KAKA MICHUZI LEO NILIKUA MSAFIRI WA NDEGE YA AIR TANZANIA TC 100 IENDAYO DAR/MWZ.
NIMEFEDHEHESHWA SANA NA DADA ALIYE KUWA KWENYE UKAGUZI WA USALAMA WA MWISHO ( LAST SECURITY CHECK POINT ) UNAPOINGIA DEPARTURE LOUNGE ( DOMESTIC) KWA KUTUMIA LUGHA ZA FEDHULI SANA KWA WATEJA BAADA YA KUWAPEKUA.
MIMI ALINIKUTA NIMEBEBA VIMIMINIKA (LIQUID) AMBAZO NI UTURI (PERFUME) NA LOTION ANAZODAI ZIMEZIDI UJAZO WA ML 100 KILA MOJA KAMA TARATIBU ZA USAFIRI WA ANGA ZINAVYO SEMA,SINA TATIZO NA HILO.
CHA KUSIKITISHA NI KWAMBA YULE DADA WA USALAMA ALIPONIAMBIA KWA FEDHULI KWA KUNIFOKEA KUWA SIRUHUSIWI KUSAFIRI NAZO,AU KAMA UNAZIMIND JIPULIZIE HIYO PARFUME YAKO MPAKA IISHE NA LOTION JIPAKE MPAKA UIMALIZE KABLA HUJAPANDA NDEGE.
JE MHESHIMIWA TEMU WEWE UNAWEZA JIPULIZIA PERFUME ILIYOZIDI 100ML NDANI YA DAKIKA 5 UKAIMALIZA AU NI KEJELI NA KUDHALILISHANA?
AU BWANA TEMU NIKULETEE LOTION ILIOZIDI 100ML UJIPAKE NDANI YA DAKIKA 5 UIMALIZE?
TEMU ONDOA UWOZO AIRPORT,UNAWALEA SANA!!!
UTANISAMEHE KAMA MUHUSIKA WA KUMFUNDA HUYU DADA SI WAKO NI WA DADA MAGRETH MUNYAGI.
NAOMBA RADHI KWA LUGHA KALI NILIYOTUMIA.
SIKU NJEMA
STAKE HOLDER

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. Wote wawili munafanana. kwani kama unajuwa sheria ni kutosafiri na vimiminika zaidi ya huo ujazo wewe uliendanazo kwamisingi ipi? watu wapo busy wamechoka kusikiliza wapumbavu kama wewe.
    Mukisafiri Nchi za nje munakuwa mumejiandaa home lakini ikiwa bongo munaota kufisadi.

    Pole kwa uzembe wako, jipulizie tu.

    G7
    UK

    ReplyDelete
  2. G7
    UK
    WEWE SI MUUNGWANA KWA KUTUKANA,LAKINI SIKULAUMU WALA SISHANGAI KUTOKANA HATA KISWAHILI HUKIJUI KUTAMKA/KUANDIKA
    JIFUNZE LUGHA KWANZA,NDIO UTUKANE WENZIO

    POLE SANA

    ReplyDelete
  3. Na wewe hapo juu unajuaje kama mlalamikaji alishawahi kusafiri kwa ndege? Inawezekana ilikuwa ni mra yake ya kwanza kusafiri na ndege na alikuwa hajui sheria. Hata hivyo huyo mfanyakazi hapaswi kutumia lugha mbaya kwa wateja alitakiwa kumweleza vizuri ni sheria gani ambazo zinatakiwa tifuatiliwe kabla ya kuingia kwenye ndege. Lugha kama hii hatakiwi kwenye sehemu za kazi.

    ReplyDelete
  4. Huyu Bwana Kaeleza upande mmoja wa Shilingi! Na kwa sababu safari ilikuwa ndani ya Tanzania alidhania ataweza kufanikisha kumshawishi huyo "security Personel" Kibongo bongo! Na kwa watu tunaoona mbali mwanadada huyo hakutumia lugha mbaya zaidi ya kumweleza aziweke kwenye kapu la vitu vya kutupwa! Huyo mlalamikaji inaonyesha dhahiri hakuridhishwa na hatua hiyo; ndipo majibu ya KWAMBA KAMA UNAZIMIND JIPULIZIE ZIISHE au JIPAKE LOTION YOTE (ZOTE)yakatokea!!! Watu wakiwa nje mbona wanavaa nguo hadi tano badala ya kutupa.....Mwanadada alifuata sheria zote sio kusingizia kwa upuuzi wa mtu!!!!!!!! Watu wapo kazi kama wewe unavyokuwa kwenye shughuli yako!!!!!!! Heshima kitu cha bure....Tujaribu kufuata taratibu husika!!

    ReplyDelete
  5. G7 huo siouungwana wakumjibu mtu si vizuri anaomba ushauri wewe unarudi kule kule. ndgu yangu pole siku nyengine kabla hujasafiri chunguza. Pia kwa wafanyakazi wanao pekuwa pia si vizuri mfahamisha mtu kwa adabu si majibu kama hayo vitu kama hivi tunakuomba issa michuzi kawaambie wananchi wetu wawache jeuri Jamani tutumie Lugha vizuri plz. G7 watu watakuja kukuzarau sasa mungu akusamehe kwa matamko uliyotumia.

    ReplyDelete
  6. Kwa watu walowahi kusoma psychology, hata ile ya Watu wa education pale UDSM inatosha kukuwezesha kung'amuwa kwamba huyu aloleta haya malalamiko ni mkorofi, na huena anaona kupanda ndege ni boge la ishu hivyo anapaswa aheshimiwe hata akikiuka kanuni za usafiri! Haiingii akilini Dada wawatu aanze tu kukwambia kama unamind perfume yako jipulizie mpaka iishe!!! Lazima kulikuwa na majibizano, yaani huyu mlalamikaji alikuwa analazimisha aachiwe asafiri na vimiminika vilivyozidi ujazo, nna hakika nahilo ingawa sikuwepo (Kwa kutumia kanuni ya kimantic)!

    ReplyDelete
  7. Sio kila sheria wanayoianzisha Marikani lazima na sisi Tanzania tuifuate. Je, wakisema kila restrooms lazima ziwe na water purifiers je watanzania mtaiweza hiyo kwenye vyoo vya mashimo?

    ReplyDelete
  8. huyo mdada airport hakupaswa kumjibu mteja hivyo!! angekuwa ni raisi kapita na vimiminiko or whatever angemwambia ajipake hadi viishe, angetumia lugha nzuri tuu, some jobs are stressfull but u have to be cool and patient!! anlidhalilisha shirika la ndege, id rather nipande ndege nyengine kuliko kukutana na mambo kama hayo.

    ReplyDelete
  9. G7 inaonesha jinsi gani unadanganya kwamba uko UK maana hapa watu they are very Diplomatic hata kama anakutukana hata kama ni police very very diplomatic sasa wewe badala ya kumpa ushauri au kutafuta solution naleta kiswahili chako cha burudi na bukoba wa wapi wewe unakaa ngara nini? umenichefua as if ujawahi kanyaga darasa!

    ReplyDelete
  10. Daaaa G7 NILIJUA KICHWANI MWAKO UNAZO KUMBE 0 HAMNA KITU SIKUTEGEMEA WEWE UNAWEZA KUMJIBU HUYU JAMAA MAJIBU KAMA HAYO SIO UUNGWANA KABISA YAANI TENA JIRUDI MKUU MAANA HUNA TABIA HIYO MIMI MWENYEWE NIMESHANGAA SANA NILIKUWA NAKUONA MTU MWENYE HESHIMA KUMBE WEWE NDIO WALE WALE WASIO JUA NINI WANAFANYA ALAA...MDAU POLE SANA KWA YOTE YALIYOKUKUTA

    ReplyDelete
  11. Pole.Niseme hivi yote yanawezekana labda na mlalamikaji alitoa kauli ambayo ilimgadhabisha muhudumu na kujibu kwa SCUD hilo.

    Lakini sasa naweza kusema kuwa wafanyakazi wa viwanja vyetu vya Bongo noma sana.Mimi imenitokea mara kibao.

    Mwezi may nilighafirishwa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro.Nilikuwa natua pale.Ndege niliyopanda mweusi nilikuwa alone,katika kutoka nje karibia watu kama 25 hivi wazungu hawakukaguliwa walikenuliwa meno na kukaribishwa Bongo ile kufika mimi nikawekwa pembeni.

    Mara ikaanza kukaguliwa Passport wakaitana na wengine kuitambua passport kama ni fake au la,baadae mkuu wao nafikiri akawaita wengine kama wa4 hivi wakaja nikaamuliwa nifungue sanduku,Nikakataa wakaniambia ni sheria.Nikasema siwezi kufungua sanduku mpaka na wale wazungu waje wakaguliwe kama mimi na nikaambia mbona mliniuliza vassination na wazungu wale hamkuwauliza.

    Wakakosa jibu.Walichofanya waliwaita hata waliokuwa wametoka nje wakaguliwa kwanza wao na mimi ndio nikakaguliwa.Mwisho boss wao akaniambia,"dogo una dharau..." nikamwambia Baab Kubwa.

    Mwingine alianza kusema nina Visa fake,nikamwambia sio juu yangu apige simu ubalozi husika aulize.Yaani vichekesho.Kwa kauli dhalili wafanyakazi wa viwanja vya ndege wanazo hasa kwa wabongo

    ReplyDelete
  12. tatizo la wadau mumeshindwa kuichambua hoja ya mtoa hoja vizuri sana. Sio muda mrefu kuna mtu kama huyu alikuja kulalamika kwamba aliombwa vichenji na watumishi wa pale airport.
    Pia jamaa amekiri kwamba alikuwa anafahamu ya kutosafiri na vimiminika zaidi ya ujazo uliosemwa. so case ipo hapa why aende na ujazo usiotakiwa?? na pia wasemaji wa hapo juu wamejaribu kuona jinsi gani mtoa hoja alivyovyoonesha weekness kwamba inawezekana kamsababishia mtumishi kureact that way..
    Mbona watu kibao wanapita hapo including wengi munaosoma blog hii hamjatukanwa?? haiitaji Degree kuelewa huyu mtoa hoja ndiye mwenye kosa la kwanza..

    G7
    UK

    ReplyDelete
  13. Wajameni,

    Hii sio airline issue ni issue ya usalama wa Anga... na kampuni husika ni mamlaka ya TCAA (Tanzania Civil Aviation Authority)

    Unatakiwa kuiomba Radhi ATC.

    ReplyDelete
  14. wewe ulosoma hiyo psychology "hata ile ya watu wa education pale UDSM" umetumia principles gani kung'amua hulka na silka ya huyo ndg mteja (msafiri ) kuwa ni mkorofi???Hadi hapo mlipofikia sasa hivi mimi naona kuwa wengi wa wachangiaji wa mada hii aidha ni wafanyakazi wa Airport (manajiosha)au ni malimbukeni wa usafiri wa anga.Hayo si majibu ya kumtolea mteja.

    Kwani sheria za usafiri wa ndege zinasema kuwa mtu akizidisha mzigo ni kujipulizia hiyo iliyobaki kama ni pafumu au kuvaa nguo tanotano kama ni nguo??Acheni hizo malimbukeni ninyi.Huyo mfanyakazi yuko pale kusimamia sheria za kiulinzi za anga na siyo kutoa majibu ya yombo dovya.

    La msingi hapo kwa huyo mfanyakazi ni kumweleza huyo mteja ama alipie gharama zaidi kwa hizo kilo zilizozidi au kuacha mzigo siyo habari ya kukebehi watu namna hiyo.
    Tuache hizo wabongo.
    Ni aibu.Naamini angekuwa mzungu hasingeambiwa hivyo.Au huyo dada alitaka huyo mteja aache pafume nae apate unyunyu nini??Usikute alikuwa anatema kikwapa kweli.Fyuuuuuuuu

    ReplyDelete
  15. Hapa kusema kweli mwenye makosa ni huyo security hakutakiwa kutumia maneno ya dharau au kumkejeli huyo mama.angemwambia tu vizuri na angemuelewa.na ana bahati ajanikuta mie kichwa ngumu angenijibu maneno hayo kwa kujifanya mjuaji ningefungua chupa ya lotion ningemwaga nusu ya lotion kwenye pipa la taka hapo na kwa vile kaniambia nijipulizie perfume ningeipuliza kwenye kona moja ya hicho chumba cha kusubiria kuondoka nusu nzima alafu ngoma ingekuwa draw.
    Cha maana ni kwamba watanzania wote kwa ujumla tuheshimiane kwenye kazi zetu sio kujaribu kumnyanyasa mtu kisa wewe ndio mwenye mamlaka juu ya mtu katika kitengo flani.
    Heshima si utumwa.
    Huyo g7 wa uk kapotoka na kuwa huko u.k ana ushamba wa ulaya bado ujamuisha manake kila hoja yeye anajaribu kuwafanya watu kama washamba akati anajua kabisa huko halipo huwezi ukapewa jibu kama halilopewa huyu dada.
    Mzawa

    ReplyDelete
  16. Habari zenu waungwana,

    Naombeni mnisikilize! Cha!

    Kuna kitu kimoja kikubwa sana kwa upande wa biashara ambapo Africa imekosa sana, Hii ikijumuisha na Tanzania. Kitu hicho ni kuwa na best customer service ktk biashara zao, Pia kumuweka mteja mbele.

    Kama kweli Makampuni, Managers wanao husika, na wamiliki wa uwanja wa ndege wanajua kile walicho soma then watakuwa wanajua kwamba Business do exists because of the so called customers or consumers.

    Unatakiwa siku zote uweze kumuweka mteja mbele na kumuona kama ni mfalme na hii ukizingatia ktk dunia tuliyo nayo kuna mashindano makubwa sana ktk biashara na ukiweza ku-lose plot then umekwisha...

    Inawezekana huyu jamaa ndio alikosea kusafiri na hivyo vitu, lakini huyu dada alitakiwa akumbuke yupo hapo kazini kwa ajili ya wateja kama huyo jamaa na alitakiwa aweze kutumia lugha nzuri na kumuelewesha jamaa. Hiki kitu ndicho Tanzania na Africa kwa ujumla tuna kosa..

    Inatakiwa managers wote waliopo Tanzania waweze kwenda kusoma zaidi eidha ndani ya Tanzania au nje ya nchi na kujua nini maana ya management na kuweza kujua nini maana ya makampuni yao kuweza kuwepo yaani wanafanya biashara kwa ajili ya wateja wao na bila ya hawa wateja then hakuna kampuni na hakuna mfanyakazi yoyote atakaye kuwepo na kulinga na vyeo vyao.

    Mimi nipo hapa UK na nimejifunza mengi sana kutoka ktk maisha ya kawaida na pia ktk elimu yangu. Nimeweza kufanya Research ktk masomo yangu na kugundua ni jinsi gani mteja alivyo na umuhimu ktk makampuni yote ya Uingereza.

    Ushauri wa bure kwa makampuni ya Tanzania na management zao:

    Mnabidi msome zaidi kuhusu market inavyo change na muweze ku-adopt na hizo changes, Mnabidia msome kuhusu Customers / Consumers behaviour, mkileta zile tabia kama ya hii post then mna-destroy kampuni zenu. Someni zaidi kuhusu markets mbali mbali duniani na msome zaidi kuhusu mabingwa wa business na markets i.e. Philip KOTLER, Michael Porter, na wengineo muweze kujua nini umuhimu wa mteja ktk kampuni na market kwa ujumla.

    Managers tumieni elimu zenu mlizo zipata na sio kuziweka chini ya uvungu. We need changes on all sectors in Tanzania. Shame on you all who always acts like the mentioned lady above upon your customers.

    NaWaKiLiShA.

    ReplyDelete
  17. HATA KAMA ANGEKUJA ML10,000, HEBU MWELEWENI MWEZENU HUYO DADA ALITUMIA LUNGHA MBAYA YEYE YUKO KAZINI SOMENI KWANZA MUELEWEWENI MLALAMIKAJI NYUMBANI HAWAJUI CUSTOMER CARE BADO TYKO NYUMA SANA

    ReplyDelete
  18. Huyu jamaa wa UK tunashukuru kwa uliyosema ila tunajua kazi unazofanya hayo ya ushauri huyajui na sikazi zako haiwezekani ukafanya utafiti nakugundua makampuni yote ya uk ni uongo hakuna anaeyefanya utafiti kwa kampuni zote. wewe beba mizigo tu acha kudanganya watz huko hawakotena.

    huyu jamaa alifanya ubabe kwakujua huyu si muhudumu tu wa uwanjani na mimi ni mteja.

    Tujifunze ustaarabu kilamahali tunapohitaji huduma

    ReplyDelete
  19. Anony September 01, 2008 1:01 AM, na Anony Tarehe August 31, 2008 2:49 PM, mnaonesha uwezo wenu wa kufikiri ni mdogo sana.

    Punguzeni pumba zenu kabla hamja anza kuzitoa kwenye blogu la kimataifa na kijamii.

    Mnatia aibu na majibu yenu, Angalia wenzenu walivyo toa concrete arguments.

    ReplyDelete
  20. Mimi nimewahi kuwa na the same issue ya kuwa na liquids zilizodi ujazo kwenye Airport moja hapa Europe, nilikuwa mbishi kidogo kutupa perfumes zangu, muhudumu wa Airport alichonishauri ni kwamba namnukuu..... ''If you don't want to loose your perfumes you can check in your hand luggage''...mwisho wa kunukuu. Wala sikujisikia offended kabisa, kwa hiyo kwa ufupi huyo dada hakupaswa kumjibu hivyo huyo msafiri, angeweza kumwambia acheck in hand luggage kama anataka, so decision ingebaki kwa msafiri. Nikirudi kwa G7 kwa ufupi nimekushusha hadhi tangia leo, kama huna cha kuchangia unaweza kukaa kimya na kuwaachia wengine, inaonekana wewe hujawa civilised vya kutosha.

    ReplyDelete
  21. tatizo nikwamba how many times hawa watumishi wa airport wamekuwa wakarimu kwetu? Nashukuru mara zote nimepita air port za kwetu sijasumbuliwa tena wamekuwa wakijitahidi kutoa service kadri ya uwezo wao. ukisikia maada kama hizi nikwamba hao watu wamejitahidi kumuelewesha mtu na akashindwa kutoa ushirikiano na hapo ndipo mambo hayo hutokea.
    Kuhusu kuhojiwa wazungu wakaachwa wala sio Tanzania tu, mimi yamenitokea amstadarm, Dubai, manchester and mara zote unashangaa kuona baadhi ya watu wanapita.. nisuala la kutoa ushirikiano sio kujifanya unaonewa tu.
    sema watu mumezowea kuwaonea watendaji wahome as if they are stupid hawajui kazi.. pia mujuwe kiburi cha wabongo kwenye maeneo hayo pia. Pia sio kwakuwa police UK and western world wapo polite ni the same kila sehemu. some places ukiwa polite kama bongo mambo hayaendi at least kwasasa mpaka some time hapo baadae.

    Just behave wale wadada wapo poa tu wala haiitaji research wala nini hii kitu ni natural.

    otherwise nasema am sory kwakumuita mpumbavu... but starborn pple huwa nimezowea kuwaita wapumbavu.

    G7
    UK

    ReplyDelete
  22. Jamani hivi hamjui UK ni ukonga? mbona mnapiga ngumi ukutani! kama dada alikuwa amechoka angekaa nyumbani kwa kifupi Customer care nyumbani ni 0 hutakiwi kujibu mteja namna hiyo hata akikutukana au hata kama anamakosa yakikuzidi unatoa taarfia kwa mkubwa wako sio unaleta mambo ya kidole juu hapa. Na wewe uliyeko ukonga kama huwezi kufikiri acha kutoa hoja naona vumbi la ndege linakuathiri hapo jirani

    ReplyDelete
  23. Haya maelezo ni ya upande mmoja kwa hiyo basi ni wajibu kufikiria ni nini kilipelekea hali kama hiyo kutokea
    ...kilichozungumzwa kuwa huenda
    mtoa malalamiko ndiyo mkorofi...

    Hiyo ni moja kati ya possibilities. Sasa basi hii inawezaje kuwa ndiyo the highest possibility;
    ni hivi huyo msafiri ameendelea kulalamika kupitia katika blog hii ambayo si rasmi katika kufikisha malalamiko yake. Inaonesha pia ni jinsi gani ambavyo hajui taratibu za kimawasiliano, zaidi ya hapo inaonesha ana tatizo kubwa la kuwasiliana na huenda ndiyo chanzo cha kadhia iliyomkuta.

    Ninakubaliana na mchangiaji ambaye ameeleza kuwa psychology inaweza kufanya kazi ya kutambua jambo, especially kama hili.

    Mimi katika viwanja vyote vya ndege nilivyosafiria kuna trash can katika sehemu ya mwisho ya ukaguzi, endapo kama una
    kitu cha kimiminika kisichokidhi matakwa kwa hakika utakiacha hata kama ulikununua kwa bei mbaya.

    Isitoshe wakati wa ukaguzi wa mwisho hakuna majadiliano kwani unaweza kusababisha hasara kwa watu ama taasisi zingine endapo kutakuwa na uvunjwaji wa taratibu.

    Kimsingi katika nchi zilizoendelea unatakiwa kuwajibika kwa vitendo vyako mwenyewe ama iwe ni makosa au kutokujua taratibu.

    Mwisho, napenda kutoa angalizo kuwa TCAA hawahusiki na security ya boarding last security gate huwa inaangaliwa na Airline wenyewe au mamlaka husika ya kiwanja cha ndege.

    ReplyDelete
  24. Customer care ni mbovu sana kwa wengi wa watanzania,kuna kero nyingi kupita kiasi,alimuradi wewe mteja ndie uanze kujikomba/ kujipendekeza kwa muhudumu ndipo upate huduma kwa furaha, ukweli tubadilike kwa wale wenye tabia kama hizo tukiwa kwenye kutoa huduma kwa mteja lugha taurua/lugha murua ni muhimu sana hata mteja kama atakua anakosea wewe maneno yako mazuri yamtulize na kujaribu kubadilisha muelekeo endapo alishaanza kukasirishwa na sheria au mipangilio ilyowekwa.

    Huyo security officer hakupaswa amkasirikie mteja wake angemuelewesha vizuri,hata kama mteja alikasirishwa na kitendo cha kuambiwa asipite na hivyo vimiminika kwenye pochi ya mkononi.

    Pole mdau ndi mambo yenyewe kipindiwalipokuwa hawajarekebisha aiport ya mwanza tukivuliwa viatu na kupekua kwa miguu na viatu umeshikilia mkononi baba mzima kama unaingia rumande kumbe unasafiri tu kwenda Dar, fikiria ushalipa cristalsaloon kwa paul sh 15000/- kwa pedicure na moneycure unaambiwa upekue tena kwa kauli mbaya utafikiri anakuonea choyo jinsi ulivyomaridadi sasa anakupa adhabu za afande chacha wa JKT.

    ReplyDelete
  25. G7 anifurahisha na unanga wake. Hata kama huyo mtumishi atasema mara mia moja...hiyo ndo kazi yake. Kwa nini amfokee mtu? Kama amechoka na kazi aseme.
    Wewe polisi apigapo muhalifi ni haki? Kukutana na watu vichwa maji ni sehemu kubwa ya kazi yake...lakini hakuna sehemu inampa haki ya kumpiga mtu. Lazima awe na subira. Hasira hasara bwana.
    Alafu inaelekea wewe hujui ku-deal na watu hata kidogo. Wajiona mjanja huku waandika starborn...hehehe. Check spelling jamani. Hiyo masters ni ya kugawa au vipi?...tehehehe
    The guy has all the rights to complain.
    Mimi na sidhani mtu mwingine yeyote anaweza kupelekana na mtu anamuita mjinga. Yani hilo tendo alilofanya na sawa na kumuita mjinga. Chukua jina lake next time ukatoe ripoti au hawavai name-tags?

    mtoto

    ReplyDelete
  26. Mie pia wiki mbili zilizopita ilinipata hiyo wkt naenda KIA na PW. Security check ya mwisho ndo naambiwa siruhusiwi kusafiri na body spray yangu pamoja na mosquito repellent (sparay) sbb vimezidi ujazo. Ninachotaka kujua kwa sisi wateja ambao tulikuwa tunasafiri mara ya kwanza kwa ndege, tungejuaje?? Na security check ya mwanzo kabisa pale mlangoni kwa nini hawakunambia hivyo hadi nilipofika mwisho? Ingekuwa ni busara kwa uongozi wa JNIA kuweka tangazo pale kwny mlango wa kuingilia kuwa vitu hivyo pia haviruhusiwi kusafiri navyo kwny hand lagguage. Na walipovichukua, wala hawakuvitupa kama wanavyookuonyesha lile pipa, badala yake waliviweka kwny mfuko uliokuwa pambeni na sio kwenye ile dustbin walionionyesha!

    Nilipenda sana nilipokuwa narudi pale KIA huyo mtu wa ku-check in akanambia mapema kabisa, kama una perfumes, spray au lotion mwachie ndugu yako huko nje, hawaruhusu kusafiri navyo.

    ReplyDelete
  27. Jamani hapa ni issue kubwa.
    mi namuungamkono mlalamikaji,hata mimi ilinitokea hii,kaka yangu alikuwa anasafiri wenda nchi fulani,wakati wa ukaguzi wa kwenda ndani check-in mbele yake na nyuma yake walikuwepo wazungu wengi,wale wazungu walikuwa hawakaguliwi kabisa,wanapita tuu,basi alivyopita yeye wacha wamkague hadi wamfungulie begi,sie tuliokuwa nje tukauliza nyie vipi mbona hamkagui wanzungu mnakagua weusi tuu,yule security wa nje alichotujibu ni kwamba nyie wabongo hamjazoea safari ndio maana tunawakagua sana hawa wazungu wamezoea safari,basi na sisi ndio tukaanza kumpa ukweli wewe haiwezekani ukatuzalilisha wabongo wenzio,basi akatokea dada mmoja anaitwa mage kama sijakosea na anavaa miwani,basi akasema nani kasema,kama nyie mnajishaua ngoja nikufundishe na nikikomeshe,akamuita polisi wa kike kuja kutuweka chini ya uliza na kutusingizia kuwa tumewatukana khali hali wao ndio walitudhalilisha pale nje,yule dada alivyotoka akatuacha na polisi ndani,yule polisi akatuambia uyu dada ni mkorofi sana tena sana ,nyie mumuombe msamaha,basi mama yangu akaanza kumuomba msamaha,akasema,sikubali umeeingia choo cha kike lazima nikuonyeshe mie ni nani,basi yule mama wa watu mtu mzima kamuomba msamaha yule binti hata kwa kosa ambalo halikutaki uku akitueleza nyie airport mnaijua au hamjui kuwa kuna mambo ya ugaidi,sasa je huu ugaidi wanafanya watu weusi tu.Watanzania tupendane natusijishushe hadhi wenyewe kwa wenyewe hawa wazungu wenyewe wanatubagua na kutudharau sasa na sisi pia tujidharau?.tutakimbilia wapi sasa?.lakini nakuambia toka hapo basi na wazungu wakaanza kukaguli.hii sio hapo tuu.hata siku moja one of my friend ana passport ya Europe siku anarudi kwake pale airport akaulizwa wewe hii passport ni yako wewe hauwezi kuwa nayo utakuwa umeiba ya mtu,lakini uyu dada maana alikuwa ni mzungumzaji mzuri aliamuambia wewe mimi sababu ni mweusi mwenzio ndo unaona kuna tatizo,lakini hawa wazungu wanaopita bila kuuliza uenda ndio wanapitisha mambo yasio maana wanajijua hawaulizwi sana au hawaulizwi kabisa.

    na wakati mwingine wanasema hee because i am mzungu ndio maana nikapita.(hata kwenye huduma tofauti hapa tz)

    Airport kwa kweli wanapaswa kubadilika,kama mmenotice mtu akija kutoka nje awe mzungu,anaweza kutoka nje kuja kuchange pesa then anarudi ndani,na akatoka na handbag yake kabisa mkashikia kwanza bila hata kukaguliwa je mtu kama uyu anakamzigo kake halamu si kameshapita,pale kuna mapungufu makubwa sana tena sana,

    mi inaniuma kama mtu anamtuhumu uyu mtoa maoni(mteja) kama uyo anayejiita G7 kwanza jina tu linamuonyesha bado ni limbukeni,wewe toka lini mtu mzima na akili zako,sina hakika kama ni msomi.anajipachika jina la watu eti G7 UK pole kaka,

    Na mwisho WATZ tujipende na wafanyakazi wa airport wawe wanapelekwa training ya kuhudumia wateja mara kwa mara.

    ReplyDelete
  28. hawa wanahitaji ubabe tu...kama kumpiga unampiga kiuhakika...kha. wacha iwe mbaya kwa wote! Yani mpk kurudi tz inakuwa taabu. Toka wapi unaanza kuwaza duh...customs na security nitapitaje. Ngoja siku aje gaidi wa uhakika awape mambo. Mie wananiudhi kabisa. Pamoja na traffic...kila kona kuomba omba tu! Ndo maana nafuu kutoishi bongo...taabu tu. Mtu akiwa na cheo anakunyanyasa utadhani boss wako...

    ReplyDelete
  29. hapo hamna kitu...hamna cha customer care/service wala nini....Huku tuliko wala hawafungui mdomo wale watu...Ni wanatupia kwenye liplasic bin lao hapo pembeni yao ....bila hata kukupa sababu na ukiuliza wanakupoint kwa mtu atakayekuepa maelezo zaidi. Na ukileta ujanja unajikuta unapelekwa kwe kile chumba na ukijidai zaidi pingu mkononi na ndege yako unaimiss....

    Hapo huyo mlalamikaji alitaka kuzipitisha kwa kujifanya he/she knows better...Na kama wewe ni stoke holderr unatakiwa kufuata sheria, sio kuzivunja.

    Inatakiwa hao wanaosearch wasiongee kitu but kutupa tu na ukitaka jawabu wawe na watu wanaospecialized kuelezea ni kwanini wametupa kama hata kusoma sheria za kuboard ndege huzijui.

    Mdada wa watu si ajabu amefanya kazi masaa zaidi ya kumi na siku nzima ni watu kama wewe mnaojua sheria lakini mnataka kuzitest. Na siajabu alikwambia hizi haziendi ...ukawa unalalamika ndio akakwambia kama unazimindi tumia zote all at once

    Tusiwalaumu wafanyakazi wetu na siye wabongo vichwa ngumu tu...kila mahali tunazania tutatumia kiswahili kirefu to get by...... Kama unataka kupitisha liquids zako kwanini usicheck in mzigo wako, ukabakia kurelax tu?

    ReplyDelete
  30. Michuzi huyo G7 ni mkurya? Am curious! Kiswahili yake mbofu mbofu sana, asingejitia ujuaji hivyo. Munafanana, mukisafiri, munaona. Nini hiki we G7? kajifunze kiswahili ndo urudi humu globuni!

    ReplyDelete
  31. G7,UK, AKILI YAKO HAINA AKILI, UMELEWESHA BADO UNACHANGIA PUMBA.

    ReplyDelete
  32. mie kwa ushauri wangu ninavojuwa ukisafiri safari za nje ya nchi hasa ulaya ndio huchuuwi zaid ya 100ml kwenye hand laggage lkn kwa africa tu sijasika na huyo mmama anaonaekana hajali kazi yake wapo wafanyakazi wengi sana pale nuymbani tananza ni mafedhulisana sijui kwauchoivu au maumbile yao mi nmamshuri huyu amuwekee skadi n je vijana wa kazi wamkate ulimi itakuwa dawa kwa wengine na funzo zuri

    ReplyDelete
  33. Inashangaza watu wanavyotoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja tu. Sote hatukuwepo uwanjani lakini dalili zinaonyesha palitokea mazungumzo makali kabla ya mambo kufikia yalipofikia. Kwenye viwanja vya ughaibuni ukileta masuala ya kujibizana kwenye mambo ya usalama na uturi wako unaweza kupelekwa kwenye chumba cha faragha na mtu aliyevaa glovu...

    ReplyDelete
  34. Me naugana na wale wanaosema customer service bongo utumbo. Imeshanitokea, me sikuwa hata na hizo perfumes zilizozidi ujazo kazi ilikuwa pale nilipotoa passport ambayo so ya kitanzania. well wageni wote watembeleapo bongo wanaweza kupata viza pale uwanjani. nilifuata sheria zote nimepanga mstari kama wazungu walivyofanya. nadhani nilichokosea ni kuongea kiswahili wakati nina kitabu cha nje. Security wacha alete mizengwe na maswali kibao eti oho nimeipata wapi hiyo passport na kwanini sina ya kitanzania. viza itakuwa ngumu kupata unless kama nitatoa cha juu. Siamini niliwekwa pale uwanjani for 2 good hours. Wafanyakazi wa uwanja wa ndege always have a reason to piss u off!

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 15, 2010

    na wewe Anonymous Sep 01, 11:28:00 PM,

    uliyemrekebisha mwenzio kiswahili na chako ni kibovu vilele....nawe G7 sikujua kuwa ubebaji wa box unaweza kupunguza uwezo wa kufikiri.....

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 26, 2010

    Wote mmeongea point nzuri sana. nawashukuru wa tz wenzangu.Tatizo hapa wala sio tu kwamba hakuna good customer service bali ni poor communication. Pale mlangoni panatakiwa paew na maandishi makubwa ya kusomeka vizuri kwa lugha kuu mbili za nchi zikimwelekeza msafiri/mteja kwamba kama ana vimiminika kwenye hand laggage aweke kwenye check in luggage. vinginevyo awape jamaa waliomsindikiza. Kwa nini basi hawafanyi hivyo? Wanavitaka wao au roho mbaya tu au vyote viwili.


    mkufunzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...