Hapa ni nje ya relwe stesheni dom ambako chinga wa kigogo wanalamba vichwa hasa vya kizungu kwa bidhaa zao adimu. Halafu kuna mshikaji kanifowadia habari njema hii. mie inglishi iz noti richebo hivyo naomba mtransleti wenyewe. stey tyunnnd!



Proud Tanzanian


I, as a Tanzanian am proud to have achieved another milestone...The
Tanzanian Shilling is now equal to more than 1,300 to 1 US$!!!!

Congratulations to all of us Tanzanians for:

1) Using Chinese toilet paper rather than Rexa or Tanpack...
2) Buying ice cream made in Kenya or South Africa rather than Azam (I
agree Ole is not good !!!)
3) Using Omo rather than Foma
4) Eating Heinz baked beans rather than Dabaga or Red gold
5) For using Shoprite as your favourite shopping destination since
"expired" South African goods are better than Tanzanian products
6) For using Anchor butter/cheese on your bread rather than ASAS or
Serengeti
7) For using Colgate and Close up as they make your teeth brighter
rather than Whitedent
8) For drinking Heineken and Red Bull rather than a good old Kili....its
a matter of image in it!
9) For drinking St.Anne and Overmeer than Dodoma wine
10) For using Farmer's choice sausages than Beef Vienna from Arusha
11) For using Kangaroo matches than KIBO match

.....and the list goes on....

Come on guys wake up....Its time for a change......BE TANZANIAN BUY
TANZANIAN....

And a request to the expatriate community...especially South
Africans...please change your mind set and help Tanzania grow by
supporting local products...

Regards

A true Tanzanian.......

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2006

    Michuzi, hiyo siyo habari njema bali ni jinsi hela yetu (Tsh)inavyoshuka kutokana na kuamini vitu vinavyotengenzwa nje ni bora kuliko vya nyumbani.Ni aibu na mbaya sana kwenye uchumi wetu.
    James

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2006

    Jamani ili bidhaa zetu zishindane zinabidi ziwe na viwango bora na hata kuzidi hivyo vya nje, hapo kila mteja atavisaka kwa udi na uvumba na vya nje vitadorora na mwishowe kupotea kabisa.Lakini kama tunaboronga kwenye Quality,standards,production,distribution na hata advertisement[mfano Dodoma wine ni bomba lakini upatikaji wake?!Binafsi huwa nikija bongo huitafuta ili kuja kutoa zawadi huku ughaibuni na kuifagilia lakini sijaziona zaidi ya miaka iendayo kama 10 hivi mwishowe huishia kununua konyagi ambayo yenyewe upatikanaji wake hauna matitizo.]Tusilaumu wakati wenyewe tunaboronga!Kwenye uchumi hakuna uzalendo ila ni viwango tu na kuchapa kazi mwendo mdundo hapo mafanikio tutapata,tena wateja watatufuata wenyewe!!
    Ahsanteni.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2006

    Inabidi kueleimisha wananchi/taifa na pia baadhi ya bidhaa zisiruhusiwe nchini....nchi nyingi sana zilizoendelea zinapiga vita bidhaa kadhaa za nje na hivyo kuruihusu tu bidhaa chache na hadimu kuingizwa nchinoi kutoka nchi za nje...Elimu kwa wananchi na serikali pia inawajibu kureview orodha ya bidhaa za kutoka nje na kuweka vizuizi ili kuboost bidhaa zinazozalishwa nchi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2006

    Mtu aliyeandika hiyo article kwa kiingereza nadhani uwezo wake ni mdogo sana katika mambo ya Int'l Finance , kwa hiyo kwa mtazamo wako unadhani sababu inayofanya thamani ya shilingi izidi kushuka ni kutokana na wananchi kutonunua TZ products tuu ?

    Hivi unajua ya kuwa tunaishi katika Free market ambapo ni lazima makampuni ya kitanzania yashindane na makampuni mengine katika price na quality ? Marekani leo makampuni makubwa kama GM yanataka kufungwa sababu yanashindwa kushindana na Japanese car makers. kwa nini watanzania tunapenda kumtafuta mchawi tuu kila siku !

    Vile vile sisi kama wazalendo tuna export nini ? Wewe audhani ni poor policy za viongozi wetu ndio zinapelekea kushuka kwa thamani?

    Acheni mambo ya kitoto kama mnatka watu wanunue bidhaa za kitanzania basi ni lazima kwa hayo makampuni kuacha kumignore customer wainvest mahela mengi kwenye research and development ........lazima wazalishe bidhaa zenye quality kubwa and they must lower price.

    ReplyDelete
  5. jamani ni kweli kwenye bidhaa nyingine huwa tunafuata ubora lakini tuangalie vitu kama OMO COLGATE, ICE CREAM and MILK,BEER, MATCHES yaani inatia aibu wakati vitu vyetu vina ubora zaidi,yaani kama kuana watu siwapendi bila\ kuficha ni wakenya

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2006

    Swali kwa anony wa saturday, 29, 7:38:14am, wewe naona umesoma intenationale financia, pamoja na kwamba umeshindwa kuilezea badala yake ukangaka kama mbogo.

    Ukiimport sana kila kitu hata chungwa linalopatikana Kabuku pale Tanga, uchumi wako unakuwaje?

    Nafikiri huyu jamaa alichojaribu kutuonyesha ni kwa jinsi gani tunavyotumia pesa zetu (ambazo zinabadilishwa na south na wengineo na kupeleka kwao hivyo kuzitoa kwenye mzunguko wetu wa pesa). Je katika hiyo elimu yako ya int'ln finance huwezi kushusha thamani ya Tshs? kwa kufanya import bila export ambapo inawezekana serikali haijaelimisha ipasavyo watanzania wafanye export(mkakati kwa ujumla)?

    Tunaomba utuelimishe mtanzania mwenzetu ili tupate ufahamu na kupata uwezo wa kukuza uchumi kwa ujumla.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...