treni stesheni ya dom. hivi sasa treni ya bara inaishia dom, na abiria hutelemka kukwea mabasi. hii ni kutokana na uhaba wa mabehewa na injini na pia kuna matengenezo ya reli kati ya dom na dar kwa sasa hadi lini haijulikani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2006

    Ndani ya Tanzania kumbi za starehe zinaota kaka uyoga, iPod zinazagaa kama mchwa kichuguuni, lakini treni iliyokuwa inafika kigoma kwa zaidi ya miaka 80 iliyopita, inaishia Dodoma. Viwete wa akili bado wanasema "bongo bwana, kumekucha, maendelo siku hizi" Pumbavu, maendeleo ya ujinga. Hakuna mabehewa, mapesa kibao yamejenga ukumbi wa bunge ambao haukuwa unahitajika kwa sababu ukumbi wa zamamni ulikuwa unakidhi mahitaji ya ki-bunge. Cha ajabu hakuna atakayewajibishwa.

    ReplyDelete
  2. Hili gari moshi bora liishie huko huko maana Dar kila siku lilikuwa linaishia kugonga gonga hovyo mikweche ya watu,kazi ilikuwa ukutane na que ya magari halafu uwe umenasa katikati ya reli halafu lenyewe ndio liwe linaingia kaazi kweli kweli, kama mtu anataka kwenda Dom mabasi kibao kila saa yapo, sasa hivi kwenye reli kwa raha zetu ukifika unakatisha tu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2006

    jamani hebu JK wafanye la amana kuhusu transpot in Tz yaani tushukuru mabasi sio treni ni ovyooooo !! ukiangalia nchi za wenzetu reli wanatilia mkazo inakwua moja ya usafiri unaohesabiwa daily sio kwetu daa!!! kumezidi na kama unakaa mikoa ya mbali ndio ulie tu na barabara ya dom dar mhh basi tu airport ya dodoma imekufa sasa makao makuu gani hata njia ya kufika hapo ni kimbembe!! inaboa

    ReplyDelete
  4. Hivyo kwa nini usafiri wa reli Tanzania usifungwe tu tukawa kama Burundi tu? Huu si upuuzi tu jamani kutukanana tu huku sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...