Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kuwa viongozi wa siasa waige mfano kwa viongozi dini kujenga tabia ya kukutana mara kwa mara wanapoona matatizo yanapoibuka katika jamii ambayo yanaweza kuvuruga umoja wetu.

Jaji Warioba ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mashauriano juu ya Umuhimu wa kuhimiza Amani na Umoja nchini, amesema kuwa viongozi wa dini wakiona mambo hayaendi sawa huwa wanakutana na kujadili lakini viongozi wa siasa hawafanyi hivyo.

Amesema kuwa viongozi siasa wawe tayari kukutana na kujadili mambo ambayo yanaashiria kuvunja umoja wetu na sio kila mtu kutumia vyombo vya habari kuzungumza juu matatizo yanayotokea.

"Tuache malumbano kwa mambo ya msingi tofauti za vyama vya siasa vinaweza kuturudisha nyuma , ulinzi wa nchi hii ni jukumu la kila mtanzania tena mzalendo" amesema Jaji Warioba

Jaji Warioba ameongeza kuwa kuna mauaji ya watu wenye Ualbino , Migogoro ya Wafugaji na Wakulima mkoani Morogoro hayo ni mambo watu lazima wanasiasa wakutane na kujadili mambo hayo.

Amesisitiza amani ikivurugwa hakuna mtu anaweza kuirudisha kwa wepesi hivyo ni lazima imani ilindwe kwa nguvu zote kwa kuachana na tofauti za kisiasa.
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza wakati alipokuwa akifungua Mdahalo wa Mashauriano juu ya Umuhimu wa kuhimiza Kulinda na Kudumisha Amani na Umoja Nchini Tanzania lililoandaliwa Tasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation.
  Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia na Prof Mwesigwa Baregu.
 Viongozi wa kisiasa na Dini mbalimbali wakifatilia Mdahalo wa Mashauriano juu ya Umuhimu wa kuhimiza Kulinda na Kudumisha Amani na Umoja Nchini Tanzania
 Wajumbe waliohudhuria Mdahalo wa Mashauriano juu ya Umuhimu wa kuhimiza Kulinda na Kudumisha Amani na Umoja Nchini Tanzania
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mdahalo wa Mashauriano juu ya Umuhimu wa kuhimiza Kulinda na Kudumisha Amani na Umoja Nchini Tanzania.Picha Zote na Humphrey Shao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...