Kibopa nambari moja duniani Bill Gates na mai waifu wake Melinda Gates leo wametembelea kituo cha utafiti cha Ifakara tawi la Bagamoyo kuangalia shughuli za utafiti wa chanjo ya Malaria unaofanywa na kituo hicho. Bill na Melinda Gates wametoa msaada kwa dola bilioni 10 kusaidi mapambano dhidi ya Malaria na ugonjwa wa Trachoma hivyo ni wadau muhimu hapa nchini na wanastahili heshima zote, japo mwenyewe hapendagi kuuza sura wala kujulikana kuwa yupo mahali. Globu ya Jamii kama kawaida yake ya kuwa mbele hatua kumi katika habari inakupa taswira za Bill Gates na mai waifu wake akiwa na watafiti na wafanyakazi wa Kituo Hicho.
Bill Gates akiwa na wafanyakazi wa Ifakara Health Institute kituo cha Bagamoyo
Bill Gates akiongea na watafiti na wafanyakazi wa kituo hicho
Bill na Melinda Gates wakiweka sahihi kitabu cha wageni Bagamoyo leo
Bill na Melinda Gates wakipata maelezo juu ya tafiti za Malaria kituoni hapo
Bill Gates akiongea na watafiti na wafanyakazi wa kituo hicho
Bill na Melinda Gates wakiweka sahihi kitabu cha wageni Bagamoyo leo
Bill na Melinda Gates wakipata maelezo juu ya tafiti za Malaria kituoni hapo
Bill Gates akipiga stori na watafiti na wafanyakazi wa kituoni hapo
MWANDISHI WETU ALOCHAPISHA HII TAARIFA FUATILIA VIZURI HUYU BWANA SIE TENA TAJIRI NR MOJA DUNIANI .....KASHAPIKULIWA ZAMANI TU
ReplyDeleteBill Gates siyo kibopa nambari moja duniani, ni nambari mbili. Nambari moja ni Carlos Slim Helu wa Mexico.
ReplyDeleteThanks.
jamani hiyo ela nimeshindwa kupiga hesabu ina maana ni Tshs 15,500,000,000,000 au nisaidieni
ReplyDeletemichuzi dola bil.10 ni sahihi umeichukua hiyo? ni nyingi si mchezo
ReplyDeletelabda itakua ni million 10 na sio bil,
Hawa jamaa kutalii majumba yao unahitaji helicopter dadadeki!
ReplyDeleteKatika watu nisiowaelewa ulimwenguni nadhani huyu naye yupo, Jamaa huwa yupo yupo tu na yeye anajichanganya kokote pale bila kujali ni kundi la watu gani. Kaka mimi napiga Kazi Mall nilikuwa napiga stori na tajiri mmoja lakini sikumjua kabisa baadae wafanyakazi wenzangu ndio wananiambia na jamaa alikuwa anaijua Tanzania balaaa
ReplyDeleteZitumieni hizo pesa za msaada kwa malengo mliokusudia
ReplyDeleteIli wengine waje na matokeo yaonekane inshallah
Kila la kheri kituoni hapo
Mpili Rama Mpili
Ni kweli Bill Gates ni kiboba #2 duniani. Hii imetokana na yeye kugawa pesa nyingi kusaidia maskini tofauti na kibopa #1 Carlos Helu Slim(Lebanese Mexican Billionaire). Carlos yeye amesema sio Santa Clause so hataki mambo ya kugawa pesa zake kwa maskini. Anadai yeye anaanzisha kampuni ambazo zinatoa ajira kwa maskini. Hivyo ndio anavyosaidia maskini na sio kama Bill Gates.
ReplyDeleteEniwei, Bill Gates nae ni bepari mzuri sana msiomuone yuko simple simple. He is one of the Greediest Capitalist just like Gordon Gecko.
Long Live Free Market Capitalism!
wabongo bana teh teh teh wanabishana eti huyu sio tajiri namba moja sasa hata akiwa tajiri namba 10 unafikiri ni suala la mchezo gates ana mihela sio mchezo na nashindwa kuelewa hao waandalizi wa shughuli hiyo yani walishindwa kuweka kiti hapo wanapotia saini ili waweze kukaa bongo juwa ni kali sana mtu anaweza kuanguka kuweni wastaarabu mnapokea milioni 10 dolla mnashindwa kumkaribisha mtu kwenye kiti huyo mtu hata obama mwenyewe anampatia heshima sababu sio mtu wa kuchezea
ReplyDeleteNa huyo Carlos Slim hafui dafu kwa Hosni Mubarak, na wote wawili wamepata pesa kwa njia chafu. Hivyo tukiangalia tajiri zaidi ya wote duniani ambaye amepata mali yake kwa njia safi anabakia kuwa Bill Gates. Isitoshe Carlos huwa hatoi misaada ya kijami japo wananchi wa Mexico wana shida balaa, jamaa anakula pesa zake bila kuwasaidia wananchi wenzake hata senti moja year-in-year-out. Bill Gates juu!
ReplyDeleteziende na zanzibar hizo bilioni
ReplyDeleteMbowe nae ageiga Bill Gate kwa kutoa magari yake bure kwa CHADEMA!!
ReplyDelete