Wikiendi hii kipindi moto cha Mitikisiko ya Pwani cha Times FM kimetimiza miaka 5 tangu kilipoanzishwa kipindi hicho ambacho hurushwa hewani kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 6 mchana hadi 9 Alasiri na mtangazaji wake mahiri Dida.

Kilele cha sherehe za kipindi hicho zitakuwa na Tamasha kubwa la muziki wa taarab tamasha hilo litafanyika katika ukumbi wa PTA HALL viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa ambapo jumla ya vikundi 9 maarufu vya taarab vitashiriki vikundi hivyo ni pamoja na Jahazi, East Africa Melody, Coast Modern Taarab,New Zanzibar Star, Five Star, Tandale Modern Taarab, Super shine na Tanzania One Theatre. Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Kazi Ajira na Vijana Mh Juma Kapuya.
Mbali na burudani hiyo pia kutafanyika mashindano ya kusaka vipaji vya waimbaji wa taarab na washindi 7 watapatiwa mikataba maalum ya kazi katika vikundi watakavyoimbia siku hiyo ya mashindano wadhamini wakiwa ni Zain T Ltd na TBL na kiingilio itakuwa shilingi 5000 na 10.000 viti maalum tamasha litaanza saa 2 usiku
Mtangazaji moto wa mitikisiko ya pwani ya times fm, Dida, akikata keki studio

Dida akilisha keki mmoja wa wasanii wa taarabu
waimbaji wa taarab toka Melody, Five Star na Tandale wakiwa na mtangazji wa kipindi hicho Dida na Meneja wa Promotions wa Radio Times fm Amani Missanah (mwenye fulanazzz ya blue) wakiwa studio za Times fm kuadhimisha kutimiza miaka 5
waimbaji wa taarab toka Melody, Five Star na Tandale wakiwa na mtangazji wa kipindi hicho Dida


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongera Mitikisiko ya Pwani na watangazaji wake bila kuwasahau mashabiki wake!!! Kidumu kipindiiii,kidumuuuuu!!! Amani Missanah mzee wa Pilot talk!!

    ReplyDelete
  2. 5 year's si mchezo

    ReplyDelete
  3. *sigh*

    YEARS not YEAR'S

    ReplyDelete
  4. ooh kumbe uyu ndo Dida???

    ooo ok

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...