Ndugu zangu,
Baadhi yenu mtakuwa nimekutaarifuni kuhusu kitabu hiki kipya. Nasikitika kukuelezeni kuwa kitabu kimeanza kupigwa vita ya chinichini.

Kwa wale ambao watakuwa hawajakisoma hawatapata tabu kujua sababu. University Bookshop na Dar es Salaam Bookshop wamepokea kitabu lakini sasa inaingia juma la pili hawataki kukiweka 'on dispaly' wala kukiuza.

Watu wakienda kukiuliza wanawaambia hawana taarifa ya kitabu hicho.Nakuombeni ndugu zangu hebu nanyi fikeni katika maduka hayo mpate uhakika wa haya nisemayo Hata hivyo kitabu kinapatikana:


Slip Way

Sea Cliff

Ibn Hazim Mkabala wa Msikiti wa Manyema

Khartan Bookshop Narung'ombe na Swahili karibu na Kariakoo Bureau du Change

Furaha Bookshop Msimbazi na Uhuru

Amnet Bookshop Msimbazi

na Livingstone Bookshop Mkabala na Msikiti wa Kipata


Mjini Tanga Duka la Maalim Masud Br. 18 kwa Pangani Road

Cathedral Bookshop wao wamekirudisha kwa Publisher.


Nini kinawatisha?

Nini kinakera katika kitabu?
Hiki ni kitabu kipya kinachoelezea mchango wa wazalendo waliopigania uhuru.
Kitabu kinaeleza yale yaliyotendeka mwaka 1958 wakati TANU ilipoingia katika uchaguzi wake wa kwanza uliojulikana kama Uchaguzi wa Kura Tatu.
Waingereza waliweka masharti ya kibaguzi yaliyopelekea TANU itishie kususa kuingia katika uchaguzi.

Matokeo yake TANU ilikuwa karibu ijigawe katika mapande mawili hasimu - ya wale wanaounga mkono kushiriki uchaguzi wakiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere Rais wa TANU na wale wanaopinga wakiongozwa na Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Kitabu kimewafufua wazalendo wengi ambao leo wamesahaulika.

Mohamed Said
Mtunzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kutokana na Lugha uliyoitumia hapa kwenye hii taarifa, ninaanza kushawishika kuwa inawezekana hao wanoa kificha au kukirudisha labda wameona kuna mapungufu katika kitabu hicho.Jaribu kushirikisha waandishi wenzio wakipitie kwanza kabla hujaanza kulaumu watu.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  2. Hizo zitakuwa ni mbinu mbaya za Mafisadi kukizima kitabu hicho, unajua wao kila wakati wanakuwa wakijishuku-shuku tu na kuanza kutumia mbinu zao za kimafia kuzima mambo. Lakini sasa hivi sayansi imekua hawataweza kukizima kama walivyofanya kwa kile kitabu cha "UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA"

    ReplyDelete
  3. please someone post a page by page au kitabu kizima somewhere on the blog kwa sie tulio mbali na nyumbani.
    Thanx!

    ReplyDelete
  4. Kama kuna kasoro za mzazi wa ccm tanu basi kitabu kitasahauliza punde.

    ReplyDelete
  5. Mbona hao anaowatetea walikaa kimya bila ya kuyasema?

    ReplyDelete
  6. Nimegoogle jina la kitabu na kugundua ni juu ya itikadi ya kiislam zaidi kuliko siasa! Hata hivyo ningependa kukisoma kwanza kabla ya hukumu! Naye michuzi sijui kama ni walewale au la

    ReplyDelete
  7. Wewe Mdau wa Cardiff humjui mohamed Said ni nani kwenye uandishi.soma kwanza vitabu vyake halafu ndio ukosoe.

    kwa taarifa yako Mohamed Said-Sydney emesoma hapo hapo Cardiff masters yake na ametunga vitabu vingi vya maana.

    jaribu kusoma kitabu chake cha Abdulwahid Sykes tena ametumia kimombo,wewe wa uliye Cardiff huwezi kuandika.

    Mohamed Said usivunjwe moyo na hawa wajivuni wa Cardiff kwa vile hawakujui. tupe email yako utuletee vitabu ughaibuni.

    Hapa UK kilete African bookshop wapo King street-Leicester Square-London utauza bila mizengwe.

    vitabu vyako hakikisha vinafika mikoani isiwe Dar tu.Hongera tuko nawe.tunakukumbuka nyakati ulipokuwa nasi hapa UK.

    Mdau London.

    ReplyDelete
  8. Mdau London, Kama nimetumia lugha ambayo imekukwaza naomba msamaha. lakini kutoa maoni sio lazima kukosoa. Inawezekana nimetumia lugha ambayo mwenzangu umeitafsiri vibaya au tofauti na nilichokuwa namanisha. Ni kweli kwamba mimi simjui Mohamed said, lakini lengo langu la kumwambia ajaribi kuwashirikisha waandishi wengine ni kwa lengo la kupata maoni yao. Kama alikwisha fanya hivyo ni vizuri.Inawezekana kuna kasoro ndogo ambayo kwake yeye kama binadamu anaweza asiione, lakini mtu mwingine akaiona.Kusema kasoro sio maana yake kwamba kitabu ni kibaya. Inawezekana kuna kitu kidogo ambacho kimekwaza watu, ambapo kama kikirekebishwa mambo yanakwenda sawa. Hilo lilikuwa ni wazo langu tu. Sina kawaida yangu kuendeleza mijadala, kwahiyo kama Mheshimiwa Mohamed Said pia nimekukwaza kwa comment yangu naomba msamaha.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  9. MAHALI POPOTE DUNIANI HUWEZI KUANDIKA KITABU KUHUSU MTU AU TAASISI FULANI BILA YA KUISHIRIKISHA NA KUTADHIMINI UKWELI WA MAANDIKO YALIYOMO NDANI UNLESS NI HADITHI YA KUFIKIRIKA, SASA UNAPOANDIKA HABARI TUSEME ZA CCM SI LAZIMA UWASHIRIKISHE WAKUELEZE YALIOENDELEA KATIKA CHAMA CHO HADI HAPO WALIPOFIKA, AU UNAANDIKA KUTOKANA NA STORY ULIZOZISIKIA TOKA KWA WATU PENGINE SI SAHIHI, UNLESS YOU WRITE NEGATIVE ABOUT THE THING, THE YOU CAN WRITE ANYTHING, KUSOMA MASTERS SI TIJA NA WALA SI KTU INAMFANYA MTU AJUWE KUANDIKA VITABU, KUNA WATU HAWANA DEGREE LAKINI WANAANDIKA VITABU VIZURI TU, MMOJA WAO SHABAAN ROBERT WA TANZANIA

    ReplyDelete
  10. wewe unayesema Mwandishi hajawashirikisha taasisi husika una uhakika na unachosema?kwa taarifa yako mohammed Said kwenye kitabu cha Abdulwahid Skyes aliomba interview na mwalimu nyerere zaidi ya mara tatu na ametembea nchi nzima kuhoji au kupata habari mbali mbali.

    kitabu kile kwa wenzetu wangempa Phd amewapitia hadi kina bibi Titi Mohamed.

    na amepitia nyaraka mbali mballi, naomba soma kwanza ndio ukosoe. hiki cha sasa sijakisoma sina comments juu ya hiki ila namjua Mohamed ni mwandishi wa vitabu vingi. publishers wake ni wa uhakika kama MINNERVA WA KNIGHTBRIDGE UK.

    nilimjua Mohamed Said kwenye makala zake gazeti la Rai enzi za 1996.sikusema kwa masters ndio kigezo cha uandishi nimeitaja baada ya kuona mtu anasema yuko Cardiff-UK huko Mohamed Said kafanya Masters.nisingesema ana masters ungesema mwandishi uchwara nimetaja ana masters wewe unaona kama nakukoga.ndivyo tulivyo binadamu.

    pia kwanini wewe usiende kuzihoji hizo taasisi kuwa maneno aliyoandika Mohamed Said yana kweli? kama hayana ukweli kanusheni?

    Mwalimu Nyerere hakuwahi kukanusha na amesoma sana vitabu vya Mohamed Said.

    kama ulikuwa ukimsikiliza Mwalimu mengi amekuwa akiyasema kuwa kuna mchango mkubwa wa wazalendo kwenye harakati zake.watu kama kina mzee Ramia wa BAGAMOYO umewahi kuwasikia?

    MOHAMED naomba email yako au simu namba yako hapa.hongera kwa kazi nzuri hawa wasikunyime usingizi kipaji kakupa Mwenyezi Mungu kitumie hata kama wanaumia.

    ReplyDelete
  11. KWANI KINACHOGOMBA HAPA NI NINI KUWATAJA WATU WALIOCHANGIA MAENDELEO NA KUGOMBEA UHURU WA TANZANIA? NI KWELI KWA NINI WASITAJWE NA KWA NINI MWANDISHI ANASHAWISHIKA KUWA KITABU KINAMIZENGWE YA KUZUWIWA KISISOMWE NA WATANZANIA, KWANI KUNA UBAYA GANI KUMTAJA RAMIA AU SYKES ALIHUSIKA KATIKA HARAKATI ZA UHURU? KAMA KINAZUIWA BASI LAZIMA KINA KASORO. WEWE NDO ULIYOLETA HABARI ZA MASTERS ILI KUONYESHA CREDIBILITY YA MWANDISHI NAMI NIKASEMA MASTERS SI TIJA KATIKA UANDISHI WA VITABU KWANI NI WENGI TU NAWAJUWA DUNIANI AMBAO HAWAJASOMA HATA DEGREE LAKINI WAMEANDIKA VITABU VIZURI TU. UKIPENDA CHONGO USIITE MAKENGEZA. MARA CHUNGU NZIMA NYERERE AMEKUWA AKIWATAJA WATU WALIOKUWA KATIKA HARAKA ZA UHURU NA WALA HAKUFICHA HILO AKIWEMO KAWAWA, TITI MOHAMED, SYKES NA WAZEE KIBAO TU WA BAGAMOYO NA MWANERUMANGO.

    ReplyDelete
  12. Binafsi sikumjua mohamed saidi mpaka nilipokuta mjadala mrefu jamii forum juu ya kitabu chake cha maisha ya abbdulwahidy sykes, samahani kama nitakosea jina. Ikabidi nikitafute kitabu kile. Naomba kukili kuwa hakuna mtu asiyependa kuona haki inadhihirika akampenda mohamed said. Maana alichokielezea katika kitabu kile ni kitu kilicho fichwa tena sii kwa bahati mbaya. Ni kwa makusudi maalum na kwa kulenga kitu maalum, haikuishia hapo nikatafuta kingine cha mzanzibar kharis khasan kwaheri ukolon kwaheri uhuru. Kichwa kilinifumuka nilipojiona kumbe watanzania wengi tumefichwa kitu kikubwa sana katika historia ya nchi hii na kwa mtu aliyemzembe wa kufikilia hawezi kulijua hilo. Sasa ukimuona mtu anakuwa mbishi kwenye tafiti zilizothibitishwa huwezi mtoa katika kile anachokiamini mpaka kisemwe na yule anayemuamini yeye. Lkn pia kuna isemi mmoja wa malcom x kuwa, mtu asiyekijua kitu au jambo ni rahisi kwake kulipinga, wadau tuache marumbano cha msingi tutafute kitabu halafu ndio tuanze kukitoa kasoro sio habari za kuhisi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...