rais wa zanzibar mh. amani abeid karume na mkewe mama shadya katika picha ya pamoja na will smith na mai waifu wake jada pinckett smith ikulu zenji
rais wa zanzibar mh. amani abeid karume akipiga stori na will smith
rais amani abeid karume akipokea zawadi ya sovenia toka kwa will smith aliyemtembelea ikulu ya zenj ijumaa hii, kwa mujibu wa mdau othman maulidi wa zanzibar leo aliyetuletea picha hizi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. usingeambiwa utafikiri waungunja fulani yaani Jada utafikira mtoto wa kizanzibari

    ReplyDelete
  2. bi jada asalamaaleikum!!! lookin good with mtandio but the shoes shows u r not from there.

    ReplyDelete
  3. we anonymous wa Tarehe August 30, 2008 7:57 AM acha uzushi mbona mama karume viatu vyake dizaini hiyo hiyo tu sema vyake nimechongeka na nyeupe.

    ReplyDelete
  4. wewe anonymous wa pili namna gani? ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi! hivyo viatu vinaonyesha nini ambacho mzanzibari hawezi kufanya? yaani unataka kusema kuwa sisi hatujui kuvaa viatu? au unasema kwa kuangalia picha tu viatu hivyo ni ghali wazanzibari hatumiliki? ahsante sana kwa mawazo finyu ya ndugu zako wa visiwani.

    ReplyDelete
  5. zanzibar ni njema, atakae aje...! Ukija zanzibar utapelekwa ikulu kama Willy…!

    Halafu utapata wenyeji wenye ukarimu na upendo, watakutembeza dole, mchamba wima, mnara wa mbao, soko muhogo, na malindi pia utapelekwa ukaone simba na ukali wake alivyonyweshwa chai..! Ha ha ha usiogope, kama utashindwa kukaa kwenye MKEKA utapewa KIGODA ukalie…!

    Zanzibar MINAZI tele, kuna mirefu na mifupi (twaita kitamli), minene na myembamba! Kama utapenda kula nyama ya dafu ukisha kunywa maji yake basi UTACHOKOLEWA, na ukinunuwa vocha ya simu pia UTASUGULIWA wala hupati tabu Zenji raha kila kitu wafanyiwa..!

    Kama WALI WA KUNDE ukisha iva UTAPAKULIWA (zanzibar hakuna self service), yaani kila kitu we utakarimiwa! Kama huna kazi mashaallah..utapelekwa pwani ya KIWENGWA ukapare samaki au “UTAPARA MIWA” mahonda! Huko mahonda ndo kwenye kiwanda chetu cha sukari, zanzibar miwa teleeeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  6. Will Smith angekutana na Gordon Brown wa Uingereza sidhani kama angemvalia viraba mtoni.

    Halafu, ningekuwa mimi Rais sijui kama ninge entertain mcheza sinema Ikulu. Sijui. Labda nina mawazo mgando, lakini sidhani kama mtu mwenye gravitas kama Nyerere angekutana na mcheza sinema Ikulu. Sijui.

    ReplyDelete
  7. Nyerere ?
    Kwa taarifa yako Harry Belfonte, alionana na kukaribishwa na Nyerere na wakanywa chai pamoja, (hapakuwepo halua tu hapo)

    "Ambassador Bomani [the Tanzanian ambassador to the United States] came and said to me, " There will be a car to pick you up to take you to the president. You will meet with the president alone,.... ". Nukuu ya Maneno ya Harry

    Ukitaka listi ya wengine waliokaribishwa na Mze Nyerere utapewa..kama ninayemzungumzia hapa humjui uliza pembeni yako

    ReplyDelete
  8. Hi Anon "August 31, 11:36AM"

    That quote was from Sylvia Hill. An American peace activist and not Harry Belfonte. check this link ..

    http://www.noeasyvictories.org/select/08_hill.php

    ReplyDelete
  9. i see no mikonoz zere!!!!

    ReplyDelete
  10. Halafu huyu Will anafanana na wakina Ba Hamadi

    ReplyDelete
  11. watanzania ni kujichanganya tu!!!
    sasa kama zanzibar ni nchi ndani ya muungano na si nchi nje ya muungano mtu maarufu kama huyu will smith ambae ni milionea huko marekani angewezaje kutambua uwepo wa raisi wa zanzibar?????
    hivi watu hawaoni kua system nzima ya muungano ni changa la macho???au kwa vile wanahisi kua wao haiwaumizi ndo mana wanapendelea wenzao inowaumiza wasieleze hisia zao juu ya muungano???
    hemu na hizo kero za muungano zitekelezwe halafu uskie kama kuna mtu atakaeponda muungano...!
    kilicho kuwepo saivi na ninachokiona miye ni kua wazanzibar wanajaribu kuinua sauti yao kupitia mjadala wa zbar ni nchi au si nchi kuelezea hisia zao na kutopendelea kwao system nzima ilokuwepo ya muungano.....hakuna asiekataa ukweli ulio kuepo sasa juu ya hadhi ya zbar ndani ya tanzania...
    tatizo la serekali ya tanganyika ni lile lile la siku zote la kuwapelekesha watu na kuficha ukweli mzima juu ya muungano wakati time has run out na watu wameshakuwa watambuzi juu ya masuala mbali mbali nje na ndani ya muungano kiasi cha kua huwezi tena kuwafool rabda kuwaforce...
    ok lets say zanzibar si nchi....wanachotkitaka wazanzibar ni kuwa wapewe mamlaka yao binafsi na huru ya kuwa nchi nje ya muungano either kwa kukuepo muungano au kutokuwepo..kwani huo muungano wenyewe hauna maana hata kidogo...
    watu kua ndugu na kuishi sehem yoyote either tanganyika au zbar isiwe ndo sababu ya kulazimisha muungano..!
    watu kama jamii wataendelea kua karibu na ndugu kama zamani ila haya mambo ya kuunganisha sera za kivyama na utawala ndio yanayoiumiza zbar kwa kweli!
    mbona tanganyika imeshikilia sana kuikumbatia zbar bila kutoa sababu za msingi za kufanya hivo linapokuja suala la kuquestion uhalali na ubora wa muungano????
    au kuna kitu kimejificha???
    watu zbar hawataki tena system ilokuwepo ya muungano...lete system nyengine au achana na wazanzibar na ujali mambo yako ya tanganyika ewe kiongozi wa kitanganyika!
    zbar will take care on it's own..
    zbar ni nchi na inajulikana dunia nzima ila tu tanganyika inaibania kujiexpress duniani na kujitaftia maendeleo!
    huo ndo ukweli kataa au kubali!

    ReplyDelete
  12. He is the most handsome man I've ever seen alive. Luv you Willy!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...