jaji mkuu mh. barnabas samatta akwia ofisini mwake. mh. samatta anatarajiwa kustaafu mwezi ujao baada ya kuitumikia idara ya mahakama kwa ustadi na uaminifu kwa miaka yote hii, akiwa mrithi wa hayati jaji mkuu francis nyalali. hivi sasa mh. samatta yuko katika ziara ya kuaga mikoa mbalimbali....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2007

    Mjomba haraka za nini tena! uwe unasoma mara mbili habari unazoweka angalia ulivyochemsha hapa eti mh Nyalali yuko ktk ziara ya kuaga mikoa mbalimbali! ina maana amefufuka?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2007

    HAMNA CHOMBO KILICHO OZA KAMA MAHAKAMA ZA TANZANIA. SASA SIJUI MCHANGO WAKE ULIKUWA UPI KATIKA KUIFANYA MAHAKAMA SEHEMU YA HAKI NA SIO SEHEMU YA RUSHWA NA KUUMIZA WANYONGE NA WASIOKUWA NA HATIA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2007

    Jamaa kambania kumuongezea muda Samatta kwasababu ni mtu ambaye haendeshwi na mtu na anapenda executive iwe inaitii mahakama wakati jamaa anataka mahakama ndio iwe inaitii executive.

    Habari zilizopo ni kuwa jaji Agustino Ramadhani ndio atakuwa chief justice mpya.

    Michuzi usibane kaka!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2007

    anony wa 11:43 ,31st of may,unaboa na ni KILAZA mkubwa saaana. Hivi huelewi nini hapo kwenye hii habari au kama vipi Bro Michuzi mwandikie tena kwa HERUFI KUBWA labda silabi zinamchanganya huyu mheshimiwa msomaji

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 31, 2007

    ANONY WA 11:43, KWA KIFUPI NI KUWA MWALIMU WAKO WA PRIMARY ALIPATA SANA SHIDA...NAMHURUMIA. KAZI IPO ANY WAY KUNA ELIMU YA WATU WAZIMA KUPITIA TAASISI YENYE JINA HILO ,JIUNGE BASI...kaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 31, 2007

    wewe anon ndiye umechemsha na wala si kaka Michu,kaka Michu kasema kuwa Samata alichukua nafasi kutoka kwa jaji Nyalali na wala hajaandika kw akukosea kama Samata ni Nyalali
    be so careful ukindika prior to paste your comments,otherwise uache kuandika tutajua tu kama upo!
    kazi nzuri kaka Michu,lete vitu zaidi

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 31, 2007

    Anon, hapo juu, wengine hatuoni kosa la Michuzi, kama wewe.

    Michuzi kaandika, "jaji mkuu mh. barnabas samatta...akiwa mrithi wa hayati jaji mkuu francis nyalali. hivi sasa mh. samatta yuko katika ziara ya kuaga mikoa mbalimbali...."

    Aliyeko ziarani ni Jaji Samatta! Angalia: Kuna alama ya kituo (.) kati ya nyalali na hivi. Neno "hivi" linaanza sentenso mpya, ingawa Michuzi hakutumia herufi kubwa!



    Wewe umechemsha sana!

    ReplyDelete
  8. hee na mimi nilisnagaa Nyalali amefufuka na kuja kuaga tena!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 31, 2007

    We anony wa may31 11:43:00Am,huna hata aibu,hebu soma tena habari ya michuzi wala hajakosea. Tatizo ni wewe ambaye huwezi kuona au hujui matumizi ya nukta(full stop). Mwombe radhi michuzi please kwa ujinga wako

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 31, 2007

    sasa wewe na michuzi nani ambaye haoni vizuri?michuzi ameandika na kituo kaweka sasa wewe na macho yako yaliyokaa kushoto ukajiona ndio unaona kumzidimwandishi?nakushauri nenda kapime hiyo mijicho yako iliyokuwa kushoto

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 31, 2007

    Jamani wana blog wote pole pole basi washikaji. Mtoa maona wa kwanza amesema ukweli hata mimi nilivyoingia kwenye blog hii nilikuwa Michuzi ameshemsha badala ya kuandika Mh. Samatta anazunguka mikoani kuaga aliandika Mh. Nyalali. Nafikiri ameligundua kosa lake akafanya masahihisho kwa hiyo sidhani kama mtu na akili yake anaweza kusema kitu ambacho hana uhakika nacho na ukiona kitu kama hicho ni lazima ujiulize kwa nini amefanya hivyo? Yeye Michuzi angeomba radhi kwa kukosea halafu ndio akasahihisha sasa alivyofanya hivyo na huyo mtoa maoni wa kwanza ofcourse itawachanganya watu. Ni HAYO TU.

    Mimi

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 31, 2007

    Arooo! Nyie wote mnaobishana kuhusu spelling na full stop nyamasa haraka.Pumbafu.

    Tunataka kuendelea kutoa hoja za maana. Ok!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 31, 2007

    Miaka hii yote....Miaka mingapi? Michuzi kama una habari tupe fact zote au acha kueka hiyo sentensi ....miaka hii yote...???!!!! Mingapi...???

    lakini asante kwa yote unayofanya humu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 31, 2007

    Ninyi wote hapo juu ndio mmechemsha na mnamuonea bure anony. wa kwanza.
    Ni kweli kuwa ilipotoka mwanzoni kabisa hii picha, Michuzi alikuwa ameandika Mhe. Nyalali hivi sasa yuko ziara ya mikoani... tuliokuwa wa kwanza kabisa kuisoma tuliona hivyo, hata na mimi niliandika kumsahihisha Michuzi lakini hakuitoa.
    Msimuonee bure huyo wa kwanza, ni kweli Michuzi kama binaadamu aliteleza tu na hakuwa na makusudi.
    Michuzi mwenyewe kama utasoma haya maoni yangu, Kiuungwana mi naomba ukubali na kuwaeleza hawa jamaa waliokuja baadae kwamba mwanzoni kabisa ulikosea.
    Huo ni UUNGWANA na UTAHESHIMIKA kwa hilo brother Michuzi.
    Come on!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 31, 2007

    Jamani michuzi alikosea, kafanya kubadili hiyo sentensi mimi niliiona pia, kwahiyo msimseme huyo mtu wa mwanzo........Michuzi ona mtu anavyovamiwa.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 31, 2007

    The President’s nominee for Chief Justice, Justice Georgina Theodora Wood has said she is going to build a culture of integrity within the judiciary as a first step to fight corruption.

    Speaking before the Parliamentary Appointments Committee, which is ongoing at the Parliament House, Justice Wood conceded that fighting corruption is an uphill task but she would make it a priority.

    She said: “It is difficult to erase perception of corruption in the judiciary…I will begin by building a culture of integrity. That is bothering and you cannot build it overnight.”

    Justice Wood said motivation and better remuneration for staff will be given serious attention. However, she said no institution could thrive especially when it comes to fighting corruption when the leadership is corrupt.

    “I will set the example for others to follow. Promotion will be merit-based and a key ingredient will be integrity and competence. Salary structures will have to be improved so people will not be tempted,” she promised.

    Justice Wood called on the public to refrain from bribing judges since that serves as a breeding ground to taint the image of the Service.

    “Leave our judges alone to work. If you have a case go to the court and get a lawyer…You can’t have 100 per cent perfect people. There could be an element of truth that corruption prevails in the judicial,” she said.

    She promised that her administration will demand accountability from the support staff as well as monitor their activities.

    President Kufuor, acting in consultation with the Council of State, nominated Mrs Wood on May 4, following the demise of George Kingsley Acquah on March 25.

    Justice Francois Yaonansu Kpegah has been acting CJ, in line with Article 144(6) of the 1992 Constitution, which states that in the event of the Chief Justice's office being declared vacant, the next in order of seniority takes charge until a substantive CJ is appointed.

    Vetting is ongoing and myjoyonline will update readers soon.


    BIOGRAPHY

    Born on June 8, 1947 Mrs Justice Wood attended Bishop’s Girls and Methodist Schools.

    She had her LLB (Hons) from the University of Ghana, Legon in 1970 after completing Wesley Girls High School, Cape Coast in 1966. She took a six-month Post-Graduate Officers Training Course at the Ghana Police College.

    She joined the Judicial Service as a District Magistrate Grade II and was later promoted to Grade I. She was promoted to the Court of Appeal as a presiding judge in 1991.

    Mrs Justice Wood last year chaired the Georgina Wood Committee that conducted an enquiry into the disappearance of 77 packets of cocaine from the MV Benjamin vessel on April 26, 2006, as well as the 588kg cocaine seized from some Venezuelans at Mempeasem, East Legon.

    Mrs Justice Wood was first nominated to the Supreme Court in 2003, at the time of the Fast Track Review Case, alongside the late Justice Afreh – a nomination she initially turned down. She is the Chairperson of the Alternative Dispute Resolution Mechanism.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 31, 2007

    http://www.myjoyonline.com/archives/news/200705/5214.asp

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 31, 2007

    ofisi nzuri lakini mbona kompyuta hamna, wanatunza vipi mafaili? au kila kitu kwa kalamu na karatasi

    ReplyDelete
  19. WADAU NAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOPO JUU YA MAJINA YA MH. SAMATTA NA HAYATI JAJI MKUU NYALALI. UKWELI NI KWAMBA AWALI NILIKOSEA NA KUWEKA MH. NYALALI NDIYE ALIE ZIARANI MIKOANI KUAGA. BAADA YA KUGUNDUA KOSA HILO NIKAREKEBISHA LAKINI KWA BAHATI MBAYA AMA NZURI KUNA WADAU WALIIDAKA SEHEMU HIYO KABLA YA MAREKEBISHO.

    NAOMBA RADHI KWA MAKOSA YA AWALI NA PIA KUNRADHI KWA KUTOOMBA RADHI NA KUFANYA MASAHIHISHO KAVU-KAVU.

    SAMAHANI WOTE KWA USUMBUFU AMA MAUMIVI MLIYOPATA

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 31, 2007

    Computer iko nyumbani kwake. Okay ...

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 31, 2007

    Michuzi furahia sana kwa vile wasomaji wako wanafuatilia sana hii blog na wako makini sana kwenye kila angle. Hawaangalii mgongomgongo tu kwa makini na kuona wenye kutoa jasho kwenye bukta zao tu bali hata mambo mengine ya siasa na serikali wapo makini sana tu.

    Hiyo ni moja ya test na ujue kuwa ukukiweka news tu hata sekunde tano hazijapita ni wangapi wameshasoma hiyo habari. Kuna wengine wanalala usiku wanaota blog yako, na wale wasiona compuer makazini kwao wanahesabu masaa ili waende nyumbani kusoma Michuzi blog. You huge now my brother. Hayo ndio mafanikio.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 31, 2007

    Hapo umeonesha uungwana mtu mzima, ila najua ulikuwa unaangalia na kucheka tu jinsi wadau wanvyoraruana. Ila umeamini kuwa wadau wapo nawe maana wanakutetea kwa nguvu zao zote, Mkuu una nguvu ya uma sasa bado kugombea ubunge kwa jimbo la BLOG.

    Aisee mii hiyo ofisi imenifurahisha hicho kijimeza cha muheshimiwa maana inaoneka ni mtoa mada mzuri sana ofisini kwake, kameza kama ka 'Lecture room' vile

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 31, 2007

    Ah kaka zangu na dada zangu ,mbona hivyo jamani.tusiwe watu wakuanza kupaka tu bila mpango jamani!!! Tuliowengi tuliona makosa ya michuzi ,ila huyu bro naye sababu comments kibao anaziminyia wala hatukujisumbua kuandika,angalia muda huyo anony wa kwanza alivyotuma comment yale lol halafu muelewe kwamba alisoma mapema zaidi yenu.
    Kwa Michuzi ukitoa usitoe hii comment umechemsha,ulipublish vp hii cooment bila kuwaeleza wanamtandao wako ulikosea.Halafu mchujo wako wa comments siuelewi ,kuna utumbo mwingine unauweka humu mpaka najiuliza sijui wanakuonga ,halafu mwingine ataleta comments za kweli na zinazoigusa jamaa ya watz unaziminya ,mi sikuelewi.Sawa tutakutana Bongo patakuwahapatoshi hapa.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 31, 2007

    Jamani Michuzi sio mtu makini, kazi zake nyingi za kiuandhishi wa habari zinakuwa za kulipualipua. Ila kwenye picha huwa yupo makini sana. Sasa nyie msibishe michuzi aliweka kama huyo Anonymous juu alivyosema. Baada ya kungundua makosa yake amerekebisha bila kuujulisha umma. Hili ni kosa kiuandishi wa habari. Michuzi kuwa makini ndugu yangu

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 01, 2007

    Jaji Bomani
    Jaji Nyalali
    Jaji Samatta

    Attornesy General
    Samata
    Sekule
    Chenge

    Mboa Wasukuma tu, jamani?

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 01, 2007

    wewe unasema wasukuma tu? Unaangaliaga court shows za USA mbona ni waspanish wengi tu ndio majudge? wasio waspanish wanahesabika. Kila kabila lina vichwa vyao.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 01, 2007

    WHO CARES KAMA WOTE NI WASUKUMA?PELEKA UPUUZI WAKO KENYA WEWE UNAYEJIITA MSUKUMA SAFI,SIKUTEGEMEA MTANZANIA ANAWEZA KUANDIKA UPUMBAVU KAMA HUU!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 01, 2007

    Michuzi nakupongeza ndugu yangu kwa kuomba radhi baada ya kukushauru ufanye hivyo. Umeonyesha UUNGWANA wa hali ya juu na umejiongezea heshima.
    Hivi ndivyo inavyotakiwa katika CIVILISED Societies. Hongera Sana! Keep it up!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 01, 2007

    Wewe anoy wa hapo juu Mhe. Jaji Samatta sio Msukuma ni Mmanda wa ziwani ziwa nyasa.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 01, 2007

    Wanablog mnisaidie, ile rangi ya kiti ina maana yoyote au Mh. Samatta ameamua tu kuwa na kiti chekundu. I heard the so called colour code sasa sijui kama hapo pia ipo au la!!!!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 01, 2007

    Wewe anony unayeandika kuhusu usukuma, Jaji Samata sio Msukuma! usibabaishwe na hilo jina lake.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 01, 2007

    We anony nayepingana na huyo msukuma safi, hujatulia. Hebu tuache tuchambue mambo, mi pia nashangaa mbona wote ni wakristo tu? Safari hii nasikia anakuja mwislam!

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 01, 2007

    Wewe unauliza mbona wote ni wakristo ???? hah haha haha waliobakia wako kule wananamchagua kiongozi wa Yanga

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 01, 2007

    Jamani hivi kati ya IGP na JUDGE nani anacheo kikubwa?????

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 05, 2007

    Kuna wakati tulipokuwa mlimani chuoni, kulitokea soo, Nyalali ali-press order kwa Mahita ya 24hrs jamaa akamatwe. Kwahilo nahisi Judge anacheo kuliko IGP

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...