hiyo ndio meza kuu ilosimamia uchaguzi mkuu wa yanga leo ukumbi wa dayamondi jubilei na matokeo yametoka muda si mrefu ulopita na washindi ni kama ifuatavyo:


1. mwenyekiti - imani madega
2. makamu mwenyekiti - rashidi ngozoma matunda


3. katibu mkuu - lucas kisasa


4. katibu mkuu msaidizi - ahmed mamba


5. mhazini - abeid mohamed abeid


6. mhazini msaidizi - godfrey mwenje


7. katibu mipango - patrick fataa


8. katibu mwenezi - francis lucas
waliogombea walikuwa 51 na wapiga kura walikuwa 1025 kati ya wanachama zaidi ya elfu 5 ambao ni pamoja na wa makundi ya yanga asili, kampuni, bomba na academia.
vigogo walioshindwa ni pamoja na baraka igangula na kibo merinyo, mohamed bindha na ismaili idrisa katika nafasi ya uenyekiti.
vigogo wengine walioshindwa ni pamoja na saidi motisha ambao walianguka katika nafasi ya makamu mwenyekiti, shabani dilunga na patrick fataa aliyejitoa.
vigogo walioanguka nafasi ya katibu mkuu ni constantine maligo na emmanuel mpangala.
mchezaji wa zamani wa yanga bakari malima 'jembe ulaya' alianguka katika nafasi ya katibu mwenezi.
katika nafasi ya uhazini baadhi ya vigogo walioanguka ni castro mketto, jeremiah michael, paschal kiyomba na evarist mwang'onda aliyejitoa.
vioja: pale rais aliyemaliza muda wake francis kifukwe alipogoma kwenda kusimamia uhesabuji kura za mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti saidi motisha kwa kile alichodai 'mgombea hana kura za kusimamia', hivyo mgombea akaomba meza kuu imsimamie. pia wanachama waliinuka kucheza 'mugongomugongo' ya twanga pepeta wakati kura zinahesabiwa...
umbea: wanachama waliokataliwa kuingia ukumbini kupiga kura walisikika wakiapa kuwa wataenda mahakamani kupinga uchaguzi baada ya kunyimwa haki yao; madai ni kwamba kwa vile ilikuwa ni siku ya kazi pamoja na kuweko na mvua kubwa na foleni ya magari wengi wao walidai kuwa walichelewa kufika kwa sababu hizo...


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2007

    Haya YANGA....tusubiri wiki moja halafu migogoro ianze kama kawa.

    Uongozi bila Matunda Yanga haupandi!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2007

    Wakome hao waliochelewa . Wabongo kwa kuchelewa tu hatujambo. Kila kitu tuna take our time. Mtu ukiambiwa saa 5.00 anafika saa 7.00. Way to go..wafundisheni watu hivyo watajua kuwa sharp sharp.

    be responsible kama mvua ilinyesha ilinyesha jijini na waliowahi wao mvua haikuwapo? na kama uliona huo mda haufai kwa vile ya majukumu mengine basi wangesema kabla utafutwe mweingine. Tumezidi excuses

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2007

    Michuzi usije ukatusahau wengine sio wapenzi wa soccer. Lini yanga na taifa star mambo yao yataisha au tuchanyie basi chachandu na kchumbari pamoja.

    We love you don't get so mad with our demands. If you are busy it is alright too. Don't mind me just talking to myself ha ha ha ha ha.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2007

    Michuzi tuwekee picha ya Ridhiwani Kikwete alivyoenda kuchukua fomu ya kuomba kuwa mjumbe wa NEC. Atamenyana na Mheshimiwa Sumaye jimbo la DAR. Kazi kweli kweli, naona mtandao unazidi kuimarishwa. Ila wasio wanamtandao nao hakubali. Mangula naye bado analia na mtandao, ameamua kuwa anagombea uwenyekiti wa CCM mkoa Iringa. Kasheshe mwaka huu!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 31, 2007

    Michuzi mbona unatuwekea UCHAFU kwenye blog hii.yanga yanga si tulishahamia premiership toka kizota astaafu

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 31, 2007

    Nawapongeza viongozi wapya na wanachama wote kwa uchaguzi. Kwa wale wapenzi wa Yanga msikose kutembelea blogu yetu ya:


    www.yangatz.blogspot.com

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 31, 2007

    Kuchagua viongozi wapya siyo tija. Point ni kwamba club ina katiba mpya ambayo inaendana na mwongozo mpya wa soka Tanzania kulingana na TFF.

    GAZ

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2007

    Hamna loloteeee!Huo uchaguzi ni kupoteza muda tuu.Migogoro hapo jangwani kamwe haitaisha, subiri siku chache zijazo mtaona.Tatizo hizi timu zetu (Yanga na Simba)zimejaa vizee na wanachama mambumbumbu, fitina na majungu.Hawajui namna timu zinavyoendeshwa.Wanacho-mind ni gate collection na vipesa toka wahindi.Soka la TZ linauliwa na timu hizi mbili.Kwa mtazamo wa haraka haraka kwenye hayo matokeo inaonyesha Yanga Asili wamerudi ulingoni.Basi tusubiri tuone Kampuni na Academia watafanya nini.Taabu kweli kweli.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 01, 2007

    Kwa wale msiofahamu huu uchaguzi ni danganya toto. katiba mpya ya club ya Yanga inasema kampuni ya Yanga ndio ita manage timu na itafanya hivyo baada ya kukodi timu toka club na kuilipa club royalty. in effect hawa viongozi wapya in due course team watai sign off kwa viongozi wa kampuni ambao ni kifukwe,sauko na lwimbo. baada ya hapo nini kitafuata? viongozi wa club kazi yao itakuwa ni kucheza dhumna,karata etc .of course likija game dhidi ya Simba mzee Matunda atashikishwa kitu kidogo kwa ajili ya 'ufundi'. nimalizie kwa kusema huu uchaguzi was just a farce perpetrated na mtu mmoja anayejiita mfadhili wa Yanga kwa sababu anazozijua yeye,surely iko siku ataumbuka.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 02, 2007

    juzi nimesoma kwenye gazeti la 'alasiri' kwamba wapambe wa huyu mfadhili ndani ya vyoo vya kwenye ukumbi wa uchaguzi walikuwa wanahonga hela wapiga kura kama hawana akili nzuri,kisa?wachague watu ambao 'mfadhili'amewa annoint. tutafiki kweli? na je haya yakitendeka Hosea na trupu lako la PCB mlikuwa wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...