Kikosi Cha Taifa Stars
Kikosi cha Rwanda
Kikosi cha Rwanda
Makapteni wa timu zote mbili wakisabahiana mbele ya waamuzi waliochezesha mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars' Mrisho Ngasa (kulia) akimtoka beki wa timu ya Rwanda 'Amavubi' Nghabo Albert katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Jerry Tegete akijaribu kupiga shuti wakati wa mchezo.
Kipa wa Amavubi, Ndayishimiye jeanluc akijarribu kuokoa kiki iliyopigwa na Mrisho Ngasa bila ya mafanikio.
Beki wa timu ya taifa ya Rwanda, Nghabo Albert akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Stars, Juma Jabu katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) ulliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1
Jooooob true true! Hata Rwanda wajemeni? Afu eti uwanja wa omu? Safari ni mureeefu true true! Duh. Embu angalia ilo likisimo (lilivyoduwaa). Uyu na utaalamu wake wa mabua wote huo bado ajuhi kuwa angelimteua Kaseja angelikuwa anasmaili nau! Ha ha haaa. Eli kamkataba kake kamesharegea! He heee!
ReplyDeleteDayasipora
Mdharau mwiba.
ReplyDeleteHakuna uwiano wa soka na ukubwa wa nchi. Chezea hengine siyo Rwanda.
hahahahah sawa sawa anony hapo juu jamaa anaonekana ni mvivu wa kufkiria saana afu kune soka kila kitu cha wezekana daika 90 lazima ue tayari kwa kila kitu.kuidharau rwanda hata mfaransa au mjinga yeyeto ka ww hapo juu dayasipora endeleeni sie tunasonga kama kawa na mtalijua jiji na wajinga wenzio ww dayasipoara.jamaani ka rwanda ketu kametiotahidi safari hii ngoja tusubirie kagame cup a.k.a cecafa tuone inakuaje
ReplyDeletemdau kigali makazi boksini kusaka chake
Taafa Stars nikama kifaranga cha kuku kilichohaidiwa nyonyo, toka enzi za kichwa cha mwendawazimu maksi hazimo,
ReplyDeleteWachezaji wamejaa misifa tu,pamoja na viongozi wao Wanazidi tu kuchanika na Pesa za Uwanja na Wafadhili, hata tovuti hakuna.
Niwakati wa kusimamia kidete Soccer Academy sasa sio hao mashaibu.
Mdau,
Barcelona
KUIFUNGA SOMALIA NCHI ISIYO NA LIGI YOYOTE WALA SERIKALI AKAONA NI KIPIMO TOSHA, AKAJISIFU KUWA NITAONDOKA TZ NA KUWAACHIA ZAWADI KUBWA, NAYO NI UBINGWA WA CAN. SASA SIJUWI YUHALI GANI? MAMBO NDO HAYO JAHAZI LISHAANZA KUTOTA
ReplyDeleteWadau mi nadhani sisi watanzania ni walaini sanaaaa (Nimejaribu kutumia neno baridi)sijui tunaweza kujivunia nini! Hatuna dila tupo tuuu mladi kumekucha baraka ya kuchekeana tuu! Inauma sanaaa!
ReplyDeleteWe Maximo zimo kweli? utamuwekaje Mussa Hassan Mgosi (Mussa Magoli) benchi halafu umuingize kipindi cha pili. Unategemea magoli yataingiaje?
ReplyDeletetuachane na hao wachezaji wa uswazi wavuta bangi, tutafute vipaji vijijini, vijana wa copa cocacola tuwatumie tutapata timu nzuri. hawa wameshindikana, hata kama tutamleta mourinho kuwafundisha hawa atachemsha tu.
ReplyDeleteWamejitahidi ila tatizo kubwa kuna siasa ambazo hazifai kwa kuendeleza soka. Upangaji wa timu mara nyingine uanaleta mashaka kama vile kuna wau wanasema fulani lazima acheze. Kama siyo hivyo, kwa kocha makini hawezi kumwanzisha benchi Mgosi, mkumbuke kuwa ktk nchi zinazojua soka mfungaji bora ni muhimu kwa taifa na hata watu wa nchi nyingine wanapotaka kucheza na timu wanapitia mchezaji mmoja mmoja wa timu pinzani kuona profile zao, sasa nashangaa kwa TZ sijui kocha nalijua hili ama anajitahidi tu kupanga kufurahisha watu, imefikia wakati soka liendeshwe kisayansi zaidi na kiukweli kuliko kuingiza sisa ambazo hazina maana, katika hili tusubiri kocha nayekuja ambaye hatokumbwa na sisa hizi na ubishi ambao hauendelezi soka. Mpeni Papic muone atakavyofanya, anajua soka ndiyo maana mara zote ingawa yuko Yanga hatosita kusifia kizuri cha timu pinzani, huyu anjua soka na si majungu
ReplyDeleteHivi jezi za stars zimebadilika? Naona katka mechi na Rwanda jezi zina nembo ya adidas.Hawakuvaa za kawaida kama zilizovaliwa na Ngorongoro Boys Ijumaa
ReplyDeleteHivi jezi za stars zimebadilika? Naona katka mechi na Rwanda jezi zina nembo ya adidas.Hawakuvaa za kawaida kama zilizovaliwa na Ngorongoro Boys Ijumaa
ReplyDeletejabu si mshambuliaji ni mlinzi wa pembeni
ReplyDeleteFRANKLY I LOVE TAIFA STARS LAKINI HIZI JEZI HAZINA MSHIKO!!!
ReplyDeletePLEASE TFF HUYO MZAMINI APELEKE HIZO RANGI MNAZO TAKA ZA JEZI ZA TAIFA KWA WATAALAMU WA KUDESIGN WALOBOBEA WASEZIINI JEZI ZA MAANA. HIZI JEZI HAZIVUTII, HALAFU TUACHE USIMBA NA UYANGA, JEZI ZA NJANO NI MZURI KWA FAIDA MOJA ZINAFANYA WACHEZAJI WAONEKANE, SISI WEUSI THEN TUNAVAA RANGI YA BLUE ILIYOFIFIA NA NYEUSI..CHECK MSAJIGWA HAPO???? KISA WASHIBIKI WA SIMBA WATACHUKIA??? HILI NI TAIFA SIYO SIMBA NA YANGA, AU JIE TFF HAMJUI KUWA RANGI INAYONG'ARA UWANJANI INASAIDIA KULETA USHINDI. BRAZIL WANAJUWA HILI, NDIYO MAANA HAWAVAI JEZI ZA KIJANI AMBAYO IMETAWALA KATIKA BENDERA YAO, WANAVAA NJANO ILI WAONANE VIZURI....NA WANAVUTIA UWANJANI
CHITU