Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula (pichani) amewataka wananchi wa Kijiji cha Losoito, kuitunza na kutohujumu miundombinu ya maji yaliyowezeshwa na kampuni ya TanzaniteOne.

Mhandisi Chaula aliyasema hayo juzi alipofanya ziara ya siku moja kwenye kijiji hicho baada ya kupatiwa taarifa kuwa kuna baadhi ya watu wameharibu miundombinu hiyo kwa kukata mabomba.

Alisema miundombinu hiyo imewezeshwa kwa pamoja na kampuni ya TanzaniteOne na Serikali kwani wanamiliki mgodi huo kwa asilimia 50 kwa 50 hivyo jamii inapaswa kuyatunza kuyathamini na kuyalinda maji.

Alisema atamchukulia hatua mtu yeyote atakayekamatwa akiharibu miundombinu ya maji kwani wananchi wa eneo hilo kwa muda mrefu waliteseka kufuata huduma hiyo umbali mrefu hadi Mirerani.

“Nimeambiwa awali kuna mama alishajifungua njiani wakati akifuata maji na baba wa kimasai akakata kitovu cha mtoto kwa kutumia sime kasha leo mtu anaharibu miundombinu hii,” alisema mhandisi Chaula.

Mkazi wa Kijiji hicho, Magdalena Peter alisema anashukuru kampuni ya TanzaniteOne kwa kuwezesha mradi huo wa maji ila bado kuna changamoto ya upatikanaji kwani wanayapata mara mbili kwa wiki.

“Awali tulikuwa tunapata maji hayo kwa wakati fofauti na tulivyokuwa tunatembea kilomita 40 hadi Mirerani ila hivi sasa tunawakati mgumu baada ya tenki hilo kupasuka,” alisema Peter.

Ofisa mahusiano wa kampuni ya TanzaniteOne, Halfan Hayeshi alisema anaomba apewe muda wa wiki mbili ili ahakikishe anafanyia matengenezo sehemu za miundombinu iliyoharibika eneo hilo.

“Nitakuja na mafundi wiki ijayo ili waangalie na kuikarabati miundombinu hiyo na pia tutanunua tenki lenye ujazo wa lita 10,000 tofauti na hili la lita 5,000 linalotumika hivi sasa,” alisema Hayeshi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...