENYEWE WAMALIZANE.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 01, 2007

    sasa hapo JK anampeleka wapi BM? Na Haka kakijana cha PCB kanafanya mazoezi mbere ya wazee? Akana adabu kabisa. Michuzi/Kipanya embu mwambieni aache kufanya mazoezi wakati wazee wanaongea. Eboo

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 02, 2007

    MIMI HAPO NAONA NI MIKATABA YA MADINI TU!! ASILIMIA TATU INAINGIA KWENYE KUJENGA NCHI, ASILIMIA THALATHINI MFUKONI, ZILIZOBAKI KWA INVESTORS, ITS REALLY A DEAL... WE DONT HAVE TECHNOLOGY? WHAT IS THE FUTURE OF TANZANIA?? NI MASHIMO YANAYOWACHWA NA INVESTORS KATIKA MINING???? MWENYEZI MUNGU AWAPE AKILI WANASIASA WETU AND WHAT SO CALLED VIONGOZI WETU, KUWA KATIKA MAPATO WANAYOPATA NAO WAINVEST KWENYE INFRA STRUCTURE AND TECHNOLOGY!!!! NATUSISAHAU KUWA TANZANIA ASILIMIA 80 TUNATEGEMEA KILIMO

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 02, 2007

    Sir Issa.. vipi kaka...hii picha ya .."..KP.."..INAVUUTIA...HUYU RAISI MSTAAFU ALIFANYA KAZI KWA BIDII SANA TUNAMSHUKURU...NA MWENZIE (..JK...RAISI WA MAMBO YA NCHI ZA NJE WA TANZANIA.., ZIARA MUHIMU BWANA...NI BURUDANI TUPU..KAAZI KWELIKWELI)..HUYU MHESHIMIWA MSTAAFU DOCTOR KAMSHAURI ASHUKE UZITO KWA FAIDA YAKE, MPAKA LEO BADO..WHAT DO U THINK...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...