Mmoja wa wazazi waliofika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, akitoa msaada wa kushikilia kwa chupa ya dripu ya dawa kwa mwanafunzi aliyedhurika na dawa ya chanjo ya Kichocho na Minyoo iliyofanyika jana
Mmoja wa mzazi wa mwanafunzi anayeelezwa kuathiriwa na dawa za kichocho na minyoo akiwa amembeba mtoto wake kumpelekwa wodini kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro wakisaidiana na wazazi wa wenye watoto walioelezwa kuwathiriwa baada ya kupata chanjo ya dawa za kichocho na minyoo jana katika Shule mbalimbali za Msingi za Manispaa ya Morogoro.

ZAIDI ya wanafunzi 363 wa shule za msingi mkoani Rukwa na Morogoro leo walikimbizwa katika hospitali mbalimbali baada ya kuanguka na kupoteza fahamu muda mfupi baada ya kupewa dawa za kinga ya kichocho na minyoo katika mikoa hiyo.

Kutokana na hali hiyo utoaji wa chanjo katika mikoa hiyo ulilazimika kusimamishwa kwa muda usiojulikana.

Tafrani kubwa ilizuka baada ya watoto hao kupoteza fahamu mara tu baada ya kunywa dawa hizo.

Habari kutoka Rukwa zinasema kuwa utoaji chanjo hiyo ulisimamishwa baada ya wanafunzi wa shule za msingi kuanguka na kutoa povu mdomoni huku baadhi yao wakitapika na kupoteza fahamu.

Kutokana na hali hiyo wazazi wa wanafunzi hao walivamia shule hizo katika Manispaa ya Sumbawanga hususan shule za msingi Chemchem, Katandala, Mwenge, Malangali na Jangwani wakitishia kuwapiga walimu kwa kile walichodai kuwa wamesababisha hali hiyo.

Hali ilizidi kuwa mbaya wakati wazazi wa wanafunzi hao walipofika hatika hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga na kukataliwa kuingia wodini wakiwa na lengo la kuwaona watoto wao waliokuwa wamefikishwa hospitalini hapo kupatiwa matibabu.
Wazazi wa watoto hao waliwapiga mawe madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo huku wakilia kitendo kilichosababisha polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia wapelekwe hospitalini kuwatawanya wananchi zaidi ya 600 kwa kutumia mabomu ya machozi.
Mabomu hayo yalipigwa kwa zaidi ya saa tatu na kuweza kuwatawanya wananchi hao waliokaa umbali wa mita 500 ingawa baadhi yao wakiendelea kulia wakidhani watoto wao wamekufa.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk. Saduni Kabuma alisema wanafunzi wote waliofikishwa katika hospitali hiyo wamepatiwa matibabu na wengi wao wameruhusiwa.
Alisema hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyefariki dunia kwa tukio hilo au aliyekuwa mahututi baada ya kumeza dawa hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Daniel Ole Njoolay aliwataka wazazi wa wanafunzi hao kutokuwa na uamuzi wa kukurupuka katika kukabiliana na matatizo badala yake wawe wasikivu kwani serikali kamwe haiwezi ikawapa sumu raia wake.
Mh. Njoolay amewataka wazazi mkoani Rukwa kuwapeleka watoto wao kesho kuendelea na chanjo ya surua na polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwani ni salama na wala hakuna madhara yatakayotokea.
Huko Morogoro chanjo ya kichocho na minyoo imekwama kutolewa baada ya kuzuka vurugu katika shule mbili ulipoenea uvumi wa kufariki dunia kwa mwanafunzi baada ya kupewa chanjo hiyo.
Katika utoaji wa chanjo hiyo wanafunzi 63 walizirai na kufikishwa katika hospitali ya mkoa kwa matibabu.
Vurugu zilizozuka zilisababisha polisi kutumia mabomu ya kutokwa na machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika maeneo ambako chanjo hiyo ilikuwa ikitolewa huku wakiwarushia mawe wahudumu na walimu kuwalazimisha wawaachie watoto wao warudi majumbani.
Polisi inawashikilia watu 25 wakiwamo wanawake wawili kutokana na vurugu hizo, zilizoanza jana saa tano asubuhi katika shule za msingi Mafisa A na B, katika Kata ya Mwembesongo hali iliyowalazimu walimu kupiga simu Kituo cha Polisi kuomba msaada wa ulinzi.
Katika vurugu hizo polisi mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Clemence Bazo, alijeruhiwa kwa kupigwa jiwe chini ya jicho lake moja na kupelekwa kwenye Hospitali ya Mkoa kwa matibabu ambako alishonwa nyuzi sita.
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, afande Thobias Andengenye alisema jeshi hilo lilikuwa halijapokea taarifa ya mtoto aliyekufa kufuatia chanjo hiyo.
Wakati huohuo, Mganga Mkuu wa mkoani Morogoro, Dk. Frida Mokiti amesimamisha utoaji wa chanjo hiyo ya kichocho na minyoo hadi itakapotangazwa tena kwa mkoa huu.

Picha hizi za matukio mbalimbali mkoani Morogoro ni kwa hisani ya Mdau John Nditi wa Morogoro na habari ni kutoka kwa mdau Gurian Adolf akiwa Rukwa na John nditi ambao wote ni watendaji wa gazeti la HabariLeo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Aibu,aibu!!Wizara ya Afya.Poleni sana waathirika, mungu yuko pamoja nanyi!

    ReplyDelete
  2. Ndio tatizo la kukariri definitions na kuiba vyeti sasa munataka kuua watoto wa watu.

    Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  3. Haya tena makubwa, kinga inaua kuliko kuponya!!!!!!! badala ya "KINGA NI BORA KULIKO KUPONYA???
    Mwee, jamani, jah; tutafika kweli???

    Poleni sana wale wote mlopatwa na msukosuko huo.

    ReplyDelete
  4. Ivi kweli tunakwenda wapi Tanzania?majaribio ya dawa wanakwenda kujaribiwa watoto wa masikini kweli ni haki??
    kwanini basi wasinge sema wawachome watoto wa bunge au shaaban robert? mtoto anakaa mjini morogoro kichocho kitoke wapi?? kwanini uchunguzi wa dawa usifanyike kwanza??
    kweli tanzania kichwa cha mwenda azimu siku zote wasomi tunao wa kufoji vyeti tuu.
    ila tukija kwenye swala la ufisadi kila mtu mjuaji.

    ReplyDelete
  5. Haya mnayo yaona ni sawa sawa na kwenye movie ya The Constant Gardener ambapo makampuni makubwa duniani wanaitumia Africa kuweza kufanya experiment trial ya madawa yao na matokeo yake ndio kama mnavyo ona.

    Hao watoto wamefanywa kama guinea pigs ili kuona reactions za hayo madawa.

    Tunataka uchunguzi uweze kufanyika na kupatiwa majibu ya wazi na ya kiakili ni kwanini hao watoto wapate hizo reactions!?

    Tunasubiria majibu.

    NaWaKiLiShA.

    ReplyDelete
  6. pole kwa watoto waliowaamini viongozi wao na madaktari na kujitoa miili yao kupata chanjo ili tu wajikute wako hosipitali kuokoa maisha yao
    hii nchi sijui imelaaniwa?
    ila viongozi mazuzu ndo maana tumeikimbia, ngoja tuone kikwete atasema nini
    vijana mkipata chance tafuteni njia kimbieni huko sio sehemu ya kukaa

    ReplyDelete
  7. Kinga ni nzuri lakini ina madhara yake bwana sio bongo tu. Huoni sasa hivi USA wazazi wanakataa
    watoto wao wasipigwe shot ya APV?

    Wanasema hiyo ni kinga ya cervix cancer lakini wengi wa waliopigwa hata wengine wamepooza baada ya kupata hiyo kinga.

    Ni vizuri kabla hawajawapa watoto hao vitu hivyo waongee na wazazi wao na kuwaeleza side effects za dawa yeyote ile.

    Na pro and cons ni vizuri kuzijua. Sometimes kichocho na minyoo one could beat without those crappy vacinations. Mbona walienda shule wengi pekupeku na vile vyoo vya shule lakini watu hawakupata vichocho wala minyoo.

    Poleni

    ReplyDelete
  8. Jamani hiyo ni chanyo gani kitaalamu? ya kichocho na minyoo? manake wengine pia tunasoma tiba lakini hatujaoikia huku ughaibuni.Au ni mpya? Au imetengenezwa kwa ajili ya Tanzania pekee? Please kama kuna mtu anaijua jina la kitaalamu la chanyo hiyo asisite kuandika ili nasi tuijue?

    ReplyDelete
  9. ukweli inasikitisha ni watoto wa watu wadogo lazima wazee wawe na hasira masindano kama haya lazima kwanza yafanyiwe uchunguzi kabla ya kuchomwa, hebu tuone jinsi watoto wengi wamepoteza faham ushukuru kuwa hakuna aliekufa lkn jee hao wanafunzi wote walichomwa na kuzirai jee wangelifariki ingelikuwa kosa la nani? wangelipotea wanafunzi wengi tu na wazazi wao wasingelikubali,na kwa tatizo hili llilojitokeza sijui mzazi gani atakubali tena mwanawe achomwe sindano yoyote ya kinga maana watakuwa na wasiwasi na kutokuwaamini wizara ya afya.MAMA WATOTO

    ReplyDelete
  10. Hapa kuna watu wanahitaji kuwajibika...hamna kingine. Kuanzia waziri ajieleze na hao waliotoa chanjo. Tena watu wanahitajika kupelekwa mahakamani...Hakuna kucheka na nyani tena. Kila siku tunavuna mabua tu...kha!

    mtoto

    ReplyDelete
  11. Daah mtihani huu! Nakumbuka mwaka 2006 zoezi hilo lilipo fanyika Kisiwani pemba, wapemba walikataa kuwapeleka watoto wao kupewa hiyo chanjo ya minyoo na vichocho! Waligoma kwa kujuwa kwamba dawa hizo zina madhara, walikuwa wanahoji iweje dawa ya maumivu kama panadol au aspirine wanauziwa, lakini dawa hizo wapewe bure?! Wakasema itakuwa wanataka kufanyiwa majaribio (wao wawe ni sample)na sababu ni majaribio lolote linaweza kutokea! Hili ndilo lililowapata wenzetu wa morogoro!

    Hizi dawa zinazokuja kwa jina la msaada ni hatari sana! Huwa bado zinafanyiwa majaribio na wao huona africa ndio sehemu za kufanyia majaribio dawa zao? Yaani sisi watanzania (waafrika) hatuna thamani hata tukifa pouwa tu! Lakini hili linachangiwa na umaskini wetu wakujitakia na ujinga wa viongozi wetu na ubinafsi!
    Mbona hatuoni watoto wa vigogo wa serkali wakipewa hizo chanjo? Au watoto wao hawahitaji chanjo?!!!

    ReplyDelete
  12. Hapa inaonekana kuna kampuni ya kigeni ya madawa imetumia udhaifu wa nchi yetu kiutawala kufanyia majaribio watoto wa Tz. Kinachotakiwa kufanyika ni hiyo kampuni kushtakiwa, ilipe hao watu mpaka ifilisiwe. Jamani wanasheria wenye uchungu na hii nchi nawaomba mjitokeze kuwasaidia hawa watoto wa maskini kushtaki liwe fundisho kwa makampuni ya madawa yanayotuchezea. (*(&^&mbafu!

    ReplyDelete
  13. This is horrfying news....how in the world is this possible??something was wrong wit tht vaccination either it has been expired or not approved??
    Tatizo ni kwamba haya madawa yanayozinduliwa na wazungu yanapimwa kwa wanyama sungura,nguruwe n.k huwezi kujua vp itakuwa reaction kwa
    mwanaadamu...I think some serious action must be taken abt this huwezi kujua labda hio chanjo ina side effects zaidi ya hizo zilizojitokeza.....Tanzania bado tupo nyuma

    ReplyDelete
  14. If anyone have read a novel or seen a movie called 'THE CONSTANT GARDENER',which was tok place in Kenya,Nairobi involves tesing of a tuberculosis drug which had a servere side effect...Which costed a lot of pplz death just to reveal out the truth...It needs a lot of courage to do something like tht and thts wats exact happened to those poor innocent kids which were given vaccination with severe side effects.... Something must be done...

    ReplyDelete
  15. kwanza mtawapaje watoto dawa bila kuwapima kujua wana matatizo gani?, kuna wengine wana magonjwa hamjui mgetakiwa kuwapima kwanza kujua kam wana alerg au lah! mnajishaua watoto wenu mbona hamuwapi, AIBU-OVYOO...

    ReplyDelete
  16. me nikisema tanzania hatuna viongozi tuna mifano tu watu wanakataa,sasa angalia halfu nafkiri hii si mara ya kwanza kutokea ilishawahi kutokea,huku nilipo ingetokea wangewashtaki,masikini watakufa kila siku.Kwanini wasingeenda kujaribu katika shule za fm academia kama st marys,feza na nyingine?wameenda huko vijijini kwa watu wasiojua hili wala lile,tanzania kazi mnayo mna vilaza watupu na si watu tunaowahitaji waongoze.Haya poleni

    ReplyDelete
  17. Litakuwa jambo muhimu na bora kwa wizara ya afya kufuata taratibu zenye uangalifu mkubwa wanapotoa chanjo au dawa mpya kwa wananchi:
    1. wizara/daktari mkuu manispaa waanze na kundi dogo la watakao pata hiyo chanjo/dawa na siku kukurupuka na kuwapatia chanjo/dawa wakazi wengi kwa mara moja.
    2. chanjo/dawa mpya ziwe zinatolewa ktk maeneo ya hospitali, ili wanaodungwa au kunywa dawa hizo waambiwe kubaki ktk mazingira ya hospitali walau kwa nusu saa kuangaliwa hali zao.
    3. wakati wa kampeni za chanjo/ kutoa dawa, wawepo wataalamu wa kuangalia madhara na mafanikio ya chanjo hiyo.
    4. wizara/daktari mkuu wa mkoa/manispaa/wilaya wafanyie kazi matokeo ya hili zoezi na kutaarisha taarifa kwa ajili ya matumizi ya kuratibu huduma za chano/dawa kitaifa.
    Mdau
    Rocky
    London.

    ReplyDelete
  18. Hakuna hata gazeti lililoandika hiyo dawa inaitwaje, imefanyiwa clinical trials wapi, imepitishwa na regulatory body gani, imeanza kutumika kwa mara ya kwanza lini na wapi, imenunuliwa au tumepewa bure na nani. Hakuna!

    Daktari Mkuu wa Mkoa amesema "serikali haiwezi kuwapa watoto sumu," lakini hiyo sio ishu hapa wewe daktari wa kukariri definitions!

    Ishu ni kwamba mmewapa watoto li chemical ambalo halija testiwa kwa watoto wa hao alchemists waliolikoroga, sijui wapi huko, mnajua wenyewe mlikolitoa! Lousy leaders, crummy press.

    ReplyDelete
  19. hizo dawa zimetengenezwa wapi? africa population is high so mnapunguzwa bila kujua.

    maradhi kama kichocho chanjo yake si vidonge wala injection.
    ukiangalia pathology ya pathogen huyo ni kama ifuatavyo;
    kichocho kinasababishwa na parazite aitwae schistoma haematobium(kwa aeast africa),ambaye ana host wawili mmoja ni snail ambaye anaishi ktk maji machafu,akishakuwa aduslt stage anataga mayai yake na kuelea ktk maji,na kwa vile mayayi hayo yana spikes au vincha vikali kwa kiswhili binadamu yeyote akiingia ktk maji hayo mayai hayo hutumia ncha hizo kupenya ktk ngozi na kuingia ktk mishipa ya damu na hasa huathiri urinary system,hivyo mtu hupata maumivu makali akitaka kukojoa,hukojoa damu na dalili nyengine

    mimi naona KİNGA Nİ KUDHİBİTİ MİTO NA MAZİWA WATU WASİTUMİE MAJİ HAYO KWA KUOGA AU KUYATUMİA KWA MAMBO YOYOTE,YANİ MAJİ MASAFİ YA MFEREJİ(BOMBA) YAPATİKANE KİLA SEHEMU,SERİKALİ ZA MİTAA ZİKATAZE RAİA WAKE KWENDA MTONİ KUOGA.NA MİTO İLOWEPO İANGALİWE NA KUWEKWA KTK USAFİ WA HALİ YA JUU.

    tukijiuliza kwanini chanjo hizo wazungu wanatengeneza halafu wanakuja kutujaribu sisi?

    jibu ni wazi kwamba maradhi hayo hayapatikani ktk nchi za wenzetu wanojali usafi na kupatikana maji safi na bora,hivyo hizo chanjo wao hawazihitaji.

    wao wanaotuona sisi hatuwezi kuyadhibiti maradhi hayo kwasababu hatuna utamaduni wa kudumisha usafi ndio wameamua kutafuta chanjo ili hata mdudu akikupata maradhi yasikupate.lkn hizo chanjo zenyewe itakuwa ndo kwanza zipo kwenye majaribio lkn kwa vile viongozi wetu tunawaamini sana hawa watu tumeletewa dawa direct tunawapa raia bila kuchunguzwa tena hapa nchini.matokeo yake ni kama hayo


    kwa upande wa minyoo inaambukizwa kwa njia ya fecaloral yani kinyesi na kula.kwa vile bongo maji hayapatikani na wala hatuna utamaduni wa kuweka masink ktk vyoo vyetu.hivyo mtu ak,ishajisaidia ni nadra kunawa mikono atajichambisha na kuendelea na kazı zake wakati huo kumbe ktk hichi kinyesi chake au cha mtu yeyote alıyepıta kama kulikuwa na mayayi ya hao minyoo yanakwenda mwilini na kuleta maradhi.

    kinga ni usafi.

    TATİZO AFRİCA LİNOTUSUMBUA Nİ LOW SANİTATİON. WE DONT CARE WAT WE EAT WAT WE TOUCH HATUJALİ KUEPUKA CONTAMINATION,so maradhi kama hayo na mengıne mengi yataendelea ikiwa serikali haitalitia mkazo hili suala la kudumisha usafi na kupatikana kwa maji,kunawa mikono,malaria,kolera,haitokwisha.

    NEVER

    KUNA TETESI NMESİKİA KWA KUA KUNA MRADİ WA KUDHİBİTİ MALARİA KWA UPANDE WA ZNZ KİLA ANAEKWENDA KUCHEKİ KTK TAASİSİ ZA SERİKALİ BASİ Nİ NEGATİVE NO MATTER HATA KAMASYMPTOMS ZA MALARİA ZİPO,SASA HUKU Sİ KUUWANA AU TUNATAKA KUJİONESHA KAMA MRADİ UMEFANİKİWA HUKU WATU WANAKUFA.TUNAJİPAKA MAFUTA KWA NYUMA YA CHUPA WENYEWE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...