Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimvisha medali Salumu Athumani baada ya kituo chao cha Tacoda kuibuka washindi wa kwanza katika mchezo wa miguu katika tamasha la michezo la Vodacom Foundation la share & care lililofanyika kwenye kiwanja cha Shekhe Amri Abeid mjini arusha na kuudhuriwa na zaidi ya watoto yatima 550.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimpongeza mmoja wa washiriki waliofanya vyema


Rajabu Hussen mmoja wa watoto waishio katika mazingira magumu akishiriki katika mchezo wa kuruka juu( Long jump) katika tamasha la michezo la Vodacom Foundation la share & care lililofanyika kwenye kiwanja cha Shekhe Amri Abeid mjini arusha na kuudhuriwa na zaidi ya watoto yatima 550.
Janeth Shirima mmoja wa watoto waishio katika mazingira magumu akiibuka kuwa mshindi katika mbio za kilometa 100 kwa upande wa wasichana katika tamasha la michezo la Vodacom Foundation la share & care

Watoto waishio katika mazingira magumu mkoani arusha wamesifia tamasha la michezo la Vodacom Foundation lililoshirikisha takribani kaya 25,na kuandaliwa na Vodacom Foundation
Akifunga tamasha hilo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda aliwapongeza waandaji kwa kuwakumbuka watoto yatima na kuwataka waendelee kuyaanda matamasha kama hayo kila mwaka,kwani ni njia mbadala ya kuibua vipaji na vitakuwa faida ya taifa letu kwa siku zijazo.
Nae Mkurugenzi wa mahusiano ya kijamii wa Vodacom Tanzania ambao ndiyo waandaaji na wadhamini wa tamasha hilo wakishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali alisema tamasha hili la michezo ambalo limefanyika hapa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid ni muhimu sana kwa vijana na watoto waishio katika mazingira magumu wa mjini Arusha na ninapenda kuahidi kuwa hatutaishia hapa tu tutagusa kila mikoa kwa mwakani kwani natambua umuhimu wa michezo kuwa ni afya,mshikamano na uleta undugu katika jamii, ninauhakika tutaibua vipaji na vitakuwa vioo kwa jamii ya Mtanzania.


Makamba amesema kuwa tamasha hilo la michezo ni sehemu ya kampeni ya mfuko wa Vodacom Foundation ya Share & Care ambayo ina lengo la kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu kwa kipindi hiki cha kuelekea kwenye sherehe za mwisho wa mwaka.


“Lengo la tamasha hili la michezo ni kuwakutanisha pamoja na kuwapa moyo na matumaini watoto hawa na kuweza kujiona kuwa wanajaliwa katika jamii zao zinazowazunguka”, amesema.


Amesisitiza kwamba tamasha hili la michezo limesaidia katika kuwaleta watoto wapatao zaidi ya 550 washio katika mazingira magumu kwa pamoja na wajisikie fahari na ilikuwa ni sehemu muhimu ya kuwapatia fursa ya kuonyesha vipaji vyao,

Mfuko huo umetumia kiasi cha shilingi milioni 25 kuandaa na kudhamini tamasha hilo la michezo.
Makamba amesema kuwa michezo hiyo pia imewafanya watoto hao kuwa na ari ya kujiendeleza kimichezo na hivyo kubadilisha mazingira yao ya kila siku.

Miongoni ya michezo iliyokuwepo ni (long Jump), kuvuta kamba, mpira wa miguu,riadha, mpira wa mikono kwa wasichana na kikapu na mingineyo mingi.

Tamasha hili la michezo ni lakihistoria na lilifungwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo na kuweza kuwapatia medali na fedha tasilimu kwa wale waliofanya vizuri katika tamasha hilo.Ambapo katika mchezo wa mpira wa miguu kituo cha Tacoda kiliibuka washindi na kujinyakulia fedha tasilimu shilingi laki moja na nusu(150,000) na kituo cha Hokodeko waliibukawashindi wa pili na kujinyakulia kitita cha shilingi laki moja(100,000)na washindi watatu ni kituo cha Rafiki one na kuondoka na Kiasi cha shilingi elf hamsini (50,000)

Nae mshindi wa kwanza kwa upande wa wasichana walioshiriki mbio za kilomita 100 Tausi Said (12) wa kituo cha shaloom mkoani Arusha alisema anashangaa miaka yote mashirika kama haya yalikuwa wapi kuandaa tamasha la michezo kama la leo?alisikika akihoji, na kusema kwa kweli nawashukuru Vodacom kwa kutukumbuka sisi watoto yatima kwa kupitia njia hii ya michezo na ninatoa wito kwa mashirika mengine yaweze kutusaidia na kutukumbuka kupitia michezo,kwani nimejisikia kuwa na Furaha ya ajabu kwa kukutana na watoto wenzangu walio wengi na siyo kwa mabaya bali ni kwa kucheza na kufurahia na kushindana kwa hali ya upendo na mshikamano.


Baada ya tamasha hilo Vodacom Foundation iliendelea na kampeni yake ya share & care na kuweza kutoa misaada kwenye vituo vya watoto yatima na waishio katika mazingira magumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Michuzi wacha utani.

    Hizo ni mita 100 sio Km 100. Hata marathon ni km 40 na ushee.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  2. Mbio za kilometa 100 hiyo ni kali amevunja rekodi ya dunia!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Bro Michuzi, hao watoto walikimbia kilometa 100 au mita 100?

    ReplyDelete
  4. Oh Uwanja kama nilivyouacha almost Miaka. Chipukizi hapo tulipiga tizi kweli, halaiki na riadha...

    ReplyDelete
  5. Ni noma alikimbia km 100,hata semenya hawezi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...