Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akishiriki katika shughuli ya uchimbaji wa
barabara ya Bureni Iramba-Kwanamburi
Mmea aina ya Mrungi umekutwa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule ukiwa umestawi.
Na Mathias Canal, Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule
amejumuika na wananchi wa Kata ya Vudee katika shughuli ya uchimbaji wa
barabara ya Bureni Iramba-Kwanamburi iliyopo katika kijiji cha Bureni
Iramba.
Dc Staki amejitokeza
katika shughuli hiyo ikiwa ni muendelezo wa kujumuika pamoja katika
shughuli za maendeleo ya wananchi na kuwahamasisha kujitokeza katika
kufanya Kazi za maendeleo ya vijiji vyao na kuwafanya wananchi kuiamini
serikali yao chini ya Rais wa serikali ya awamu ya tano Dkt John Pombe
Magufuli.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Dc Staki
amewataka wananchi wa kata hiyo kushirikiana na serikali katika
kuchochea shughuli za maendeleo kwani muda wa kampeni umemalizika hivyo
kwa sasa ni wakati wa kufanya Kazi kwa bidii ili kuimarisha kauli mbiu
ya serikali ya Hapa Kazi Tu.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi
waliopata nafasi ya kuzungumza n kuuliza maswali wamempongeza Mkuu huyo
wa Wilaya kwa namna ambavyo anashiriki shughuli za maendeleo hivyo
wamemuahidi kumuunga mkono.
Wananchi wa maeneo hayo wametakiwa
kujihusisha na shughuli za maendeleo kwa kulima mazao halali ya biashara
ikiwemo kulima tangawizi na kuachana na mazao haramu kama ulimaji wa
mirungi.
Mara baada ya mkutano huo wa hadhara Mkuu huyo wa Wilaya
aliongozana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo walielekea
katika kijiji cha Kisesa kwenye shamba la mkulima Bw Johnson Charles
Mshana ambaye anajihusisha na kilimo cha Mirungi ambaye pia alikataa
Barabara na nguzo za umeme wa Tanesco zisipite shambani kwake kwa ajili
ya kuboresha shughuli za maendeleo katika kata hiyo ya Vudee na maeneo
ya jirani.
Mara baada ya kufika katika shamba hilo mkulima huyo
hakuwepo jambo lililopelekea kukamatwa kwa binti yake ambaye alikutwa
kwenye shamba hilo la Mirungi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...